Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-09 16:31:31    
Shughuli muhimu za wahudumu wa usafi na wakulima katika mwezi May

cri

Utalii ni shughuli muhimu katika kipindi cha likizo ya May Day nchini China, ambapo watu wengi sana wanapenda kutalii sehemu mbalimbali. Kwenye sehemu ya utalii yenye mandhari nzuri ya mlima wa Manjano watu wanaweza kuwaona wahudumu wa usafi waliovalia vizibao vya rangi ya manjano wakitunza usafi wa mazingira katika njia za wapitazo watalii. Wafanyakazi hao wanachukulia mlima wa Manjano kama ni nyumba wanayoishi na kuwepo wao katika njia za huko kila siku ni kama marafiki wakubwa wasioweza kuachana, kila siku wanafanya kazi za kutunza mazingira kwenye mlima wa Manjano bila kujali uchovu.

Idadi ya watalii ilianza kuongezeka kwa wingi kuanzia katikati ya mwezi Machi, na ilifikia kiasi cha watalii elfu 10 kwa siku mwishoni mwa mwezi Aprili, katika siku 4 za mwanzo za likizo ya siku kuu ya May Day, idadi ya watalii waliotoka nchini na nchi za nje ilikaribia elfu 90. Ongezeko kubwa la idadi ya watalii kwenye mlima wa Manjano, pia limesababisha kazi kubwa kwa watunza mazingira wa huko.

Bw. Shu Shengting ni mfanyakazi wa shirika la utunzaji wa mazingira la sehemu ya Beihai kwenye mlima wa Manjano, kazi zake hasa ni kuweka usafi kwenye barabara itokayo hoteli ya Beihai hadi mlima Shixinfeng. Alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa kila siku anaanza kufagia barabara kutoka saa 12 asubuhi, na kuondoa virundo vya takataka mnamo saa 12 jioni, wakati ambao watalii wameondoka kwenye mlima wa Manjano, kila siku anafanya kazi kwa saa zaidi ya 10, na karibu kila siku mchana anakula njiani chakula alichochukua asubuhi kutoka nyumbani.

Bw. Xie Rongwu pia ni mfanyakazi wa shirika hilo la utunzaji wa mazingira isipokuwa kazi zake ni kuokota takataka zilizotupwa kwenye mitelemko ya milima, hali akining'inia kwa kutumia kamba aliyojifunga kiunoni kutokana na kukosa njia ya kufikia katika mitelemko hiyo. Mwandishi watu wa habari alimuuliza, kama kazi zake hizo ni za taabu, alisema, "Kazi zetu si rahisi, lakini si kitu, ilimradi watalii wanaona mazingira ya mlima wa Manjano ni mazuri na safi."

Habari zinasema, katika kipindi cha mapunziko ya siku kuu ya May Day, wahudumu wa usafi wa mlima wa Manjano wanafanya kazi kwa utaratibu mzuri, mchana kuna watalii wengi, hivyo wanaokota takataka kwa haraka na kuhakikisha hakuna takataka zinazozagaa kila wakati. Kiongozi wa idara hiyo alisema, watunza mazingira wanafanya kazi kubwa, kila siku wanafanya kazi kwa saa zaidi ya 12, na kila mhudumu anainama mara kiasi cha elfu 10 kwa siku kuokota takataka zilizotupwa barabarani.

Katika likizo ya siku kuu ya May Day, wakulima wa kaskazini mashariki ya China walikuwa na "wiki ya dhahabu" ya kupanda tumaini lao. Kutokana na hali ya hewa ya mkoa wa Jilin, kipindi cha kupanda mbegu za mazao ya kilimo kilichelewa kwa siku 10 hivi mwaka huu kikilinganishwa na miaka ya zamani.

Baada ya kuingia majira ya mchepuo mwaka huu, hali ya hewa ilikuwa baridi kwa mfululizo, hivyo ujoto ulioko ndani ya udongo haukuwa mwingi, hali ambayo imechelewesha kipindi cha kupanda mbegu kwa siku 5 hadi 10 hivi tofauti na miaka ya nyuma. Katibu wa chama wa tawi la kijiji cha Paibu wilayani Nongan Bw. Zhao Haitao alisema, katika miaka ya nyuma, pirikapirika za kupanda mbegu zilianza tarehe 15 mwezi Aprili, lakini mwaka huu zilianza karibia na tarehe 1 mwezi May.

Familia ya mkulima Jin Guoyu wa kijiji cha Tantuo wilayani Nongan inalima zao la mahindi katika shamba leke hekta moja na kidogo tokea miaka mingi iliyopita, mwaka huu alimaliza kupanda mbegu za mahindi tarehe 2 mwezi May. Alisema, "Ujoto ulioko ndani ya udongo haukutosha baada ya kuingia majira ya Spring mwaka huu, hivyo hawakupandikiza miche ya mihindi mpaka baada ya kunyesha mvua ya kwanza karibu kufikia tarehe 1 mwezi May." Alisema, kwa kawaida wakulima wa kijiji chao wanapanda mbegu katika kipindi cha siku kuu ya May Day, hali ambayo ni tofauti sana na miji, kwani kipindi cha siku kuu ya May Day ya mwaka huu ni wakati mzuri sana wa kupanda mbegu kwa wakulima.

Ni sawa kabisa na wilaya ya Nongan, wilaya kadhaa nyingine maarufu kwa uzalishaji nafaka za mkoa wa Jilin, China, wakulima wa wilaya hizo pia walikuwa na pirikapirika ya kupanda mbegu katika kipindi cha siku kuu ya May Day. Mtaalamu mashuhuri wa utalii wa mkoa wa Jilin Bw. Wu Guangxiao alisema, siku kuu ya May Day ni siku kuu halisi ya kufanya kazi kwa wakulima, kazi za wakulima zingeheshimiwa na wotu wote wa China. Wingi mkubwa watu wa China wanaishi katika sehemu za vijiji, jamii nzima inatakiwa kufuatilia maendeleo ya uchumi wa sehemu ya vijiji na ongezeko la pato la wakulima, aliongeza, ni baada ya wakulima kutajirika tu, ndipo mahitaji ya nchini yatapoweza kuzinduliwa, na mambo ya utalii yataweza kukuzwa zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2006-05-09