Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-09 16:29:18    
Barua 0509--Shindano la chemsha bongo la "Mimi na Radio China kimataifa"

cri

Mtu mmoja akifikia umri wa miaka 65, anakuwa ameingia katika kipindi cha uzeeni; lakini Radio China kimataifa inayotimiza miaka 65 inaendelea katika hali yenye nguvu na uhai.

Miaka 65 iliyopita, matangazo ya Radio ya China yalianza huko Yanan, kituo cha mapinduzi ya China, tangu hapo matangazo ya Radio ya China yaliendelea siku hadi siku, toka Radio ya Xinhua ya Yanan, Radio Beijing hadi Radio China kimataifa, marafiki wengi zaidi wa sehemu mbalimbali duniani wameijua, kuifahamu na kuipenda China inayobadilika, inayozifungulia mlango nchi za nje na inayoendelea siku hadi siku.

Tarehe 3 Desemba mwaka huu itakuwa siku ya kudhimisha miaka 65 tangu Radio China kimataifa ianzishwe. Ili kuwawezesha wasikilizaji wa nchi mbalimbali waielewe vizuri zaidi historia ya miaka 65 ya Radio China kimataifa, kuanzia tarehe 14 mwezi huu Idhaa ya kiswahili ya Radio China kimataifa itaanzisha shindano la chemsha bongo la "Mimi na Radio China kimatafaifa", ambapo tutasoma makala 4 kuhusu shindano la chemsha bongo.

Kama tulivyofanya katika mashindano ya chemsha bongo ya miaka iliyopita, katika shindano hilo la chemsha bongo , kila tukimaliza kusoma makala moja tutatoa maswali mawili ili wasikilizaji wajibu. Shindano hilo la chemsha bongo litamalizika mpaka tarehe 1 Septemba mwaka huu, ambapo wajumbe wa kamati ya Radio China kimataifa watathibitisha majibu watakayotuletea wasikilizaji wetu na kuwachagua wasikilizaji watakaopata nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu pamoja na nafasi maalum, washindi wa nafasi maalum wataalikwa kuja Beijing mwezi Desemba mwaka huu kushiriki shughuli za kuadhimisha miaka 65 ya Radio China kimataifa, ambapo pia watapata nafasi ya kutembelea nchini China kwa wiki moja bila malipo.

Na wasikilizaji wetu wametuletea barua wakisifu ziara ya rais Hu Jintao wa China nchini Kenya kuanzia tarehe 27 hadi 29 Aprili.

Msikilizaji wetu Haasan Kipkerrich wa Nairobi Kenya anasema, nimepata habari hizo kutoka kwenye televisheni tulifurahia rais wa China kufanya ziara ya kiserikalil nchini kwetu, na tumefurahia msaada ambao aliotuletea, naomba Kenya na China zingeweza kuzidisha ushirikiano ili uhusiano kati ya nchi zetu mbili uzidi kuimarika zaidi. Matangazo yaliyotolewa na Radio China Kimataifa yalikuwa ni matangazo ya kufaa sana, na pia iliweza kutuelimisha kuhusu ziara hiyo na juhudi ambazo serikali ya china ilizo fany aili kusaidia nchi za Afrika na moja wapo ni Kenya, napongeza Radio China kimataifa kwa habari ambazo zilitupatia kuhusu ziara ya rais wa jamhuri ya watu wa China.

Alon tanohi ni mhandisi wa ndege katika Kenya Airways, alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, ziara hiyo ya rais Hu Jitnao nchini Kenya imekuwa inafaa kwa uhusiano na maendeleo ya nchi zetu mbili,. Nimepata habari hiyo kwa kusoma magazeti, televisheni, pia nimeijua kutoka kwa Radio China Kimataifa, ambayo inatangaza Kiswahili hapa Nairobi. Ripoti zenu zilikuwa ni nzuri , za kufaa , na zilikuwa na maelezo ya kutosha ya kutufurahia.

Na msikilizaji wetu Tomas naliyeko alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, mimi nafurahi sana kwa kuona rais Hu kututembelea, hiyo ni heshima sana kwa serikali yetu ya Kenya, pamoja na China. Tunashukuru tuendelee kufanya hivyo, maana yake tutakuwa kitu kimoja, Tuendelee kufanya hivyo, ziara yake itakuwa na umuhimu mkubwa sana, tunamfurahia sana. Alisema, alifungua radio nilipoendesha gari, alisikia mambo yalikuwa yanayoendelea nchini Kenya na China, tunafurahia sana.

Bw.Xavier L.Telly ? Wambwa wa Bungoma Kenya ametuletea barua pepe akisema, safari ya siku tatu ya Rais wa Jamhuri ya watu wa China Mheshimiwa Hu Jing Ntao hapa nchini Kenya ilinidondoa katika uso na moyoni mwangu machozi ya furaha. Kwani nilifurahishwa na matamushi yake ya kishujaa pamoja na Rais Mwai Kibaki walipojadiliana kwa amani jinsi ya kuzidisha uhusiano baina ya China na Kenya kuhusu udiplomasia, uchumi na maendeleo, utamaduni, utalii, michezo na kadhalika.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Rais Hu aliburudishwa na midundo za ngoma motomoto, maanake ni utamaduni na utalii kati ya China na Kenya utapata kudumu milele daima.

Kituo cha FM-CRI Kenya kilipata nguvu na mwelekeo mpya kulingana na safari ya Rais Hu.

Masomo ya Conficius na lugha ya Kichina katika chuo kikuu cha Nairobi ni kama harusi ya kimapenzi.

Pia risala ya Balozi wa Kenya nchini China Bi Ruth Sereti Solitei kuhusu Safari ya Rais Hu nchini Kenya ilinipendeza mno

Idhaa ya kiswahili 2006-05-09