Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-15 16:07:04    
Kikundi cha upinzani chakataa kutia saini makubaliano ya amani nchini Sudan

cri

Tarehe 14 kiongozi wa kikundi cha kundi kubwa la upinzani "the Sudan Liberation Army", SLA, Bw. Mohammed al-Nur kwa mara nyingine tena alikataa ombi la Umoja wa Afrika la kukitaka kikundi hicho kisaini makubaliano ya amani na kuufanya mchakato wa amani nchinin Sudan umekwe.

Mwanzoni mwa mwezi Mei kutokana na usuhulishi wa jumuyia ya kimataifa, kundi kubwa la upinzani "the Sudan Liberation Army" SLA na serikali ya Sudan zilisaini makubaliano ya amani huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria kuhusu suala la Darfur, lakini kikundi cha "the Justice and Equality Movement" kinachoongozwa na Bw. Mohammed al-Nur kilikataa kusaini makubaliano ya amani. Baadaye, japokuwa jumuyia ya kimataifa ilifanya juhudi kubwa na maofisa pamoja na wajumbe wa Umoja wa Mataifa walikwenda huko Darfur kulishawishi kundi la SLA na kikundi cha "the Justice and Equality Movement", lakini hawakupata mafanikio yoyote.

Wachambuzi wanaona kuwa sababu ya kukwama kwa makubaliano hayo ya amani inatokana na upinzani ndani ya makundi yenyewe ya upinzani. Hivi sasa nchini Sudan kuna makundi mawili ya upinzani, moja ni kundi la "the Sudan Liberation Army" yaani SLA kwa kifupi, ambalo lina nguvu zaidi, lingine ni kikundi cha "the Justice and Equality Movement" ambacho ni kidogo. Na kundi la SLA limegawanyika katika vikundi viwili: kimoja kiinaongozwa na Bw. Mninni Arcua Minnawi aliyekuwa naibu mwenyekiti wa SLA, na kinngine kiinaongozwa na Nur ambaye alikuwa mwenyekiti wa SLA. Kutokana na ugomvi wao wa kugombea madaraka, viongozi hao wawili waliachana, kwa hiyo ni vigumu kuwapatanisha. Kundi la Minni Arcua Minnawi na serikali ya Sudan waliposaini makubaliano ya amani, Nur alitangaza kujitoa kutoka kwenye mazunzumzo na kukataa kusaini makubaliano ya amani.

Idadi ya wafuasi wa kikundi cha Minnnawi ni kikubwa ikilinganishwa na watu wa kikundi cha Nur, lakini kikundi cha Nur kinatokana na kabila la Wafur ambalo lina watu wengi katika sehemu ya Darfur, kwa hiyo kina ushawishi mkubwa katika sehemu hiyo. Kutokana na hali hiyo, kazi ya kumshawishi Nur asaini makubaliano ya amani, ni muhimu sana katika juhudi za usuluhishi wa jumuyia ya kimataifa.

Nur aliwahi kukubali kusaini makubaliano ya amani, lakini masharti yake yalikuwa kwamba serikali ya Sudan lazima ikidhi matakwa yake ya kutoa fidia kwa waathirika wa vita katika sehemu ya Darfur, kushiriki zaidi kuwanyang'anya silaha wanamgambo wa Kiarabu na kuwapangia maisha ya wakimbizi wanaorudi nyumbani. Lakini Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa haukuunga mkono matakwa ya Nur kwa sababu alijitoa kutoka kwenye makubaliano ya amani, na makubaliano hayo umekwisha sainiwa na pande mbili, kama matakwa yake yatatekelezwa, mkataba huo hautakuwa na maana na hakika itasababisha upinzani mkali kutoka kwa Minnawi na huenda kutamfanya ajitoe kutoka kwenye makubaliano ya amani. Kwa hiyo wasuluhishi wa jumuyia ya kimataifa wanataka Nur asaini kwanza makubaliano hayo, na baadaye azungumze na serikali ya Sudan kuhusu matakwa yake.

Tarehe 15 baraza la usalama la Umoja wa Afrika litafanya mkutano nchini Ethiopia. Wasuluhishi wa jumuyia ya kimataifa walikuwa wakitumai siku hiyo itakuwa ni siku ya mwisho kabla ya serikali ya Sudan na vikundi vidogo kusaini makubaliano hayo. Lakini kwa kutokana na jinsi hali ilivyo sasa, lengo hilo halitaweza kutimizwa. Hata hivyo, jumuyia ya kimataifa haijaacha juhudi zake, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa unaendelea kusuluhisha vikundi mbalimbali visanini makubaliano hayo ya amani.

Idhaa ya kiswahili 2006-05-15