Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-17 16:54:15    
Mapishi ya kichwa cha samaki na vichipukizi vya mianzi

cri

Mahitaji:

Kichwa cha samaki, nyama iliyosagwa gramu 75, vichipukizi vya mianzi, doufu gramu 50, vitunguu maji gramu 10, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, mchuzi wa soya vijiko vitatu, chumvi nusu kijiko, pilipili manga na pilipili hoho kiasi kidogo.

Njia:

1. osha kichwa cha samaki, tia mvinyo wa kupikia na mchuzi wa soya.

2. ondoa maganda ya vichipukizi vya mianzi, kata doufu iwe vipande vipande.

3. tia mafuta kwenye sufuria yaache yachemke, tia vipande vya vitunguu na tangawizi halafu tia kichwa cha samaki kisha kikaange, kipakue na ukiweke kwenye sufuria. Kaanga vipande vya doufu na uviweke kwenye chungu.

4. Pasha moto tena, tia nyama iliyosagwa korogakoroga tia mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya, chumvi, pilipili manga korogakoroga zipakue na weka kwenye sufuria, mimina maji, tia vipande vya vichipukizi vya mianzi, pilipili hoho, na uache ichemke kwa nusu saa. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.