Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-17 19:37:01    
Kunywa maji kwa kufuata kanuni za kisayansi kutajenga afya

cri

Maji ni muhimu zaidi kwa mwili wa binadamu, binadamu akipoteza asilimia 15 ya maji mwilini, maisha yake yatakuwa hatarini. Hivyo, kunywa maji ni jambo ambalo kila mtu anapaswa kulifanya kila siku, lakini watu wengi hawafikiri kwa makini njia mwafaka ya kunywa maji. Utafiti umeonesha kuwa, kunywa maji kwa kufuata kanuni za kisayansi kunafaa zaidi kwa afya.

Kwanza, tunawajulisha wasikilizaji wetu mtu mmoja anayependa sana kunywa maji nchini China. Kwa watu wa kawaida, si rahisi kunywa maji kilo moja kwa mara moja, lakini kijana mmoja wa mji wa Chongqing anayeitwa Yu Guanxiong anaweza kufanya hivyo, na anakunywa maji kilo 25 kila siku. Tabia yake hiyo ya ajabu inatokana na ajali aliyopata miezi minne iliyopita. Tarehe 21 mwezi Desemba mwaka jana, kijana huyo alipata na ajali barabarani na alijeruhiwa vibaya, ingawa maisha yake yalinusurika lakini alianza kuwa na tabia hiyo. Alisema:

"sitaki kunywa maji mengi kiasi hicho lakini nasikia kiu kila baada ya kunywa maji. Ingawa nasikia njaa lakini sitaki kula chakula hata kidogo, nakunywa maji tu."

Siku hadi siku, nakunywa maji mengi zaidi na kula chakula kidogo zaidi. Kutokana na tatizo la utapia mlo lililosababishwa na tabia hiyo, uzito wake umepungua kwa kilo zaidi ya kilo 10. Hivyo alipaswa kupata matibabu kwenye hospitali.

Profesa Li Qifu wa hospitali ya kwanza ya chuo kikuu cha udaktari cha Chongqing aliona kuwa tatizo la ndugu Yu Guanxiong lilisababishwa na kujeruhiwa kwa ubongo wake katika ajali. Profesa Li alisema:

"figo ni kiungo kinachosaidia mwili usipoteze maji, lakini figo inadhibitiwa na vitu vinavyotoka kwenye ubongo ambavyo kwa kitaalama unaitwa arginine vasopressin (AVP). Tatizo la ndugu Yu Guanxiong ndilo linasababishwa na upungufu wa vitu hivyo ubongoni. Maji mengi yanapotea kutoka kwenye mafigo, basi utasikia kiu na utakunywa maji mengi zaidi."

Maji anayokunywa ndugu huyo hayafyonzwi mwilini na mengi yanatoka mwilini kupitia figo. Ndiyo sababu ingawa anaendelea kunywa maji bado anasikia kiu.

Hadithi ya Bw. Yu Guanxiong imethibitisha kikamilifu kuwa njia zisizo sahihi za kunywa maji zitaathiri afya. Basi kwa kawaida binadamu anapaswa kunywa maji kwa kiasi gani kila siku ili kutosheleza mahitaji ya mwili? Utafiti umeonesha kuwa, kiasi cha maji ya kunywa lazima kilingane ne kile cha maji yanayotoka mwilini kila siku. Hivyo mbali na kula chakula, kwa kawaida tunapaswa kunywa maji lita moja au mbili kila siku, ili kukidhi mahitaji ya mwili. Lakini kiasi cha maji ya kunywa pia kinategemea katika hali tofauti. Kwa mfano katika majira ya joto, wakati wa kufanya mazoezi makubwa ya viungo au kufanya kazi katika hali ya joto, unapaswa kunywa maji mengi zaidi.

Ni wakati gani tunapaswa kunywa maji na kwa kiasi gani? Huenda watu wengi wakasema watakunywa maji wakati wa kusikia kiu. Profesa Li Qifu alisema:

"ukisikia kiu mwili wako tayari umekosa maji. Hivyo tunapaswa kunywa maji mara kwa mara, usinywe maji tu wakati unasikia kiu tu."

Kiu ni dalili ya upungufu wa maji mwilini. Kunywa maji baada ya kusikia kiu ni tabia mbaya, itasababisha miili yetu kukosa maji mara kwa mara na hali hiyo itadhuru afya. Hivyo ni afadhari tunywe maji mara nyingi na kiasi kidogo kwa kila mara.

Kwa kawaida, inafaa kunywa maji kikombe kimoja baada ya kupiga mswaki, na kunywa kikombe kingine saa 4 asubuhi hivi, kimoja baada ya kula chakula cha mchana, kimoja saa 9 mchana, kimoja kabla ya chakula cha jioni, na kimoja kingine kabla ya kulala.

Aidha, kunywa maji wakati wa kufanya mazoezi ya mwili ni mambo yenye elimu. profesa msaidizi wa hospitali ya kwanza ya chuo kikuu cha udaktari cha Chongqing Bw. Zhou Bo alisema:

"tunajua kuwa tunapoteza maji kutokana na kutokwa na jasho jingi wakati wa kufanya mazoezi ya mwili, kama tunakunywa maji wakati wa kusikia kiu, hali ya uwiano mwilini imeharibika. Hivyo kwanza tunapaswa kunywa maji kabla ya kufanya mazoezi, pili baada ya kufanya mazoezi, tunapaswa kunywa maji kwa mara nyingi na kidogo kwa kila mara, ukinywa maji mengi mara baada ya mazoezi ya mwili, utapata madhara."

Bw. Zhou Bo alieleza kuwa, tatizo linalosababishwa na kunywa maji mengi baada ya mazoezi ya mwili linahusiana na kupotea kwa chumi mwilini. Wakati wa kufanya mazoezi ya viungo, jasho jingi linatoka pamoja na chumvi nyingi. Kama tukikunywa maji mengi wakati huo, kutokana na halijoto ya juu mwilini, maji hayo pia yanatoka mwilini na jasho pamoja na chumvi, kama hivyo, chumvi ndani ya damu inapungua zaidi, na uwezo wa kuhifadhi maji ukapungua, kiasi cha maji yataingia kwenye chembechembe na kuzivimbisha, basi utasikia kizunguzungu. Hiyo ni dalili za tatizo la kunywa maji mengi baada ya mazoezi ya mwili.

Hivyo, njia sahihi ya kunywa maji baada ya kufanya mazoezi ya mwili ni kuwa, kwanza kusukutua kinywa na kulainisha koo, halafu kunywa maji kidogo, halafu kunywa kidogo tena. Baada ya mazoezi ya mwili, jasho jingi likitoka, , itakuwa bora zaidi kwa afya kunywa maji yenye chumvi ndogo.

Mwisho, tuongelee kuhusu maji yasiyo salama kwa matumizi ya binadamu. Kwanza ni maji yaliyolimbikizwa kwa muda mrefu. Watoto wakinywa maji hayo mara kwa mara, itaathiri ukuaji wa miiili yao, kwa wazee, itaharakisha uzeee. Ya pili ni maji yaliyokuwa yanachemka katika chombo cha kuchemshia maji kwa umeme. Maji kama hayo yakitumiwa mara kwa mara, itavurugu uwezo wa kazi za tumbo. Ya tatu ni maji yaliyochemshwa tena. Maji yakichemshwa tena, kiasi cha kemikali ya sumu inayoitwa nitrite kitaongezeka na kuleta madhara kwa afya.

Idhaa ya Kiswahili 2006-05-17