Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-19 18:14:15    
Spika wa bunge la umma la China atarajia uhusiano kati ya China na Ulaya utaendelea siku hadi siku

cri

Spika wa Bunge la umma la China Bwana Wu Bangguo ambaye yuko ziarani nchini Romania tarehe 18 alitoa hotuba kwenye kasri la bunge la Romania akisema, China inaiunga mkono Romania kujiunga na Umoja wa Ulaya na kuamini kuwa mchakato wa Romania kujiunga na Umoja wa Ulaya utatia uhai mpya kwa maendeleo ya Umoja wa Ulaya, pia utaleta fursa mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya.

Romania ni kituo cha kwanza katika ziara hiyo ya spika Wu Bangguo katika nchi 4 za Ulaya. Baada ya nusu mwaka, Romania, ambayo ni rafiki wa China tangu zamani itakuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Katika hotuba yake, spika Wu alisema China inaheshimu mfumo wa jamii na njia ya maendeleo iliyochagua Romania kwa kufuata hali halisi ya nchi hiyo, na kuheshimu sera yake kwa nchi za nje kwa ajili ya kujiunga na Ulaya. Spika Wu alisema:

China inaunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya Romania na wananchi wake kwa ajili ya kujiunga na utandawazi wa Umoja wa Ulaya. China ina imani kuwa, baada ya kujiunga na Umoja wa Ulaya, Romania hakika itatia uhai mpya kwa maendeleo ya Umoja wa Ulaya, jambo hili litaleta fursa mpya kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.

Tokea Umoja wa Ulaya uanzishwe mwaka 1993, umoja huo ulipanuliwa mara mbili na kuwa na nchi wanachama 25 wa hivi sasa, kutoka nchi wanachama 12 mwanzoni, thamani ya jumla ya uchumi wa Umoja wa Ulaya inalingana na ile ya Marekani. Tarehe 1 Januari mwakani, Umoja wa Ulaya utapokea tena nchi wanachama wawili na kutimiza upanuzi wake wa mara ya tatu katika historia yake. Hotuba ya spika Wu Bangguo pia imeiwakilisha China kueleza uungaji mkono wa China wa siku zote kwa mchakato wa utandawazi wa uchumi wa Umoja wa Ulaya. Spika Wu alisema:

China inaunga mkono utandawazi wa uchumi wa Umoja wa Ulaya, China inafurahia Umoja wa Ulaya uoneshe umuhimu wake mkubwa zaidi katika mambo ya kikanda na kimataifa. Umoja wa Ulaya ni kundi la nchi zilizoendelea lililo kubwa zaidi kuliko mengine duniani, na China ni nchi inayoendelea iliyo kubwa zaidi kuliko nyingine duniani. Ingawa kuna tofauti kubwa ya historia, utamaduni na mifumo ya kisiasa kati ya pande hizo mbili, lakini katika miaka 30 iliyopita tangu China na nchi za Umoja wa Ulaya zianzishe uhusiano wa kibalozi, uhusiano kati ya pande mbili unaendelea vizuri katika hali ya utulivu, na pande hizo mbili zimekuwa na maslahi mengi ya pamoja. Spika Wu alisema:

Maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya yameonesha kuwa, nchi zenye mifumo tofauti ya jamii zikishikilia kanuni tano za kuishi pamoja kwa amani, kupanua maslahi ya pamoja, na kuondoa migongano kwa njia mwafaka, hakika zitaweza kuimarisha ushirikiano na kuendeleza uhusiano.

Maendeleo ya miaka 30 yamezifanya China na Umoja wa Ulaya ziongeze zaidi uaminifu wa kisiasa, kupanua siku hadi siku ushirikiano wa kunufaishana katika sekta za uchumi na biashara, na kuzidisha maingiliano katika sekta za utamaduni. Spika Wu alisema:

China siku zote inauchukulia uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya kwenye hadhi muhimu katika mambo ya kidiplomasia ya China. Kuendeleza siku hadi siku uhusiano wa kimkakati na kiwenzi kati ya China na Umoja wa Ulaya katika sekta mbalimbali kunalingana na maslahi ya kimsingi ya pande hizo mbili, pia kunasaidia kuleta maendeleo mazuri ya uhusiano wa kimataifa, na kusaidia amani, utulivu na maendeleo ya dunia.

Idhaa ya Kiswahili 2006-05-19