Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-22 16:29:52    
Serikali mpya ya Iraq yakabiliwa na changamoto kubwa ya hali mbaya ya usalama

cri

Tarehe 21 waziri mkuu mpya wa Iraq Nuri al-Maliky kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, serikali mpya ya Iraq itachukua hatua kali kutuliza ghasia nchini Iraq. Lakini katika siku hiyo hiyo milipuko isiyopungua mitatu ilitokea na kusababisha watu zaidi ya 70 kufariki na kujeruhiwa. Hali mbaya ya usalama imekuwa changamoto kubwa kwa serikali iliyoanzishwa siku chache zilizopita.

Mapema katika siku hiyo, mlipuko uliokuwa unawalenga polisi wa Iraq ulitokea karibu na barabara na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine 24 kujeruhiwa. Mchana katika siku hiyo, katikati ya mji wa Baghdad mkahawa mmoja ambao askari polisi wa Iraq wanakwenda mara kwa mara ulitokea mlipuko wa kujiua, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 13 wakiwemo askari polisi watatu na wengine 18 kujeruhiwa. Pamoja na hayo, katika siku hiyo mlipuko mwingine wa bomu lililotegwa ndani ya gari ulitokea magharibi mwa Baghdad, na kusabaisha vifo vya watu watatu na wengine 15 kujeruhiwa.

Pamoja na hali hiyo, nchi zilizotuma majeshi nchini Iraq zimekuwa zikifikiria kupunguza au kuondoa kabisa majeshi yao. Balozi wa Marekani nchini Iraq Zalmay Khalilzad tarehe 20 alisema, Marekani itakuwa makini kuondoa jeshi lake, lakini inataka kupunguza idadi ya askari wake. Katika siku hiyo, waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair pia alisema, jeshi la Uingereza litaendelea kuwepo nchini Iraq, lakini kadiri utulivu unavyotengamaa, majeshi yote ya nje yanataka kukabidhi jukumu la kulinda usalama kwa jeshi la Iraq. Naibu waziri mkuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa Italia Massimo D'Alema katika siku hiyo pia alisema, wiki hii bunge la Italia litafanya mkutano kujadili mpango wa kuondoa jeshi lake kutoka Iraq. Habari kutoka gazeti la "Asahi" la Japan, zinasema, kwa kuwa baraza la mawaziri la Iraq limekamilishwa, Japan inafikiria kuondoa askari wake kutoka Iraq, kwa makadirio, waziri mkuu wa Japan atajadiliana na rais Bush kuhusu suala hilo katika ziara yake nchini Marekani mwezi Juni.

Hali ya usalama inaendelea kuwa mbaya na nchi zinazotuma majeshi zinataka kupunguza au kuondoa majeshi yake nchini Iraq, hali hiyo ni changamoto kubwa kwa serikali ya Nuri al-Maliky.

Kwanza, watu wanaoshughulikia usalama katika serikali mpya bado hawajateuliwa. Tarehe 20 kwenye orodha ya mawaziri iliyopitishwa, nafasi za waziri wa mambo ya ndani na ulinzi wa taifa na usalama hazikujazwa, inawapasa waziri mkuu Maliky na manaibu wawili wazishughulikie nafasi hizo kwa muda. Na viongozi wa madhehebu ya Shiya, Suni na Wakurd siku zote wana hamu kubwa kuchukua nafasi hizo, kama Maliky asipoweza kutatua vizuri suala hilo huenda Iraq isiwe na utulivu.

Pili, migogoro kati ya madhehebu ya kidini na ya kikabila imeathiri usalama wa Iraq kwa miaka mingi. Mapambano ya kugombania madaraka ya kisiasa na kiuchuni kati ya madhehebu ya Shiya na Suni na Wakurd yanaongezeka siku hadi siku badala ya kupinga ukaliaji wa majeshi ya nje kama ilivyokuwa hapo kabla. Katika wakati makundi hayo matatu yanapokuwa katika mapambano vikosi vya makundi hayo havitakubali kutaacha silaha zao. Viongozi wa Wakurd na Suni hivi karibuni walisema, wanapinga pendekezo la Maliky la kunyang'anya silaha kutoka kwa wanamgambo.

Tatu, Kundi la "Al-Qaeda" linaloongozwa na Abu Musab al-Zarqawi bado ni tishio kubwa kwa serikali mpya. Kabla ya kuasisiwa kwa serikali hiyo, Zarqawi alisema hataitambua "serikali ya kibaraka" inayoendeshwa na Marekani, na kusema atafanya mashambulizi mengi. Kukaliwa na majeshi ya nchi za nje kumekuwa kisingizio chake cha kufanya mashambuzi, ataendelea kutumia hasira za watu wa Iraq dhidi ya majeshi ya nje kufanya mashambulizi.

Nne, majeshi ya polisi na serikali yanahitaji kurekebishwa haraka, lakini kutokana na migogoro kati ya makundi, marekebisho yanakumbwa na vikwazo vingi.

Wachambuzi wanaona, hali ya usalama nchini Iraq haina matumaini ya kuwa nzuri, serikali ya Maliky inahitaji kutuliza ugombeaji wa madaraka kati ya madhehebu na makundi, ili kuthibitisha watu watakaoteuliwa. Pamoja na hayo hivi sasa serikali hiyo mpya bado haina nguvu za kutosha kuhakikisha usalama, bali inahitaji Marekani na Uingereza kuendelea kuisaidia katika kulinda usalama na kurekebisha majeshi ya polisi na serikali, kama majeshi ya nchi za nje yakiondoka yataacha hali ya machafuko ambayo haitaisha nchini Iraq.

Idhaa ya kiswahili 2006-05-22