Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-23 15:16:17    
Shindano la chemsha bongo la "Mimi na Radio China Kimataifa" (2)

cri

Radio China kimataifa inayosonga mbele

Kwanza tunatoa maswali mawili ya makala hii ya pili, la kwanza: Hivi sasa Hivi sasa Radio China kimataifa ina vituo vingapi vya waandishi wa habari katika sehemu mbalimbali duniani? Swali la pili: Kila siku Radio China kimataifa inatangaza kwa lugha ngapi kwa nchi za nje ?

Mwishoni mwa miaka ya 70 ya karne iliyopita, China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Tokea hapo, Radio China kimataifa ilianza kufuata njia ya mageuzi na maendeleo, ambapo mvuto wake ulipanuliwa siku hadi siku. Jarida la Ujerumani liitwalo: Radio Kurier lilisifu mabadiliko ya vipindi vya matangazo ya lugha ya kijerumani ya Radio China kimataifa kuwa ni "upepo mwanana kutoka China iliyoko mbali", na kuisifu Radio China kimataifa kuwa ni "radio inayopendwa na watu". Wakati huo Shirika la klabu za radio la Amerika ya kaskazini liliichagua Radio China Kimataifa kuwa "radio kubwa zaidi kuliko nyingine duniani".

Kadiri China inavyoendelea siku hadi siku ndivyo nchi mbalimbali duniani zinavyotaka kuifahamu China kwa undani siku hadi siku, ambapo Radio China kimataifa iliongeza na kubadilisha vipindi vya matangazo yake, ambapo vipindi vya matangazo ya Radio China kimataifa vilianza kuwa vya aina mbalimbali, ambavyo vinalenga kuwafahamisha watu duniani hali halisi ya maendeleo ya China, mhariri wa ngazi ya juu Mzee Wang Zuozhou ambaye aliwahi kupewa tuzo ya juu kabisa ya habari ya China alituambia.

Bwana Wang Zuozhou alianza kufanya kazi katika Radio China kimataifa mwanzoni mwa miaka ya 60, ana umri wa miaka 70 mwaka huu, alikuwa mmoja wa waandishi wa habari wa Radio China kimataifa aliyefanya kazi nchi ya nje. Alipokumbusha kazi yake katika kituo cha waandishi wa habari cha Radio China Kimataifa alisema:

Siku ya kwanza tangu kuanzishwa kituo chetu cha waandishi wa habari nchini Ufaransa tulianza kazi yetu na kushinda taabu mbalimbali kwa kukusanya habari nchini humo, ambapo tulitoa habari nyingi kwa wakati. Kwa mfano, mimi nilishiriki kwenye kazi ya kutoa habari kuhusu Makubaliano ya amani ya Afghanistan yaliyosainiwa huko Geneva, baada ya dakika zaidi ya 20 tu tangu kusainiwa kwa makubaliano hayo, tulitoa habari hiyo.

Kuanzia mwaka 1980, Radio China kimataifa ilianzisha vituo vyake vya waandishi wa habari katika nchi na sehemu mbalimbali duniani. Vituo vya waandishi wa habari vya CRI vilivyoko Tokyo, Japan na Belgrade, Yugoslavia vilikuwa vituo vya waandishi wa habari wa CRI vilivyoanzishwa mapema zaidi. Miongoni mwa waandishi wa habari waliotumwa kufanya kazi katika vituo hivyo, Bibi Liu Suyun ni mmoja aliyesifiwa zaidi, ambaye aliwahi kutoa habari nyingi katika tukio la milipuko iliyotokea huko Jerusalem. Bibi Liu alipokumbusha tukio hilo alisema:

Mwezi Oktoba mwaka 2000 mgogoro ulianza kufanyika kati ya Palestina na Israel kwenye ukanda wa Gaza, ambapo tulikwenda Gaza na bendera ya taifa letu, tulishuhudia mpalestina mmoja akipigwa risasi na kutokwa na damu, akaaunguka chini, tulikuwa tuko karibu sana naye, jambo hili lilinifanya nione kuwa, vifo na uhai vipo karibu sana na sisi. Katika miaka kadhaa baadaye nilipofanya kazi katika vituo vya waandishi wa habari, nilishuhudia mapambano ya kijeshi mara kwa mara.

Hivi sasa Radio China kimataifa imekuwa na vituo 27 vya waandishi wa habari katika sehemu mbalimbali duniani, na waandishi wa habari wa vituo hivyo wanaweza kutoa habari kwa wakati juu ya matukio makubwa yaliyotokea au yanayotokea duniani. Kutokana na upanuzi na maendeleo ya matangazo ya Radio China kimataifa, hivi sasa Radio China kimataifa inatangaza kwa lugha 43 kwa siku, na muda wa matangazo yake ni zaidi ya saa 780 kwa siku, Radio China kimataifa imekuwa moja ya radio tatu kubwa zaidi za kimataifa duniani.

Baada ya kufanya mageuzi na ufunguaji mlango, wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wanaokuja China kufanya kazi, kusoma, kutalii na kufanya biashara wanaongezeka zaidi siku hadi siku. Ili kuwafahamisha sera za China za nchini na kwa nje na kuielewa China kwa usahihi, na pia kuwasaidia vijana wengi nchini China wanaofanya kazi na wanaosoma, mwaka 1984 Radio China kimataifa ilianzisha matangazo yake ya lugha ya kiingereza kwa watu wa sehemu ya Beijing. Ofisa msimamizi wa matangazo hayo Bi.Wang Lu alipozungumzia matangazo hayo alisema kwa majivuno:

Tulianzisha matangazo yetu ya kiingereza kwa watu wa sehemu ya Beijing, matangazo yetu hayo yakiwemo vipindi vya muziki na vipindi vingine vya kiingereza ambavyo viliandaliwa vizuri zaidi kuliko vingine nchini China, ambavyo vyote vilianzishwa mara ya kwanza nchini China, hivyo tunaona fahari. Kutokana na jinsi mvuto wa Radio China kimataifa unaoongezeka siku hadi siku, mbinu moja tu ya matangazo ya radio hiyo haiwezi tena kulingana na mahitaji ya maendeleo ya hali ya mambo.

Mwaka 1998, Radio China kimataifa ilifanya juhudi kubwa kukuza matangazo yake kwenye mtandao wa internet, na kuanzisha tovuti ya CRI Online ya lugha mbalimbali kwenye mtandao. Hivi sasa tovuti hiyo imeendelezwa kuwa ya maandishi ya lugha 43, na wasikilizaji wanaweza kusikiliza vipindi vya lugha 48 kwenye tovuti. Takwimu zilizokusanywa zinaonesha kuwa, tovuti ya CRI Online inajulikana zaidi miongoni mwa tovuti mbalimbali zilizoanzishwa na radio kubwa mbalimbali za kimataifa za nchi mbalimbali.

Ili kuiwezesha China ielewe zaidi utamaduni wa nchi mbalimbali, wafanyakazi wa Radio China kimataifa pia walitafsiri hadithi, filamu na maandishi mengi ya taaluma za nchi za nje kwa kichina, wakati huo huo pia walitafsiri maandishi mengi maarufu ya China kwa lugha za kigeni, na kuusambaza utamaduni wa China katika nchi mbalimbali duniani. Na baadhi ya wafanyakazi wa idhaa mbalimbali za Radio China kimataifa walitoa mchango mkubwa katika kuhimiza maingiliano ya utamaduni kati ya China na nchi za nje, na kusifiwa na nchi mbalimbali. Mtangazaji mzee wa idhaa ya kiurdu Bwana Lu Shuilin ni mmoja wao. Mwaka 1997 alipewa nishani ya mafanikio mazuri iliyotolewa na serikali ya Pakistan. Alipozungumzia jambo hili, Bwana Lu alisema kwa unyenyekevu sana:

Nilikuwa nimefanya kazi kwa kadiri iwezekanavyo katika wakati wa baada ya kazi, nilifanya kazi niliyoipenda. Kama kazi hiyo imechangia maingiliano ya utamaduni kati ya China na Pakistan, kweli hili pia ni moja ya matumaini yangu.

Wasikilizaji wapendwa, sasa tunarudia maswali mawili ya makala hiyo ya 2 ya shindano la chemsha bongo la "Mimi na Radio China kimataifa", swali la kwanza: Hivi sasa Hivi sasa Radio China kimataifa ina vituo vingapi vya waandishi wa habari katika sehemu mbalimbali duniani? Swali la pili: Kila siku Radio China kimataifa inatangaza kwa lugha ngapi kwa nchi za nje?

Wasikilizaji wapendwa mlikuwa mkisikiliza maelezo kuhusu Radio China kimataifa inayosonga mbele, wiki ijayo wakati kama huu mtakaribishwa kusikiliza makala ya tatu ya shindano la chemsha bongo la "Mimi na Radio China kimataifa", msikose kutusikiliza.

Idhaa ya Kiswahili 2006-05-23