Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-23 15:53:54    
Nafasi mpya muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa China

cri

Hivi sasa sekta moja inayoibuka haraka nchini China, imekuwa nafasi mpya muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa China. Sekta hiyo ni uvumbuzi wa utamaduni, ambao ni pamoja na sanaa ya maonesho ya michezo, filamu na michezo ya televisheni, burudani ya teknolojia ya tarakimu, uendelezaji wa software za kompyuta pamoja na utengenezaji wa michezo ya katuni. Katika miaka ya karibuni, sekta hiyo ya uvumbuzi wa utamaduni imekuwa inachukua nafasi kubwa mwaka hadi mwaka katika maendeleo ya uchumi ya baadhi ya miji iliyoendelea.

Umaalum mkubwa wa sekta ya uvumbuzi wa utamaduni ni kufanya uvumbuzi, kuunganisha uvumbuzi wa sanaa ya utamaduni na teknolojia ya kisasa, na kunufaika kiuchumi kwa kupitia uendelezaji wa masoko. Moja ya uvumbuzi wa utamaduni ni sekta ya burudani kwenye simu za mkononi, ambayo inastawi hatua kwa hatua. Huduma zenye nyongeza ya thamani zinazotolewa na kampuni za burudani za simu za mkononi zikiwa ni pamoja na upashanaji wa habari za mambo ya multimedia, kuingia kwenye mtandao wa Internet kwa simu za mkononi na kuongeza michezo mingi mipya ya simu za mkononi, vimebadilisha mawazo ya zamani kuhusu upashanaji habari wa kijadi wa simu za mkononi. Hivi sasa watu wengi nchini China wanapenda kuwa na huduma za aina hiyo kwenye simu za mkononi. Kampuni ya teknolojia ya upashanaji habari ya Xinshi ya Beijing ni moja ya kampuni za burudani ya simu za mkononi, na michezo iliyobuni inapendwa na watu wengi hususan vijana, hali kadhalika imeleta pato kubwa kwa kampuni hiyo. Naibu mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Hu Bin anafurahia mustakabali wa soko la huduma za burudani kwenye simu za mkononi.

"Michezo yenyewe ni sekta yenye uvumbuzi sana, shughuli za kuleta nyongeza ya thamani kwa utoaji wa huduma za burudani ya simu za mkononi ni sekta moja mpya. Hivi sasa vijana wengi wanapenda kufanya shughuli nyingi kwa kutumia simu zao za mkononi zikiwa ni pamoja na michezo ya simu za mkononi na kusikiliza muziki na kuangalia picha za katuni wakati mwenye simu anatafutwa katika simu."

Kampuni ya teknolojia ya upashanaji habari ya Xinshi ya Beijing ilibuni michezo ya simu za mkononi kutokana na riwaya za "Gongfu" na "Hadithi ya Nchi Tatu", ambazo watu laki 1 waliitunza katika kompyuta zao. Bw. Hu alisema, wakati walipobuni michezo ya simu za mkononi walizingatia wahusika na mambo yaliyomo katika hadithi hizo za asili, waliunganisha vizuri utamaduni na teknolojia ya kisasa ili kuleta maono yanayotofautiana na yale ya zamani.

"Karibu kila mwezi tunabuni michezo miwili ya simu za mkononi sisi wenyewe, kitu tunazingatia zaidi ni kufanya watu waone kuwa michezo tuliyobuni siyo mambo rahisi, bali ni yenye vitu vya utamaduni ndani yake."

Hivi sasa sekta ya uvumbuzi wa utamaduni inaendelezwa kwa haraka katika baadhi ya miji iliyoendelea kiuchumi ikiwemo Beijing, Shanghai, Shenzhen na Hangzhou, ambapo baadhi ya vituo vya sekta ya uvumbuzi wa utamaduni vimeanzishwa hatua kwa hatua. Katika eneo la Zhongguancun la Beijing, ambalo linasifiwa kuwa ni "Silicon Valley" ya China, kuna kampuni nyingi za uvumbuzi wa utamaduni. Naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi ya eneo la ustawishaji la sayansi na teknolojia Bw. David alisema, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana kampuni zaidi ya 200, zikiwemo za software, michezo, muziki na uchapishaji, zilihamia kwenye eneo la ustawishaji wa sayansi na teknolojia la Zhongguancun. Sasa eneo hilo limebadilika kuwa sehemu zenye uvumbuzi wa utamaduni, na kuzingatia kukuza umaalumu na ubora wake.

"Eneo la ustawishaji la Zhongguancun linakuza ubora wa teknolojia na sekta ya uzalishaji mali kwa kutegemea idadi kubwa ya wavumbuzi na mazingira bora ya kipekee ya sekta ya uvumbuzi, katika siku za baadaye litazingatia uzalishaji bidhaa za teknolojia ya tarakimu, kuendeleza michezo inayochezwa kwenye tovuti, video ya michezo ya katuni, huduma za nyongeza ya thamani ya Internet na nyongeza ya thamani ya simu za mkononi, pamoja na kuhimiza maendeleo ya michezo ya sinema na video.

Kama ilivyo kwa mji wa Beijing, mji wa Shanghai ulioko kwenye pwani ya mashariki mwa China, katika miaka michache iliyopita pia umepiga hatua kubwa katika sekta ya uvumbuzi wa utamaduni. Takwimu inaonesha kuwa hivi sasa thamani ya uzalishaji mali ya sekta ya uvumbuzi wa utamaduni ya Shanghai inachukua 7.5% ya pato la mji huo. Shanghai imenuia kuendeleza Asia kuwa kimoja cha vituo vya uvumbuzi wa utamaduni vyenye athari kubwa.

Sekta ya uvumbuzi wa utamaduni ni yenye umaalumu wa kuwa na nyongeza kubwa ya thamani na hifadhi ya mazingira ya asili. Hivi sasa mikoa mbalimbali nchini inachukulia uendelezaji wa sekta ya uvumbuzi wa utamaduni kuwa ni moja ya hatua muhimu za kubadilisha muundo wa utamaduni, inajitahidi kuboresha mfumo wa sheria na kanuni kuhusu sekta ya uvumbuzi wa utamaduni, inafanya utafiti na kubuni sera za uhamasishaji juu ya usimamizi wa haki-miliki ya kielimu, ukusanyaji wa kodi, ukusanyaji wa mitaji na uungaji mkono wa kifedha na wataalamu. Profesa wa chuo kikuu cha umma cha China Bw. Jin Yuanpu amesema, hivi sasa kuna hali ya kukosa ulingano katika maendeleo ya uchumi wa taifa, kuhimiza maendeleo ya sekta ya uvumbuzi wa utamaduni ni mwelekeo wa marekebisho ya muundo wa utamaduni na kuinua kiwango cha sekta ya uzalishaji mali. Alisema hivi sasa sekta ya uvumbuzi wa utamaduni ya China bado iko katika kipindi cha mwanzo cha maendeleo, hivyo wakati wa kuhimiza maendeleo ya sekta hiyo, kunatakiwa kuwepo kueneza utamaduni maalumu wa mikoa mbalimbali ya China hadi sehemu mbalimbali ya dunia kwa kutumia bidhaa za uvumbuzi wa utamaduni.

"Sekta ya uvumbuzi ya utamaduni ya China inatakiwa kufuata njia ya maendeleo inayoendana na maendeleo yao katika sehemu mbalimbali, katika utekelezaji wake tunatakiwa kueneza mambo mazuri ya China hadi nchi mbalimbali duniani."

Bw. Jin Yuanpu alisema, uendelezaji wa sekta ya uvumbuzi wa utamaduni unainufaisha China na kuibadilisha kuwa nchi inayozalisha bidhaa za teknolojia ya kisasa na zenye nyongeza kubwa ya thamani kutoka nchi kubwa ya uzalishaji na usindikaji bidhaa kwa kutumia wafanyakazi wengi na zenye nyongeza ndogo ya thamani. Kutokana na hali halisi ya hivi sasa, soko la uvumbuzi wa utamaduni la China linaendelezwa kwa kasi, lakini soko hilo bado halijakomaa, mahitaji yake bado hayajawa tulivu, sekta ya uvumbuzi wa utamaduni ni sekta ya uzalishaji mali yenye hatari lakini pia ina mustakabali mzuri.

Idhaa ya kiswahili 2006-05-23