Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-29 20:00:56    
China kuchukua hatua kuinua ufanisi wa matumizi ya raslimali ya maji

cri

Mkutano wa taifa wa kazi kuhusu rasilimali ya maji, ambao unafanyika hivi sasa kwenye mji wa Eerduosi, mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ulioko sehemu ya kaskazini mwa China, tarehe 28 ulitoa wito wa kutaka kuchukuliwa hatua zaidi katika miaka mitano ijayo, ili kuinua ufanisi wa matumizi ya maji, na kupunguza wastani wa matumizi ya maji ya mwaka katika uzalishaji mali yenye thamani ya Yuan elfu 10 kuwa chini ya 6%. Kutokana na hayo, China itajenga mfumo wa udhibiti na usimamizi kuhusu raslimali ya maji.

 

"Kwanza, idara za usimamizi zilizoko kwenye maeneo ya mitiririko ya mito zinatakiwa kufanya udhibiti wa matumizi ya maji ya sehemu zake, ambapo mikoa mbalimbali inatakiwa kubuni kwa haraka vigezo vya matuimzi ya maji vya sekta muhimu zinazotumia maji mengi. Pili, kuboresha usimamizi wa uidhinishaji wa matumizi ya maji. Tatu, kusimamia kwa makini matumizi ya maji yaliyoko chini ya ardhi, kuweka mpango mwafaka wa kupeleka maji kwenye sehemu zenye upungufu mkubwa wa maji na zenye mazingira dhaifu ya asili."

China ni nchi yenye upungufu wa rasilimali ya maji, wastani wa rasilimali ya maji kwa kila mtu ni chini ya theluthi moja ya wastani wa rasilimali ya maji kwa kila mtu duniani, wastani wa upungufu maji katika mwaka wa kawaida ni mita za ujazo karibu bilioni 40, miji zaidi ya 400 nchini China ina upungufu wa maji, na miji 110 kati ya hiyo ina upungufu mkubwa wa maji.

Ingawa kuna upungufu mkubwa wa maji, lakini nchini China pia kuna tatizo la matumizi holela ya raslimali ya maji, na ufanisi wa rasilimali ya maji ni mdogo. Umwagiliaji maji mashambani ni wa ovyo; Kiwango cha matumizi ya maji yaliyokwisha tumika na kusafishwa ni cha chini sana kikiwa ni cha kiwango cha mwanzoni mwa miaka ya 80 ya karne iliyopita cha nchi zilizoendelea; Katika maisha ya kawaida, matumizi ya vyombo vinavyozuia matumizi ya ovyo ya maji bado hayajaenezwa kwenye sehemu mbalimbali nchini, na mwamko wa watu wa kubana matumizi ya maji bado unatakiwa kuinuliwa.

Naibu waziri wa maji wa China Bw. Hu Siyi anaona, katika hali ya namna hiyo, China inapaswa kujenga jamii yenye kubana matumizi ya maji na kuinua ufanisi wa matumizi ya raslimali ya maji.

"Sekta ya kilimo inatakiwa kufanya marekebisho kuhusu mfumo wa umwagiliaji maji mashambani, kuhimiza ujenzi wa miradi ya majaribio ya umwagiliaji maji mashambani kwa njia ya kubana matumizi ya maji na kufanya marekebisho dhidi ya mifereji iliyopo; Sekta ya viwanda inatakiwa kufanya marekebisho ya teknolojia na kutumia zana za kisasa za kubana matumizi ya maji, kuhimiza usafishaji wa maji yaliyokwisha tumika na kutumia maji ya bahari kwenye sehemu ya pwani."

China inatarajia kuinua ufanisi wa matumizi ya raslimali ya maji kwa kutumia mbinu hizo, na kujitahidi kuongeza matumizi ya maji ya kumwagilia mashambani ifikapo mwaka 2010, kupunguza kwa udhahiri matumizi ya maji viwandani, na kufanya matumizi ya maji ya sekta ya huduma kukaribia kiwango cha kisasa duniani.

Licha ya suala la upungufu wa rasilimali ya maji, uchafuzi wa maji pia ni suala linalosumbua sehemu nyingi za China. Katika baadhi ya sehemu za China, mito na maziwa vimekauka kabisa, maeneo ya ardhi oevu yanapungua. Naibu waziri wa maji wa China Bw. Hu Siyi amesema, katika miaka mitano ijayo wizara ya maji ya China si kama tu itahimiza jamii ya China kubana matumizi ya maji, bali pia itaimarisha hifadhi ya rasilimali ya maji ili kuhakikisha usalama wa maji ya kunywa na usalama wa mazingira ya asili ya mito.

Idhaa ya Kiswahili 2006-05-29