Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-05-30 20:24:31    
Uvumbuzi umekuwa nguvu ya kuhimiza maendeleo ya viwanda vya China

cri

Kwenye mkutano wa baraza la Asia la Boao uliofanyika hivi karibuni, maofisa wa idara husika za serikali ya China, viongozi wa viwanda vya serikali na wakurugenzi wakuu wa kampuni za kimataifa walikuwa na majadiliano kuhusu mchango na umuhimu wa uvumbuzi kwa maendeleo ya viwanda vya serikali ya China. Wanaona kuwa hivi sasa uvumbuzi wa teknolojia umekuwa nguvu ya kuhimiza maendeleo ya viwanda vya serikali ya China, ambao unakuza kwa mfululizo nguvu yake ya ushindani kwenye soko la kimataifa.

Nchini China, viwanda vya serikali ni nguzo ya uchumi wa taifa na ni uhai wa uchumi wa China. Viwanda 15 kati ya viwanda 18 nchini China vinavyochukua nafasi 500 za mbele duniani ni viwanda vya serikali. Serikali ya China inazingatia sana kuhimiza viwanda vikubwa vya serikali kukuza nguvu ya uvumbuzi. Naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi wa mali za serikali ya baraza la serikali Bw. Wang Ruixiang alipotoa maelezo kuhusu suala hilo, alisema,

"Viwanda ni injini na nguvu kuu ya uvumbuzi wa China. Jambo muhimu kabisa katika kujenga nchi yenye nguvu ya uvumbuzi ni kuimarisha hadhi ya viwanda katika uvumbuzi wa teknolojia, na kujenga mfumo mpya wa uvumbuzi wa teknolojia unaoendana na hali mpya ya masoko. Viwanda vingi vikubwa vya serikali vinahusika na sekta muhimu za uchumi wa taifa, na vinabeba majukumu muhimu katika mipango ya muda mrefu na wastani pamoja na miradi mikubwa ya sayansi na teknolojia ya taifa."

Bw. Wang Ruixiang alisema, kutokana na maendeleo ya miaka mingi, uwezo wa uvumbuzi wa teknolojia wa viwanda vikubwa vya serikali umekuzwa kwa udhahiri, na yamepatikana mafanikio makubwa ya kiteknolojia. Katika miaka 5 iliyopita idadi ya hataza zilizosajiliwa za viwanda vikubwa vya serikali iliongezeka kwa wastani wa 28% kwa mwaka, ambapo idadi ya hataza zilizosajiliwa za viwanda vikubwa vya serikali katika mwaka 2005 ilizidi elfu 10. Aidha, uwezo wa uvumbuzi wa viwanda vikubwa vya serikali katika usimamizi na ujenzi wa utaratibu pia umeimarishwa kwa udhahiri.

Shirika la uchukuzi wa baharini la China, COSCO lililoanzishwa kabla ya miaka 45 iliyopita ni shirika kubwa la serikali linaloshughulikia uchukuzi wa baharini na usambazaji wa bidhaa. Katika miaka ya karibuni, shirika hilo lilipata maendeleo ya haraka, na maeneo ya shughuli zake yamepanuka kwa mfululizo. Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Wei Jiafu akitoa mhadhara kwenye mkutano wa mwaka 2006 wa baraza la Asia la Boao, alisema, shirika lao linazingatia sana uwezo wa uvumbuzi wa usimamizi wa ndani na ujenzi wa utaratibu. Alisema,

"Ili kuleta maendeleo ya shirika hilo, kwanza kabisa tuliboresha muundo wa shirika unaoendana na utashi wa masoko. Kwa mfano, hivi sasa hisa za matawi ya shirika hilo zinamilikiwa na pande mbalimbali isipokuwa shirika kuu ambalo wingi wa hisa zake zinamilikiwa na serikali peke yake."

Hivi sasa, shirika la uchukuzi wa baharini la China limekuwa na meli za kisasa zaidi ya 600 zenye uwezo wa kubeba uzito wa tani milioni zaidi 35, na kuwa shirika la kimataifa ambalo uchukuzi wa mizigo unazidi tani milioni 300 kwa mwaka. Shirika hilo la uchukuzi si kama tu linashughulikia usafirishaji wa makontena, mizigo ya kawaida na maalumu pamoja na mafuta ghafi ya petroli katika miji ya Guangzhou, Shanghai, Tianjin, Qingdao, Dalian, Xianmen na Hongkong ya China, bali pia shughuli zake zimepanuliwa hadi nchi za Japan, Korea ya Kusini, Singapore, Marekani ya kaskazini, Ulaya, Australia na Afrika ya Kusini. Hivi sasa meli zenye alama ya "COSCO" zinaonekana kwenye bandari zaidi ya 1,300 za nchi zaidi ya 160 duniani.

Alipotathmini mafanikio ya shirika hilo, Bw. Wei Jiafu alisema, uvumbuzi ni nguvu inayohimiza maendeleo ya kasi ya shirika lao. Alisema,

"Maendeleo ya shirika yanategemea uvumbuzi wa teknolojia na kuinua ufanisi, na pia yanategemea utaratibu mpya wa usimamizi, na kuongeza hamasa kwa shirika ili kuongeza nguvu ya ushindani ya shirika kwenye masoko."

Mwaka 1998, faida lililopata shirika la uchukuzi wa baharini la China ilikuwa Yuan zaidi ya milioni 500 tu, lakini faida lililopata mwaka 2005 ilizidi Yuan bilioni 20, ikiwa ni ongezeko karibu mara 40.

Pamoja na maendeleo ya uwezo wa uvumbuzi wa kampuni na viwanda vya serikali ya China, nguvu ya ushindani ya kundi moja la viwanda vya serikali kwenye soko la kimataifa iliongezeka kwa mfululizo.

Kwenye mkutano mkuu wa baraza la Asia la Boao wa mwaka huu, washiriki wanaona kuwa viwanda vya serikali vya China vikiwa nguzo ya uchumi wa taifa, vinatakiwa kuvumbua mtindo mpya na kuongeza ubora wa maendeleo ili kuimarisha hadhi ya kuongoza kwenye uchumi wa taifa.

Idhaa ya Kiswahili 2006-05-30