Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-06 15:45:14    
Uchumi wa mapumziko wapata ongezeko jipya la uchumi wa China

cri

"Sekta ya mapumziko" bado lilikuwa ni neno ambalo lilikuwa halisikiki sana miaka michache iliyopita nchini China, lakini mwaka huu neno hilo limekuwa linatajwa na watu mara kwa mara; tena mapumziko, likizo na ununuzi vimekuwa ni masuala yanayotajwa mara kwa mara na serikali hadi watu wa kawaida.

Takwimu kutoka idara ya takwimu ya China zinaonesha kuwa, ikilinganishwa na uwekezaji wa mali zisizohamishika na biashara ya nje, ambazo ni sekta zenye ongezeko la kasi, kati ya nguzo tatu za maendeleo ya uchumi wa China, siku zote ununuzi ni sekta yenye nguvu dhaifu. Wataalamu wanaoshiriki kwenye maonesho ya kwanza ya sekta ya mapumziko duniani, wamesema hali ya kuzorota kwa sekta ya ununuzi nchini China sasa inabadilika haraka kutokana na ustawi wa uchumi wa mapumziko.

Kupanuka kwa kundi la wanunuzi, hususan la wanunuzi wa wakazi wa mijini, sekta ya mapumziko inastawi kwa haraka. Takwimu zilizotolewa na idara ya utalii ya China zinaonesha kuwa, shughuli za utalii, ambazo zinachukua nafasi muhimu ya sekta ya mapumziko, idadi ya watalii wa nchini mwaka 2005 ilifikia bilioni 1.2, na pato la shughuli za utalii lilikuwa ni Yuan bilioni 768.6. Kutokana na uhimizaji mkubwa wa sekta ya utalii kwa ununuzi na maendeleo ya uchumi, mikoa 24 ya China inachukulia shughuli za utalii kuwa nguzo ya sekta ya uzalishaji mali, sekta inayohimiza maendeleo au sekta bora.

Sekta ya mapumziko ni sekta inayohusu mambo yanayofanywa wakati wa mapumziko, shughuli za mapumziko na mahitaji ya mapumziko ikiwa ni pamoja na mambo ya burudani, utalii, huduma, utamaduni na michezo ya kuimarisha nguvu ya mwili, pamoja na sekta nyingine zinazohusiana nayo.

Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa shughuli za mapumziko cha taasisi ya utafiti wa sanaa ya China bibi Ma Huidi alisema, utatuzi wa tatizo la kuzorota na matatizo mengine yanayoukabili uchumi wa China, ni kuimarisha matarajio ya watu kuhusu ununuzi vitu wa hivi sasa na wa siku za baadaye, pamoja na kuongeza dhamira ya wakazi ya kununua vitu. Shughuli za sekta ya mapumziko zimefungua mikoba ya fedha ya watu, na kuleta nafasi nyingi za ajira kwa watu, na zimekuwa njia muhimu inayohimiza ununuzi wa vitu.

Takwimu zinaonesha kuwa wastani wa pato la kila mtu kwa mwaka ukifikia dola 1,000 za kimarekani, mtu atakuwa na mahitaji ya utalii. Katika mwaka uliopita, wastani wa pato la kila mtu ulifikia dola za kimarekani 1,700, hii inamaanisha kuwa uchumi wa mapumziko wa China umeingia kipindi cha maendeleo ya kasi ya uchumi wa mapumziko, jinsi ilivyo kama mafuta ya petroli yanavyotoka kwa nguvu kutoka kwenye kisima cha mafuta. Katika mwaka huo, siku za mapumziko zaidi ya 110 zilichochea sana shauku ya ununuzi ya watu wa China.

Mjumbe wa kamati ya elimu ya taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Yang Shengming anaona, kuanzishwa kwa "wiki ya dhahabu" ya mapumziko wa China kumeleta mageuzi mapya ya wazo kuhusu maendeleo ya uchumi, ambayo yamehimiza uboreshaji wa uchumi na muundo wa ununuzi. Alisema, "Kurekebisha uzalishaji mali kwa kufuata ununuzi wa watu, na kuongoza na kuamua mwelekeo wa masoko na kurekebisha muundo wa uzalishaji bidhaa kwa kufuata mahitaji ya watu, kumekuwa msingi wa kubuni sera za maendeleo endelevu ya uchumi kwa serikali."

Kukuza mahitaji ya nchini kumezingatiwa sana na serikali ya China. Mpango wa 11 wa maendeleo ya miaka 5 uliotolewa mwaka huu unasema, tunatakiwa kuwa na wazo la kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa njia ya kukuza mahitaji ya nchini, na kufanya mahitaji ya nchini, hususan mahitaji ya ununuzi ya watu kuwa msingi wa kuhimiza ongezeko la uchumi, na kubadilisha njia ya kuleta ongezeko la uchumi kwa kutegemea uwekezaji na usafirishaji wa bidhaa kwa nchi za nje kwa njia ya kuleta ongezeko la uchumi katika hali ya uwiano kati ya ununuzi na uwekezaji na kati ya mahitaji ya nchini na mahitaji ya nchi za nje.

Naibu waziri mkuu wa China Bibi Wu Yi alisema, kutokana na hali halisi ya China, ambayo inachukua maendeleo ya uchumi na jamii ya muda mrefu kuwa msingi, China na sekta husika zitakuwa na maendeleo makubwa zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2006-06-06