Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-07 20:12:03    
Mapishi ya uji wa viazi vikuu na figili

cri

Mahitaji

Mchele kikombe kimoja, viazi vikuu gramu 300, nusu kilo ya figili, maji vikombe kumi, kiasi kidogo cha chumvi, pilipili manga na giligilani

Njia

1. osha mchele, kasha ukaushe. Osha viazi vikuu na figili, nauvikate viwe vipande vidogo.

2. tia maji kwenye sufuria, baada ya kuchemka, tia mchele, vipande vya viazi vikuu na figili, korogakoroga, baada ya kuchemka, punguza moto kidogo endelea kuchemsha kwa dakika 10.

3. tia chumvi kwenye uji, pilipili manga na giligilani. Mpaka hapo uji huo uko tayari kunywewa.