Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-07 20:45:09    
Utaratibu mzuri wa kula unaweza kukinga saratani ya utumbo mkubwa

cri

Saratani ya utumbo mkubwa ni moja ya saratani za kawaida. Wagonjwa wengi wa saratani ya aina hiyo wapo barani Amerika ya Kaskazini, Oceania na Ulaya, ni wachache tu wapo katika mabara ya Asia na Afrika. Katika miaka 20 iliyopita, idadi ya wagonjwa wa saratani hiyo imeongezeka katika nchi nyingi duniani. Utafiti mpya umeonesha kuwa, saratani hiyo inahusiana zaidi na kuboreka kwa kiwango cha maisha, muundo na mwenendo wa kula chakula. Hivyo satarani hiyo inaweza kutokea kutokana na kula chakula tu. Lakini je ni vyakula gani vinavyoweza kusababisha saratani hiyo? Na kwa vipi watu wanaweza kujikinga na saratani hiyo kwa kurekebisha muundo wa chakula?

Mzee Ye Xianquan mwenye umri wa miaka 62 anayefanya kazi mjini Beijing ni mgonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa ya kipindi cha mwisho. Alipokumbuka chanzo cha saratani yake, alisema ni mwenendo mbaya wa kula chakula ndio uliomsababishia ugonjwa wake. Alisema:

"nilikuwa nakula mboga za majani kidogo. Toka mwaka 1982 hadi mwaka1984, nilikuwa ninafanya kazi huko Hongkong. Wakati huo, niliona kwa mara ya kwanza mikahawa ya Mcdonald's na KFC, basi nikaanza kupenda na kula chakula kingi cha haraka, kikiwemo tambi za haraka, hamburger na chips, pamoja na jibini na siagi."

Kama ilivyokuwa kwa Mzee Ye Xianquan, watu wengi wanapenda kula vyakula vilivyosafishwa kwa hatua kadhaa wa kadhaa kikiwemo chakula cha haraka. Lakini utafiti umeonesha kuwa, chakula cha aina hiyo kinahusiana kwa kiasi fulani na saratani ya utumbo mkubwa. Wataalamu wanaeleza kuwa, katika nchi za Amerika ya Kaskazini na Ulaya ambazo kuna wagonjwa wengi wa saratani ya utumbo mkubwa, ambao wanakula vyakula vingi vilivyosafishwa kwa hatua kadha wa kadha.

Kutokana na kusafishwa kwa hatua nyingi, vyakula vya aina hiyo vina mafuta mengi na selulosi (cellulose) chache. Utafiti umethibitisha kuwa, vyakula vya aina hiyo ni chanzo muhimu cha saratani ya utumbo mkubwa. Daktari mkurugenzi wa idara ya saratani katika hospitali ya Xiyuan ya Beijing Bi. Yang Yufei alisema,

"aina ya mafuta iliyopo kwenye chakula inayotiwa saturated aliphatic ina vitu vinavyoweza kusababisha saratani, aidha, mafuta mengi yakiingia kwenye mwili, yatahimiza utoaji wa maji ya nyongo, na maji hayo pia yanatoa vitu vinavyoweza kusababisha saratani kutokana na athari za vijidudu kwenye utumbo."

Nyama za aina mbalimbali ni chakula chenye mafuta mengi ambacho watu wanakula sana. Utafiti umeonesha kuwa, watu wanaokula nyama zaidi ya nusu ya kilo kwa siku, uwezekano kwa watu hao kupatwa saratani ya utumbo mkubwa unazidi kwa asilimia 30 hadi 40 kuliko watu wanaokula nyama kidogo. Aidha, wataalamu wanapendekeza kula nyama ya ndege au samaki badala ya nyama ya nguruwe na ng'ombe, kwa kuwa nyama ya ndege na samaki zina unsaturated aliphatic nyingi zaidi na saturated aliphatic kidogo, na zinaweza kupunguza uwezekano wa kupatwa saratani ya utumbo mkubwa.

Sababu nyingine kubwa kwa chakula kilichosafishwa kwa hatua nyingi kusababisha saratani hiyo ni kuwa kiasi kikubwa cha selulosi kinapungua kwenye hatua za usindikaji, na selulosi ni kitu ambacho kinaweza kuzuia kwa ufanisi ukuaji wa chembechembe za saratani. Daktari mkurugenzi wa idara ya saratani katika hospitali ya Xiyuan ya Beijing Bw. Yang Yufei alieleza:

"kwanza, vyakula vyenye selulosi vina vitamin nyingi ambayo tunaona ni kitu cha kuzuia ukuaji wa chembechembe za saratani; pili selulosi inachangia nguvu ya kazi ya utumbo mkubwa, na kupunguza muda wa vitu venye sumu kubaki kwenye utumbo mkubwa na kupunguza uwezekano wa kupata saratani hiyo."

Je ni vyakula gani vina selulosi nyingi zaidi na tunapaswa kula kiasi gani kila siku? Wataalamu wanaona kuwa, kila mtu anapaswa kupata gram 20 hadi 30 za selulosi kutoka kwenye chakula kila siku, ili kutimiza kiasi hicho, njia moja ni kula nafaka za aina mbalimbali, hasa mahindi, uwele na shayiri. Chakula cha mizizi kama karoti, maharage na viazi kina selulosi nyingi. Chakula kingine chenye selulosi nyingi ni matunda na mboga. lakini usipendelee kula aina moja tu, kula vyakula mchanganiko kunaleta uwiano wa lishe.

Licha ya vyakula hivyo, vyakula vya kukaanga pia vinaweza kusababisha saratani ya utumbo mkubwa. Naibu daktari mkurugenzi wa idara ya satarani katika hospitali ya XiYuan ya Beijing Bw. Wu Yu alisema:

"watu wengi wanapenda kula chakula cha kukaanga, lakini kwa kweli ni tabia mbaya. Mafuta ya kupikia yakichemshwa hadi kufikia nyuzi 160 sentigredi, yatatoa vitu vikali vinavyoweza kusababisha saratani, ikiwemo Benzopyrene."

Licha ya chakula cha kukaangwa, vyakula vya kuokwa na vya makopo pia havifai kuliwa sana. daktari mkurugenzi wa idara ya saratani katika hospitali ya Xiyuan ya Beijing Bw. Yang Yufei alisema:

"hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Kwa kuwa kutokea kwa saratani kunaendelea taratibu kwa muda mrefu, si lazima kuwa unaweza kupata saratani hiyo kwa kula mishikaki mara moja au mbili."