Mapendekezo ya nchi sita ya kutatua suala la nyuklia la Iran yaliyowasilishwa kwa Iran hivi karibuni na mwakilishi mwandamizi anayeshughulikia mambo ya kidiplomasia na sera za nchi za nje wa Umoja wa Ulaya yanafuatiliwa sana na vyombo vya habari vya Marekani na Ulaya. Mapendekezo hayo yanalenga kutatua suala la nyuklia la Iran kwa kuipatia Iran manufaa na adhabu kwa pamoja, ikiwa ni pamoja na kuruhusu Iran kusafisha uranium nchini humo. Wachambuzi wanaona kwamba mapendekezo hayo ni uamuzi mkubwa wa kurudi nyuma usiowahi kutolewa na Marekani na Umoja wa Ulaya, na kutokana na mapendekezo hayo, pengine "tatizo sugu" la nyuklia la Iran litatatuliwa.
Imefahamika kwamba uamuzi wa kurudi nyuma kwenye mapendekezo yaliyotolewa na Marekani na Umoja wa Ulaya ukiwa ni pamoja na kuruhusu Iran kuendelea na shughuli za kusafisha uranium nchini humo, lakini sharti lake ni kwamba lazima isimamishe shughuli zote nyeti za nyuklia zinazofanyika sasa, na kusimamisha shughuli za nyuklia zitakazoanzishwa katika mchakato wa mazungumzo ya nyuklia hadi Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki litakapokuwa limefanya uamuzi baada ya uchunguzi wa shughuli za nyuklia na kuhakikisha shughuli za nyuklia za Iran kweli zinafanyika kwa ajili ya matumizi ya amani. Isitoshe kwa mara ya kwanza Marekani imekubali kushiriki kwenye mazungumzo ya suala la nyuklia la Iran ikiwa pamoja na nchi za Umoja wa Ulaya.
Hapo awali, Marekani ilikuwa haitambui Iran kuwa na haki ya kutumia nishati ya nyuklia kwa amani, hata Umoja wa Ulaya ambao ingawa ulitambua haki hiyo lakini pia haukuruhusu Iran iwe na shughuli za kusafisha uranium, kwani teknolojia hiyo inaweza kutumika kuzalisha umeme na pia kutengeneza silaha za nyuklia. Lakini kwa nini sasa Marekani na Umoja wa Ulaya zimebadilisha sana msimamo kwa Iran?
Kwanza, Iran inamiliki mafuta, ambacho ni kitu muhimu kwa Marekani na Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya unategemea sana mafuta ya Iran. Mwaka 1999 hadi 2005, Umoja wa Ulaya uliingiza mafuta kutoka Iran yenye thamani ya Euro bilioni 10.1 kutoka bilioni 3.8, kiasi cha kutegemea mafuta ya Iran kimeongezeka kwa 165%. Zaidi ya hayo, bidhaa za Umoja wa Ulaya zilizouzwa nchini Iran ziliongezeka hadi 42% ya soko la Iran mwaka 2005 kutoka 36% mwaka 2000. Kama hatua za kuiadhibu Iran kiuchumi au kwa vita zitachukuiwa, nchi za Umoja wa Ulaya nchi zitakazoathirika zaidi. Kutokana na sababu hiyo, Umoja wa Ulaya ulikuwa unashikilia njia ya kidiplomasia kutatua suala la nyuklia la Iran.
Kadhalika, kama suala la nyuklia la Iran likiingia kwenye hali mbaya, bei ya mafuta itapanda sana. Kwa sababu theluthi moja ya mafuta duniani yanasafirishwa kutoka mlango bahari wa Hormuz, kama mlango huo ukifungwa, bei ya mafuta ingepanda hadi kufikia dola za Kimarekani 150 kwa pipa. Kwa makadirio, kama mlango bahari huo ukifungwa kwa miezi mitatu, thamani ya bidhaa zilizozalishwa nchini Marekani zitashuka kwa 4% hadi 5% na kiasi cha ukosefu wa ajira kitaongezeka kwa 2%.
Pili, Marekani inahitaji Iran katika suala la Iraq. Mauaji yanatokea mara kwa mara nchini Iraq, hali ya usalama inakuwa mbaya bila kuweza kuboreshwa. Huu ni usumbufu mkubwa wa Marekani ambayo inalaumiwa nchini na nchi za nje, na kama Marekani ikitaka kujinasua kutoka hali hiyo lazima ifikirie athari kubwa ya Iran kwa madhehebu ya Shiya nchini Iraq.
Tatu, Kama chama cha rais Bush wa Marekani kikitaka kushinda kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba mwaka huu, ni lazima Bush apige hatua katika utatuzi wa suala la nyuklia la Iran, kuiadhibu Iran kwa vita hakika sio chaguo la kwanza, kwani vita vya Iraq iliyolizamisha jeshi la Marekani ndani ya matope vimewakirihisha sana wananchi wa Marekani.
Russia, China na nchi nyingine nyingi zinashikilia kutatua suala la nyuklia la Iran kwa njia ya mazungumzo. Marekani imetambua kwamba itakuwa vigumu kupata msimamo wa pamoja dhidi ya Iran.
Kurudi nyuma kwa nchi za Magharibi hakika ni ushindi mkubwa wa Iran. Kiini cha mgogoro wa suala la nyuklia la Iran uliodumu zaidi ya miaka mitatu ni kwamba Iran iwe na haki ya kusafisha uranium au vipi? Hivi sasa nchi za Magharibi zimekubali haki yake hiyo. Kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 8 rais Ahmadinejad wa Iran alisema, "Watu wa Iran wamewashinda watu wa Magharibi katika mapambano" na kusema, "Iran iko tayari kufanya mazungumzo na pande zote husika kuhusu masuala yanayovutia".
Hata hivyo, wachambuzi wanaona kwamba bado ni mapema kusema kama Iran itakubali "mapendekezo ya nchi sita". Maofisa wa Ulaya na Marekani walidokeza kwamba muda wa miaka kadhaa utahitajika tokea kusimamisha shughuli za kusafisha uranium wakati wa mazungumzo yanapofanyika hadi kurudisha shughuli hizo baada ya kuhakikishwa na Shirika la Kimataifa la Nishati la Atomiki, lakini je muda huo mrefu utakubaliwa na Iran? Hatuna uhakika.
Idhaa ya kiswahili 2006-06-09
|