Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-09 18:27:09    
Umoja wa Ulaya wapenda kufanya mazungumzo na mashauriano ili kutatua matatizo yaliyopo kwenye ushirikiano na China katika sekta za uchumi na biashara

cri

Mjumbe wa Kamati ya biashara ya Umoja wa Ulaya Bwana Peter Mandelson tarehe 8 kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hapa Beijing alisema kuwa, kuendeleza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na China ni muhimu sana kwa Ulaya, Umoja wa Ulaya unapenda kufanya mazungumzo na mashauriano ili kutatua matatizo yaliyotokea katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye sekta za uchumi na biashara.

Bwana Mandelson anafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 5. Wakati wa ziara yake hiyo, Bwana Mandelson na waziri wa biashara wa China Bwana Bo Xilai wamebadilishana maoni kuhusu Umoja wa Ulaya kutoza ushuru wa kupinga maporomoko ya bidhaa za viatu vyenye bei nafuu vya China, uhifadhi wa hakimiliki ya ujuzi nchini China na mazungumzo ya Doha ya shirika la biashara duniani na masuala mengine. Bwana Mandelson alisema, Umoja wa Ulaya unapenda kufanya mazungumzo na mashauriano ili kutatua matatizo yaliyotokea kwenye ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya katika sekta za uchumi na biashara. Alisema:

Kuendeleza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na China ni muhimu sana kwa kila mtu barani Ulaya, kwani tunasaidiana katika maslahi yetu. Kuendeleza uhusiano huo pia ni changamoto kubwa sana ya kiuchumi na kisiasa, tunapaswa kufanya mazungumzo na mashauriano ili kuondoa matatizo yalitokea katika ushirikiano huo.

Bwana Mandelson alisema hivi sasa barani Ulaya kuna maoni ya misimamo mikali, ya kwanza ni kuhofia kuimarishwa kwa nguvu ya kiuchumi ya China kutasababisha mapambano ya kijeshi na kidiplomasia kati ya China na Ulaya; ya pili ni kuona kuwa mapinduzi ya kiuchumi yanafanyika duniani, Bara la Ulaya linapaswa kutafuta mgao na faida kwenye soko bila kujali chochote. Bwana Mandelson anaona maoni hayo ya misimamo mikali yote ni ya makosa, Bara la Ulaya linapaswa kuwa na imani juu ya uwezo wake wa ushindani, na kujenga uhusiano wa kunufaishana na China.

Katika miaka ya hivi karibuni uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya umeendelea kwa haraka, katika mwaka 2004 na 2005, kwa miaka miwili mfululizo, Umoja wa Ulaya umekuwa mwenzi mkubwa kwanza kwa China katika sekta za biashara, na hivi sasa China imekuwa mwenzi mkubwa wa pili wa biashara kwa Umoja wa Ulaya. Lakini wakati huo huo mikwaruzano ya kibiashara kati ya pande hizo mbili pia inaongezeka siku hadi siku. Tokea mwezi Julai mwaka jana, Umoja wa Ulaya ulifanya uchunguzi kwa kupinga maporomoko ya bei ya bidhaa za viatu vya China, ulipotoa uamuzi wa hatua ya mwanzo, Umoja wa Ulaya ulikanusha bila kuthibitisha kwa makini hadhi ya uchumi wa soko huria ya makampuni yote ya China yaliyojibu mashitaka, na kutoza ushuru wa muda hata kufikia asilimia 19.4. China imetoa malalamiko yake juu ya hiyo, na kuutaka Umoja wa Ulaya uyatendee makampuni ya viatu ya China kwa haki na halali wakati wa kutoa uamuzi wa mwisho.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 8, Bwana Mandelson alisema, Umoja wa Ulaya utashughulikia kwa makini matakwa ya China, na utafanya juhudi katika kujadili namna ya kuyawezesha makampuni ya China yanayojibu mashitaka ambayo yametimiza masharti yaweze kupewa hadhi ya uchumi wa soko huria.

Uhifadhi wa hakimiliki ya ujuzi ni suala linalozungumzwa mara kwa mara katika majadiliano kati ya Umoja wa Ulaya na China. Bwana Mandelson alisema, Umoja wa Ulaya unasifu serikali ya China kwa juhudi zake za kuhifadhi hakimiliki ya ujuzi, na unapenda kuimarisha ushirikiano na China katika uhifadhi wa hakimiliki ya ujuzi. Alisema:

Nimetiwa moyo na sera zilizotolewa na serikali ya China kuhusu uhifadhi wa hakimiliki ya ujuzi na hatua zinazochukuliwa na serikali ya China. Hivi sasa tunatakiwa kutatua masuala mengi, natumai ushirikiano kati ya Umoja na Ulaya utakuwa barabara zaidi, ili matatizo hayo yatatuliwe vizuri.