Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-12 16:49:41    
Sehemu ya Lao Cheng Huang Miao mjini Shanghai

cri

Katika sehemu ya katikati mjini Shanghai, kuna sehemu moja maalum iitwayo Laochenghuangmiao, ambapo kuna bustani yenye hali tulivu, maduka mengi yaliyoanzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita, na pia kuna mikahawa mingi ya chakula na chai. Sehemu hiyo imekuwa kama alama moja ya mji wa Shanghai.

Zamani hekalu la kuabudiwa kwa mungu wa kulinda miji wa dini ya kidao ya China liliitwa kuwa Hekalu la Chenghuang. Katika sehemu ya Laochenghuangmiao mjini Shanghai, kweli kuna hekalu moja la Chenghuang lililojengwa mwanzoni mwa karne ya 15, katika miaka mia kadhaa iliyopita, kwenye sehemu ya hekalu hilo yalikuwepo maduka mengi, ambapo wafanyabiashara wengi walipenda kukusanyika huko. Ndiyo maana wakazi wa Shanghai waliita sehemu hiyo kuwa Laochenghuangmiao, maana yake kwa kichina ni hekalu la kale la kuabudiwa kwa mungu wa kulinda miji. Hivi sasa sehemu ya Laochenghuangmiao kwa wakazi wa Shanghai inamaanisha sehemu ya makazi ya zamani pembezoni mwa hekalu la kale, sehemu hiyo inawavutia watu wengi na kupendwa na wakazi wa Shanghai.

Katika sehemu hiyo, kuna njia moja yenye urefu wa mita kumi kadhaa, kandoni mwa njia hiyo kuna mikahawa mingi ya vyakula, vyakula hivyo karibu ni vya aina zote za vyakula vya kienyeji huko Shanghai. Mkahawa wa Mantou wa Nanshang unajulikana zaidi kuliko mingine, kwani malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili alipofanya ziara mjini Shanghai aliwahi kutembelea mkahawa huo. Mkahawa huo ni rahisi kupatikana, watalii wakiangalia kwa makini kidogo wataweza kuona mbele ya mkahawa huo huwa kuna msururu wa wateja wanaosubiri kuingia ndani.

Chakula cha Mantou kinachouzwa kwenye mkahawa huo kwa kweli ni chakula kinachoitwa Baozi na wachina wa kaskazini, yaani vitafunwa vya kichina. Wateja wengi wanapenda kula chakula cha Baozi cha mkahawa huo, lakini wanapaswa kusubiri kwa muda kutokana na wateja wengi. Bwana Steve Omara kutoka Canada ambaye anafanya kazi mjini Shanghai, mara kwa mara anakwenda kwenye mkahawa huo kula Baozi, alisema siku moja alisubiri kwenye msururu kwa saa moja.

Nilisubiri kwa saa moja na kuingia ndani kula chakula cha Baozi, kwani chakula cha Baozi cha mkahawa huo ni chakula kinachojulikana sana mjini Shanghai, wateja wanastahili kusubiri. Nimekula kwenye mkahawa huo kwa mara kadhaa, naona chakula cha Baozi cha mkahawa huo kweli ni kitamu sana.

Mkahawa wa Mantou wa Nanshang umekuwa na historia zaidi ya miaka 100, chakula cha Baozi cha mkahawa huo kilitengenezwa kuwa kitafunwa kidogo, umbo lake kama ni mnara, ganda lake ni jepesi kama karatasi, na ladha yake kweli ni tamu sana.

Wapishi wa mkahawa huo pia wanaweza kutengeneza chakula cha Baozi cha aina mbalimbali chenye ladha nzuri sana.

Hivi sasa mjini Shanghai vyakula vingi vya kienyeji vinaweza tu kupatikana katika sehemu ya Laochenghuangmiao, vyakula vya aina mbalimbali vinavyopendeza vinaweza kuwawezesha wakazi wa Shanghai wakumbuke siku za zamani. Kijana Ling Min alisema, kila mara anakwenda sehemu ya Laochenghuangmiao kula vyakula vya jadi vya aina mbalimbali kwa ajili ya kukumbuka siku za zamani. Alisema:

Nakuja sehemu hii kula vyakula vya aina mbalimbali vya jadi naona kama ninaishi katika siku za zamani. Sehemu hiyo ya Laochenghuangmiao ina hali tofauti na sehemu nyingine, vyakula vingine vya jadi havitaweza kupatikana katika mikahawa ya sehemu nyingine mjini Shanghai, vyakula hivyo kweli ni kama alama moja ya mji wa Shanghai.

Baada ya kula vyakula mbalimbali kwenye njia hiyo iliyojaa mikahawa mbalimbali, tunaweza kutembelea njia nyingine iliyojengwa zamani. Njia hiyo iliyo karibu sana na njia iliyojaa mikahawa ina upana wa zaidi ya mita 3 ambayo ilijengwa kwa mawe na matofali. Kwenye kando mbili za njia hiyo kuna maduka mengi ambayo karibu yote ni ya nyumba za rangi nyekundu zenye ghorofa mbili, kila duka limening'inizwa chapa mbalimbali za mauzo ya vitu mbalimbali, chapa hizo zinawavutia sana watu. Na maduka hayo yote ni majengo yenye michongo ambayo yanaonesha mtindo dhahiri ya ujenzi wa kichina.

Sehemu ya Laochenghuangmiao ni sehemu yenye mkusanyiko wa watu, mikahawa na maduka, lakini labda watalii kutoka nje hawawezi kutarajia kwamba katika sehemu hiyo kuna bustani moja yenye utulivu ambayo ilijengwa zamani sana. Bustani hiyo iitwayo Yuyuan imekuwa na historia ya zaidi ya miaka 400, inasemekana kuwa bustani hiyo ilijengwa na ofisa mmoja wa zama za kale kwa ajili ya baba yake mzazi.

Bustani Yuyuan ina eneo la hekta 2, ndani ya bustani kuna majengo zaidi ya 20, majengo hayo yenye maroshani marefu na mafupi yanaegemeana na kupatana na vilima na mawe na miti inayositawi. Ndani ya bustani hiyo, kuna kilima kilichojengwa kwa mawe yenye rangi ya manjano tani elfu kadhaa kinachojulikana sana, urefu wa kilima hicho ni mita 14, kilima hicho ni kikubwa zaidi kuliko vingine, ambacho kilijengwa zamani zaidi kuliko vingine katika sehemu ya kusini ya Mto Changjiang, umbo lake linapendeza sana.

Katika bustani hiyo iliyojengwa katika zama za kale, kila mti una historia yake, hata kila jengo lina hadithi yake, ukitembelea katika bustani hiyo, wafanyakazi wa usafishaji huwa wanaweza kukusimulia hadithi moja. Mfanyakazi mzee wa usafishaji wa bustani hiyo Bwana Zhu alipotoa maua yaliyoanguka kwenye dimbwi ndani ya bustani, alitueleza hadithi kuihusu jengo jekundu la ghorofa mbili lenye michongo, alisema:

Mbele ya jengo hilo kuna maua mengi ya aina mbalimbali, hivyo jengo hilo linaitwa Jengo la Wanhualou, maana yake ya kichina ni Jengo lenye maua mbalimbali ya aina nyingi. Mbele ya jengo hilo kuna miti miwili ya Gingko na Lotus Magnolia, mwanzoni miti hiyo miwili yote ni Gingko, mmoja wa kiume na mwingine wa kike, lakini mti mmoja wa kike ulipigwa na radi ukafa, ndiyo maana baadaye watu walipanda mti mwingine wa Lotus Magnolia.

Ndani ya Bustani ya Yuyuan watu wanaotembea wanaweza kukaa kila mara, ambapo wanaweza kuangalia vitu mbalimbali, kuta na mapaa ya majengo yaliyotiwa nakshi mbalimbali, kuangalia miti mikubwa iliyopandwa miaka mia kadhaa iliyopita, ama kujiburudisha katika kuwalisha samaki waliofugwa ndani ya bwawa, kweli wanaweza kujisikia raha mustarehe.