Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-13 19:40:20    
Njia mpya ya uwekezaji kwa viwanda vya China

cri

Katika kipindi fulani kilichopita, nchi zilizoendelea zilipenda sana kununua viwanda vya nchi za nje. Lakini tokea mwanzoni mwa mwaka uliopita, viwanda vya China vyenye teknolojia ya kisasa vilitenda vitendo vya kushtusha vya kununua viwanda vya nchi za nje. Je, kwa nini viwanda vya China vinawekeza katika nchi za nje? Viwanda hivyo vya China vitakabiliwa na matatizo gani katika masoko ya nchi za nje?

Mwezi May mwaka uliopita, kampuni ya Legend, ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa nchini China katika sekta ya uzalishaji wa kampyuta, ilinunua shughuli zote za kampyuta za binafsi za kampuni ya IBM kwa dola za kimarekani bilioni 1.25, baada ya kuchukua shughuli hizo za kampuni ya IBM, kampuni ya Legend inachukua nafasi ya 3 katika sekta ya uzalishaji kampyuta duniani kwa mauzo ya dola za kimarekani bilioni 13 kwa mwaka. Naibu mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Legend Bw. Liu Xiaolin alipoeleza ununuzi huo alisema,

"Kampuni ya Legend inafahamu sana soko la China, nchini China watu wengi sana wanajua nembo ya Legend, ambayo imechukua nafasi kubwa sana ya soko la China. Nafasi inayochukua kampuni ya IBM katika soko la China ni ndogo sana ikilinganishwa na ile ya kampuni ya Legend. Mauzo makubwa ya kampuni ya Legend yako nchini China, wakati wingi wa kampyuta zinazozalishwa na kampuni ya IBM zinauzwa katika masoko ya nchi za nje, katika upande wa bidhaa, kampyuta za binafsi za mezani za kampuni ya Legend ni bora, wakati kampuni ya IBM inajulikana zaidi kwa laptop kampyuta. Kutokana na hali ya namna hiyo, hakuna uwezekano mkubwa wa mgongano kati ya kampuni hizo mbili, bali ni kwamba uunganishaji wa kampuni hizo mbili utachukua sifa zote nzuri za kampuni hizo mbili."

Ununuzi wa kampuni ya Legend ni sehemu moja ndogo za shughuli za viwanda vya China za kununua viwanda vya nchi za nje tokea mwaka jana. Kampuni ya mafuta ya asili ya petroli ya China kununua kampuni ya petroli ya asili ya PK ya Kazakstan na kampuni ya magari ya Nanjing kununua kampuni mashuhuri ya Rover ya Uingereza ni mifano inayoonesha nguvu imara ya viwanda vya China. Pamoja na maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, viwanda vya China vimekomaa zaidi, si kama tu vinachukua nafasi kubwa ya soko la nchini, bali vinashika njia ya kununua viwanda vya nchi za nje.

Msaidizi wa waziri wa biashara wa China Bw. Chen Jian alisema, hesabu ya uwekezaji katika nchi za nje mwaka jana, inaonesha, ununuzi wa viwanda katika nchi za nje umekuwa mkazo uliotiwa katika shughuli za uwekezaji za viwanda vya China katika nchi za nje.

"Mwaka 2005, uwekezaji wa China katika nchi za nje ulifikia dola za kimarekani bilioni 6.9, zikiwa ni ongezeko la 26% kuliko mwaka uliotangulia, dola za kimarekani bilioni 2.3 kati yake zilitumika katika kununua viwanda vya nchi za nje. Maendeleo ya kasi ya uwekezaji wa China katika nchi za nje, na kupanuka kwa haraka kwa masoko, si kama tu vilihimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya China, bali pia vilichangia marekebisho ya muundo wa uzalishaji na upangaji wa uzalishaji bidhaa duniani."

Habari zilisema, kampuni na viwanda vipya vya China vyenye uwezo wa utafiti na uvumbuzi vya China, vikiwemo vile vinavyojulikana sana hapa nchini kama kampuni za Zhongxing, Huawei, haier, Hisense na Ligend, zimeanza kutekeleza mikakati ya kujiendeleza katika nchi za nje kwa njia ya uwekezaji na ushirikiano wa uendeshaji. Sekta nyingi bora za China zikiwa ni pamoja na za vyombo vya umeme vinavyotumika majumbani mwa watu, viwanda vya nguo, viwanda vya ushonaji nguo na ushindikaji wa chakula, zimeanzisha viwanda au kampuni katika nchi za nje, ambavyo vinahamisha ziada ya uwezo wa uzalishaji, mali-ghafi na vipuri kwenye masoko ya kimataifa, na kuwa vituo vya uzalishaji kwa mashirika ya biashara yaliyoko nchi za nje.

Mkurugenzi wa idara ya uwekezaji wa baraza la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa Bw. Khalil Hamdani alisema, katika miaka ya karibuni China imejitokeza duniani kununua viwanda vya nchi za nje.

"Kati ya mwaka 1999 na mwaka 2005, kwa uchache kabisa kampuni za China zimenunua viwanda 277 duniani, ambazo zimetia for a kwenye bara la Asia. Mbali na hayo, ununuzi wa China katika nchi zilizoendelea umeongezeka kwa haraka, hatua ambayo inaonesha kuwa uwekezaji wa China katika nchi za nje, unaelekea kununua viwanda na kampuni maarufu, teknolojia ya kisayansi na zana za uzalishaji, yakiwa ni pamoja na masoko ya nchi zilizoendelea."

Ni dhahiri kuwa harakati za kujiendeleza kwa viwanda vya China katika nchi za nje zilipita njia yenye shida. Mwaka 2005, kutokana na shinikizo la kisiasa nchini Marekani, kampuni ya China ya uchimbaji visima vya mafuta ya asili ya petroli kwenya bahari, ililazimika kuacha ununuzi juu ya kampuni ya mafuta ya asili ya petroli ya Unocao ya Marekani. Mwaka huu, kampuni ya Legend, ambayo ilifanikiwa kununua kampuni nchini Marekani, ilipatwa na matatizo katika uendeshaji wa shughuli zake nchini humo. Mwanzoni mwa mwaka huu, kampuni ya Legend ilipata oda ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani ya kampyuta zenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 10, lakini biashara hiyo ya kawaida ilizuiliwa na baadhi ya watu nchini Marekani, hata baadhi ya wabunge wa taifa walisema, kununua kampyuta za Legend kutaleta kitishio kwa usalama wa Marekani. Kutokana na shinikizo hilo, ingawa wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabatili oda hiyo, lakini ilipeleka kamyuta hizo kwa idara nyingine, tena ilisema itakagua kwa makini oda ya kampyuta za aina hiyo.

Naibu mkuurugenzi mkuu wa kampuni ya Legend Bw. Liu Xiaolin alisema, ingawa walipatwa kizuizi kikubwa cha kisiasa, lakini kampuni na viwanda vya China havitaacha wazo lao la kuwa kampuni za kimataifa

"Madhali kampuni na viwanda vya China viingie nchi za nje kama kampuni na viwanda vingi vya Japan na Korea ya Kuisini, kufanya nchi za nje zione nguvu ya uchumi wa China na kuona kuwa kampuni na viwanda vya China vinaendesha shughuli zake kwa haki, bila kuficha na kufuata kanuni za kimasoko katika nchi za nje, ndipo wanunuzi wa nchi za nje watapenda kampuni za China ikiwemo kampuni ya Legend, na kuondolewa mashaka yao."

Wataalamu wanasema, ingawa ununuzi wa kampuni za China katika nchi za nje umefuatiliwa na watu wengi duniani, lakini nafasi inayochukua China duniani bado ni ndogo sana, hadhi ya ununuzi ya kampuni ya China duniani bado iko nyuma. Ikiwa tunakadiria uwezo wa ununuzi wa kampuni za China katika nchi za nje kwa kuangalia pato la nchini la China au kwa thamani ya biashara ya nje, basi ununuzi wa viwanda wa China katika nchi za nje ukitaka kufikia kiwango cha Uingereza au Marekani, kwa uchache kabisa uta, pato la China au thamani ya biashara ya nje ya China vinatakiwa kuongezeka kwa mara 10.