Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-13 20:01:01    
Barua za wasikilizaji 0611

cri

Msikilizaji Dominic Ndugu Muholo P.O.Box 1990. Kakamega,Kenya anasema katika barua yake kuwa, Mimi nikiwa msikilizaji wenu wa Radio China kimataifa, nawatakia afya bora na heri njema katika huu mwaka mpya wa 2006 wafanyi kazi na watangazaji wote wa Radio China kimataifa kwa kazi nzuri wanaofanya.

Narudisha pongezi kwa barua zenu nilizopata hivi karibuni zilizoandikwa tarehe 12/12/2005. nilipata moja tarehe 28/3/2006 na nyingine tarehe 30/3/2006 pamoja na kadi ya ukumbusho wa kisiwa cha Taiwan? kisiwa cha hazina cha China.

Pia nashukuru serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa ufadhili wanaotupatia kila mara hasa tukikumbuka uwanja wetu kwa michezo wa kimataifa wa Kasarani uliojengwa karibu miaka 20 iliyopita ni wa hali ya juu sana, ambapo tumewahi kuandaa michezo ya jumuiya ya madola ya bara la Afrika.

Na sasa hivi wachina wanatutengenezea barabara magharibi mwa Kenya, kwa hakika hii inaonesha uhusiano na urafiki mkubwa kati ya nchi hizi mbili. Pia naomba waendelee kutufadhili kwa kila sekta ili uchumi wa nchi yetu ipate kumairika na kupunguza umaskini inayotukabili kwa kiwango cha juu sana.

Ninashukuru pia kwa kituo cha pekee Barani Afrika cha utangazaji kilichojengwa Kenya na ikazinduliwa mwishoni mwa mwezi Januari 2006, kwa kazi nzuri inayofanya kwa kushirikiana na kituo cha utangazaji cha K.B.C Kenya, na ikiwa ni Radio China kimataifa F.M. Nairobi, Kenya.

Pia napenda kusema kuwa kituo hicho cha Radio China kimataifa F.M. Nairobi,Kenya, haisikiki magharibi mwa Kenya hata kidogo. Naomba idara husika kuchunguza jambo hili na ikiwezekana watuwekee mitambo Kakamega, Eldoret na kisumu.

Kwa kumalizia nawakumbusha wenzetu wa Bungoma (salama club) waache salamau za jamaa na ukoo kwa vile zimepitwa na wakati na badala yake wakumbuke mashabiki wa Radio China kimataifa nao watasalimiwa na mabingwa wa kimataifa.

Ujumbe, mtaka cha mfunguni sharti ainame!

Msikilizaji Geoffrey Wandera Namachi wa Co-op LTD Nairobi SLP 57333 Nairobi,Kenya anasema katika barua yake kuwa, hakika CRI 91.9 FM hapa Nairobi Kenya inasikika vizuri sana. Matangazo hayo yanasikika kwa njia maridhawa. Na kwa hilo, ndio sababu napenda kusikiliza CRI kila siku. Mimi ni msikilizaji marufu na tena shabiki mkubwa wa CRI. Kwa miaka mitatu mfululizo nikichangia kwa maoni na mapendekezo kutoka kwa matangazo na vipindi. Barua zangu nyingi zilisomwa na wafanyakazi wa CRI walioko hapa Nairobi Kenya. Kweli tumedumisha urafiki mwema kati yangu na wafanyakazi wa CRI. Jambo ambalo nimeyashuhudia ni kwamba watu wa China hawana ubagusi wowote hata kidogo.

Kutokana na kuwepo CRI hapa Kenya kumenifunza mengi. Kwa sasa naelewa machache kuhusu China bara na Taiwan. Lengo langu kubwa ni kuifahamu China na vitogoji vyake. Kuhusu swala la waziri mkuu wa Japan Bwana Jorekero Zeizumi kwenda kwenye hekalu kutoa heshima kwa wahalifu wa vita halikufurahisha dunia nzima. Hata hivyo tarehe 27/3/3006 Bwana Jorekero Zeizumi alisisitiza kuwa atakwenda tena kwenye hekalu la zekuni kutoa heshima zake kwa mizimu ya wahalifu wa kivita kabla muda wake kukamilika. Alipohojiwa na wandishi wa habari, Bwana Jorekero alisema kuwa swala hilo ni lake kibinafusi.

CRI 91.9 FM imenipa furusa nzuri ya kujua viongozi wa China. Kwa vile hupenda kufuatilia matangazo, nafahamu kuwa Chama tawala cha kikoministi cha China kinaongozwa na katibu mkuu wa kamati kuu ya chama Bwana Hu Jintao, waziri mkuu wa China ni Bwana Wen Jiabao, waziri wa mambo ya nje wa China ni Bwana Li Zhao Xing, waziri wa kilimo ni Bwana Bo Xilai, na waziri wa maji Bwana Yang Shuchen naye waziri wa fedha Bwana Jin Renqing. Hakika CRI 91.9 FM matangazo yenu nayafuatilia mbio zaidi. Kama sio CRI, hakika singelijuwa hayo mazuri ya dunia.

Niliweza pia kufuatilia ziara ya Rais Hu Jintao wa China akiwa Hanoi, Vietnam. Bwana Tao ndiye rais wa kwanza kuhutubia bunge la Vietnam. Akiwa mwenyekiti wa Chama tawala cha kikoministi cha China, alisema kuwa maendeleyo ya China hayawezi kumdhuru mtu yeyote au taifa lolote lile. Aliongeza kusema kuwa kudumisha maendeleyo ya China kutasaidia kuleta amani, utulivu, na usitawi, wa demokirasia kote duniani.

Katika harakati hizo, ili CRI itambue kuwa matangazo hayo huwa nayafuatilia siku hadi siku, hapa kuna baadhi ya mikoa na miji ambayo ina shuguli nyingi za kila siku nchini China. Kwa mfano mkoa wa Liangning uliopo kaskazini mashariki mwa China, una vijiji vingi. Vilevile kuna mkoa wa Tibeti ambao unapendwa na watali wengi sana. Pia kuna sehemu kama vile Beijing, Hongkong, Taiwan, Shanghai, Hangzhou, Tianjin Hubei na Baitou.

Kuhusu swala la kongozi wa Taiwan, Bwana Chen Shuibian kutaka kukomesha kamati ya mazungumzo ya muungano wa taifa, kuhusu swala la China na Taiwan, matamshi yake Bwana Shuibian hayakufurahisha ulimwengu nzima.

Mwaka 2005 China ilifanikiwa kufanya urafiki na zaidi ya mataifa 200 kote duniani. Na katika hali hiyo CRI ilitupa furusa ya shindano la chemsha bongo ambalo tungali tunasubiri matokeyo yake; vilevile pia kuna shindano lingine kuhusu kuzinduliwa kwa CRI 91.9FM Nairobi Kenya, kuhusu maneno aliyosema mkurugenzi mkuu wa CRI. Shindano hilo lilifanyika tarehe 5, 12 na 19 mwezi wa pili mwaka 2006. mashindano yote nilishiriki kama kawaida, na nasubiri matokeyo yake.

Maendeleo ya China yanapanuka siku hadi siku, uchumi wa China unaongezeka kila siku. Katika matangazo ya hivi karibuni, tulidokezewa kuwa China imeanzisha kujenga reli ya Sumaku yenye urefu wa kilomita 175 kutoka Shanghai hadi Hangzhou. Hii itasaidia wakazi wa sehemu hizo mbili kwa urahishishaji wa biashara haswa wakulima na wafanya biashara ndogo ndogo.

Pongezi na shukurani nyingi kwa China na watu wake. Hongera watangazaji wa CRI, vilevile mama Chen, Fadhili Mpunji hali kadhalika Josephine Liyumba. Pongezi zingine ni kwa balozi wa China nchini Kenya Bwana Guo Jongli kwa wajibu mkubwa anaotekeleza nchini Kenya.

Mwisho nafurahia vipindi, kusema kweli mpangiliyo au ratiba ya vipindi ni bora zaidi. Sehemu ya sanduku la barua inapendwa na wasikilizaji wengi sana. Kwa kuwa ndio sehemu pekee inayosomwa barua za wasikilizaji. Maoni yangu ni kuwa pole pole ndio mwendo.

Idhaa ya Kiswahili 2006-06-13