Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-14 18:12:29    
Mapishi ya asparaga pamoja na pilipili za rangi mbalimbali

cri

Mahitaji

Asparaga gramu 200, pilipili hoho gramu 50, pilipili mboga gramu 50, pilipili ya rangi ya manjano gramu 50, kiasi kidogo cha wanga wa nyama ya ng'ombe, chumvi na vipande vya vitunguu maji.

Njia

1. osha asparaga, na ondoa mzizi wake, halafu uikate iwe vipande. Kata pilipili hoho, pilipili mboga na pilipili ya rangi ya manjano ziwe vipande.

2. tia mafuta kwenye sufuria washa moto mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia vipande vya vitunguu maji, korogakoroga, halafu tia vipande vya asparaga korogakoroga kwa dakika mbili, tia vipande vya pilipili hoho, pilipili mboga na pilipili ya rangi ya manjano na endelea korogakoroga, tia chumvi na wanga wa nyama ya ng'ombe, korogakoroga kisha pakue, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.