Kutokana na mpango wa usalama aliotoa waziri mkuu wa Iraq Bw. Nuri al-Maliki, jeshi la polisi la Iraq pamoja na jeshi la Marekani lililoko nchini Iraq, tarehe 14 mwezi huu yalianzisha operesheni kubwa ya usalama, ambayo haijawahi kutokea tangu kuangushwa kwa utawala wa Sadam Hussein mwaka 2003.
Bw. Maliki alitangaza kuwa, operesheni hiyo itakuwa ya muda mrefu. Atarefusha muda wa hali ya hatari inayozuia watu kutotembea nje wakati wa usiku na kuzuia watu wasiwe na silaha, licha ya hayo hatua kali zimechukulia za kutoa pigo kali dhidi ya magaidi na wafuasi wa kundi la Al Qaeda.
Ofisa mmoja wa jeshi la Iraq, ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema, askari kiasi cha elfu 20 wa Iraq, askari wa usalama wa wizara ya mambo ya ndani elfu 50 na askari elfu kadhaa wa jeshi la Marekani wameshiriki katika operesheni hiyo. Ofisa wa usalama wa Iraq alidokeza kuwa operesheni hiyo yaa usalama ni pamoja na kuongeza askari wa doria na vituo vya ukaguzi ili kuimarisha ulinzi na usalama juu ya njia ziendazo Bagdad, kuwasaka watu wenye silaha na kufanya mashambulio ya ndege dhidi ya mahali wanapojificha magaidi.
Vyombo vya habari vinasema, lengo kwanza la operesheni hiyo ni kutuliza mashambulio ya kundi la Al Qaeda baada ya Abu Musab al-Zarqawi, kinara wa kundi hilo nchini Iraq kuuawa. Baada ya Zarqawi kuuawa tarehe 7 mwezi huu na jeshi la Marekani, mashambulio mapya ya kisilaha yaliitingisha Iraq, hususan mji wa Bagdad. Takwimu zilizotolewa na wizara ya ulinzi ya Iraq tarehe 13 may zilionyesha kuwa, katika siku 7 zilizopita, jeshi la muungano nchini Iraq lilishambuliwa mara 52, ambapo jeshi la usalama la Iraq lilishambuliwa mara 67 na raia wa Iraq 263 waliuawa katika mashambulio 63.
La pili, serikali mpya ya Maliki inahitaji hali ya Iraq kuboreshwa ili kupata kuaminiwa na wananchi na kuimarisha msingi wa utawala wake. Baada ya kuasisiwa serikali mpya nchini Iraq, mapambano ya madhehebu ya kidini na mashambulio ya kimabavu yaliongezeka kwa mfululizo, mazingira mabaya ya usalama yameathiri vibaya utawala wa serikali mpya, kutishia mchakato wa usuluhisho wa kisiasa kati ya makundi mbalimbali nchini Iraq, ambapo watu wanaoathirika zaidi ni wananchi wa kawaida. Waziri wa ulinzi wa Iraq Bw. Abedel Qader Mohammed Jassim alisema, asilimia 80 ya mashambulio ya kigaidi na vitendo vinavyokiuka sheria vilitendeka kwa makusudi dhidi ya wananchi wa kawaida, ambapo mashambulio ya kisilaha dhidi ya jeshi la usalama la Iraq na jeshi la muungano nchini Iraq ni kiasi cha 15% na 5%.
Tatu, kutuliza ghasia nchini Iraq pia ni matakwa ya kisiasa ya serikali ya Bush. Vita ya Iraq inaathiri imani ya watu juu ya rais Bush wa Marekani, ambapo uungaji mkono wa watu wa Marekani juu yake unapungua kwa mfululizo. Baada ya Zarqawi kuuawa, uungaji mkono juu ya rais Bush uliongezeka kidogo. Bush anataka kupata upya uungaji mkono wa watu wa Marekani kwa kutumia nafasi hiyo. Tarehe 12 mwezi May Bush alisimamia mkutano wa maofisa wa ngazi ya juu huko Camp David kwa ajili ya kujadili hali ya nchini Iraq.
Wachambuzi wanaona, ingawa zoezi hilo ni kubwa, lakini itakuwa vigumu kwa utawala wa Marekani na Iraq kutimiza malengo yao.
Kwanza, mashambulio ya kimabavu ya kundi la Al Qaeda hayataisha kutokana na kifo cha Zarqawi. Kiongozi mpya wa kundi hilo Abu Hamza al-Muhajer alitoa taarifa kwenye tovuti, na kuapa kulipiza kisasi juu ya kifo cha Zarqawi.
Pili, kuongezeka kwa mapambano ya kisilaha nchini Iraq, kunatokana na chanzo cha nchini na nje ya Iraq, na mgongano wa maslahi ya makundi na mgongano wa kimadhehebu ya kidini umesababisha mapambano ya kisilaha nchini Iraq.
Wachambuzi wanasema, licha ya kuchukua hatua za kiusalama, Maliki anajitahidi kuhimiza usuluhisho wa kitaifa, kuhimiza Marekani kuweka mapema ratiba ya kuondoa jeshi lake nchini Iraq, na kuwaacha wairaq kuitawala Iraq, na kuleta utulivu na maendeleo nchini humo.
|