Mkutano wa 6 wa Baraza la wakuu wa nchi wanachama wa Jumuia ya Ushirikiano ya Shanghai umefanyika tarehe 15 huko Shanghai, China. Wakuu wa nchi wanachama na wajumbe waliohudhuria mkutano huo wamejadili mafanikio yaliyopatikana katika maendeleo ya jumuia hiyo tangu ianzishwe miaka mitano iliyopita, wamejadili pia mwelekeo wa maendeleo ya kipindi kijacho na kutunga mpango wa ushirikiano na hatua halisi.
Marais wa nchi wanachama wa jumuia hiyo China, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Russia, Tajikistan na Uzbekistan, wakuu au wajumbe wa nchi wachunguzi za Mongolia ya Nje, Iran, Pakistan na India pamoja na rais wa Afghanistan na wajumbe wa jumuia za kimataifa wamehudhuria mkutano huo.
Rais Hu Jintao wa China ameendesha mazungumzo na kutoa hotuba. Amesifu sana mafanikio yaliyopatikana katika jumuia hiyo katika miaka mitano iliyopita, amesema, siri ya mafanikio kwa jumuia hiyo ni kutokana na kutetea na kutekeleza kihalisi "moyo wa Shanghai" wa kuaminiana, kunufaishana, kuwa na usawa, kufanya mashauriano, kuheshimu ustaarabu wa aina mbalimbali na kutafuta maendeleo ya pamoja. Ili kuijenga sehemu hiyo iwe sehemu ya masikilizano yenye amani ya kudumu na ustawi wa pamoja, rais Hu Jintao ametoa mapendekezo manne akisema:
Tunapaswa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na ujirani mwema, tunapaswa kuzidisha kwa kina ushirikiano wa kufuata halisi halisi ili kusukuma mbele maendeleo ya sekta mbalimbali na kuleta maslahi halisi kwa wananchi wa nchi wanachama mbalimbali.
Rais Hu Jintao amedhihirisha kuwa, nchi wananchama zinapaswa kuendeleza maingiliano kwenye sekta ya utamaduni, kuimarisha msingi wa kijamii, aidha kushikilia ushirikiano wa ufunguaji wa mlango na kulinda amani ya dunia.
Katika hotuba yake, rasi Hu amesisitiza kuwa, China inashikilia njia ya maendeleo ya amani, na maendeleo ya China yataleta kwanza fursa kubwa kwa nchi jirani zake. Alisema:
Dunia inafuatilia maendeleo ya China na kufuatilia njia ya maendeleo ya China katika siku za mbele. Napenda kusisitiza kwa makini hapa kuwa, China itashika bila kutikisika njia ya maendeleo ya amani, kushikilia kutekeleza mikakati ya kunufaishana na kutafuta maendeleo ya pamoja, kushikilia sera ya kidiplomasia ya ujirani mwema na kushirikiana na nchi jiarani katika kutafuta maendeleo kwa pamoja.
Katika mazungumzo kati ya pande mbalimbali, marais wa nchi wanachama , marais wa nchi wachunguzi na wajumbe wa jumuia za kimataifa wametoa hotuba wakitoa mapendekezo halisi kwa ajili ya maendeleo ya Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai.
Rais Putin wa Russia alipotoa hotuba alisisitiza kuwa, uhusiano wa kimkakati na kiwenzi ulio wa usawa umeanzishwa kati ya nchi wananchama wa Jumuia ya Ushirikiano ya Shanghai, uhusiano huo umewekwa kwenye msingi wa mtizamo wa pamoja. Alisema:
Naona jumuia hii imekuwa jumuia ya kimataifa inayopevuka, ambayo inaweza kutatua kwa kujitawala na kujiamulia masuala yanayoikabili sehemu hiyo katika kulinda amani, usalama na maendeleo. Kuthibitisha uhusiano wa kimkakati na kiwenzi ulio wa usawa ni jambo muhimu zaidi katika mchakato wa maendleeo ya jumuia hiii, naona lazima kuthibitisha na kuimarisha uhusiano huo kwa kupitia kusaini makubaliano ya pande nyingi.
Rais Musharaf wa Pakistan ambayo ni nchi mchunguzi wa jumuia hiyo alipotoa hotuba alisema, Pakistan inapenda kufanya ushirikiano barabara na Jumuia ya Ushirikiano ya Shanghai na kutoa mchango wa kiujenzi kwa kutimzia lengo la jumuia hiyo.
|