Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-16 20:41:40    
Waziri mkuu wa China Wen Jiabao kufanya ziara katika nchi saba za Afrika(1)

cri

Tarehe 9 Juni, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bwana He Yafei alifanya mkutano na waandishi wa habari akiwafahamisha hali ya ziara ya waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao katika nchi saba za Afrika atakayofanya kuanzia tarehe 17 hadi 24 Juni, nchi hizo saba ni Misri, Ghana, Congo Brazzaville, Angola, Afrika ya kusini, Tanzania na Uganda.

Bw. He Yafei alisema Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea, lina nchi 53, na idadi ya watu zaidi ya milioni 800. Katika historia nchi nyingi za Afrika ziliwahi kukumbwa na utawala wa kikoloni, na nchi zote za Afrika zilikamilisha jukumu la kujipatia uhuru mwishoni mwa karne iliyopita baada ya mapambano ya muda mrefu. Katika miaka ya karibuni, nchi za Afrika zimeimarisha ushirikiano, kujitahidi kustawisha uchumi, kutatua migogoro ya kikanda barani Afrika, kutunga na kutekeleza mpango wa ushirikiano mpya wa maendeleo ya uchumi barani Afrika, na kupata mafanikio kadha wa kadha katika kulinda utulivu wa kisiasa na kukuza uchumi. Nchi za Afrika zimekuwa nguvu muhimu katika kuleta amani na maendeleo duniani.

Bw. He Yafei alisema urafiki na mawasiliano kati ya watu wa China na nchi za Afrika yamekuwa na historia ndefu. Kuanzia mwaka 1956 tangu China ianzishe uhusiano wa kibalozi kati yake na Misri, uhusiano kati ya China na nchi za Afrika ulifungua ukurasa mpya. Katika miaka 50 iliyopita, China na nchi za Afrika zinasaidiana, kuungana mkono, uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya pande hizo mbili umeimarishwa na kukuzwa mwaka hadi mwaka. Katika miaka ya karibuni, uhusiano kati ya China na Afrika umepata maendeleo mapya, na ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata mafanikio mazuri. Mwaka 1956 thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilikuwa dola za kimarekani milioni 12 tu, na mwaka 2005 thamani hiyo iliongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 39.7. Ilipofika mwaka 2005, uwekezaji wa moja kwa moja wa China katika nchi za Afrika ulifikia dola za kimarekani bilioni 1.12. China imetoa misaada ya aina mbalimbali kwa nchi za Afrika, na kujenga miradi 900 kwa Afrika, reli ya TAZARA imekuwa mnara wa urafiki kati ya China na Afrika.

Zaidi ya hayo ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika katika sekta za elimu, afya, utamaduni pia umepata maendeleo mazuri. Ilipofika mwaka 2005, serikali ya China kwa jumla ilikuwa imetoa misaada ya mafunzo kwa wanafunzi elfu 18 wa nchi 50 za Afrika, na kuwatuma madaktari elfu 16 kufanya kazi katika nchi mbalimbali za Afrika. Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lililoundwa mwaka 2000 limekuwa baraza la kufanya mazungumzo kati ya viongozi wa China na nchi za Afrika na utaratibu mzuri wa kuhimiza ushirikiano, baraza hilo limesukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika.

Bw. He Yafei alisisitiza kuwa China na nchi za Afrika zote ni nchi zinazoendelea, ambazo zina maoni ya pamoja na maslahi ya pamoja katika masuala mengi. Wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Afrika, serikali ya China inatumai kusukuma mbele zaidi uhusiano huo pamoja na nchi za Afrika. Mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China ilitangaza waraka wa sera ya China kwa Afrika, mwezi Aprili mwaka huu, rais Hu Jintao alifanya ziara katika nchi tatu za Afrika. Na safari hii ya waziri mkuu Wen Jiabao katika nchi saba za Afrika itakuwa shughuli nyingine muhimu ya kidiplomasia ya China barani Afrika. Bw. Wen Jiabao atafuata sera ya kuimarisha urafiki, kuzidisha uaminifu, kupanua ushirikiano ili kupata maendeleo kwa pamoja, kufanya majadiliano kwa kina na viongozi wa nchi hizo saba kuhusu njia ya kuimarisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano wa pande mbilimbili, na kupanga mwelekeo wa maendeleo ya siku zijazo.

Bw. He Yafei alisema Misri ni kituo cha kwanza cha ziara hii ya Bw. Wen Jiabao barani Afrika. Misri pia ni nchi kubwa inayoendelea katika sehemu ya mashariki ya kati na Afrika. Tangu China na Misri zianzishe ushirikiano wa kimkakati mwaka 1999, nchi hizo mbili zimepata maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali na kudumisha mawasiliano na usawazishaji kuhusu mambo ya kimataifa. Mwaka huu ni mwaka wa kuadhimisha miaka 50 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, waziri mkuu Wen Jiabao atakutana na rais Mubarak, spika wa bunge, mwenyekiti wa baraza la mashauriano, na waziri mkuu wa nchi hiyo. Viongozi wa nchi hizo mbili watakumbusha mchakato wa maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili katika miaka 50 iliyopita, na kujadiliana namna ya kuzidisha ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili. Pande hizo mbili pia zitasaini makubaliano mengi ya ushirikiano katika sekta za siasa, uchumi na biashara, utamaduni na elimu. Bwana Wen Jiabao na waziri mkuu wa Misri Bwana Nazifu watahduhuria kwa pamoja tamasha kubwa la kuadhimisha miaka 50 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya China na Misri uanzishwe litakalofanyika kwenye sehemu ya piramidi na kutoa hotuba muhimu.(Inaendelea)