Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-16 20:46:57    
Waziri mkuu wa China Wen Jiabao kufanya ziara katika nchi saba za Afrika(2)

cri

(Inaendelea)

Kuhusu ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao nchini Ghana, Bw. He Yafei alisema, Ghana ni moja ya nchi za Afrika zilizo kusini mwa Sahara zilizoanzisha mapema uhusiano wa kibalozi na China, watu wa nchi hizo mbili wana urafiki mkubwa wa jadi. Katika miaka 46 iliyopita tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, ushirikiano kati ya Chian na Ghana katika sekta mbalimbali umeimarishwa siku hadi siku, nchi hizo mbili zinaungana mkono katika mambo ya kimataifa, zimepanua ushirikiano katika sekta za ujenzi wa miundombinu, mawasiliano ya simu, na nguvukazi. Atakapokuwa nchini Ghana, Bw. Wen Jiabao atabadilishana maoni kwa kina na rais Kufur kuhusu kuzidisha urafiki wa jadi, kupanua ushirikiano wa kunufaishana na mambo mengine yanayozihusu pande zote mbili, na kuhudhuria uzinduzi wa mradi wa ukarabati wa barabara uliosaidiwa na serikali ya China. Nchi hizo mbili pia zitasaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara, elimu na afya.

Alipotaja ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao atakayofanya nchini Kongo Brazaville, Bw. He yafei alisema, China na Kongo Brazaville zilianzisha uhusiano wa kibalozi mwaka 1964, uhusiano huo unaendelea vizuri. Rais Denis Sassuo Ngwesu wa Kongo Brazaville ni mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, ametoa mchango mkubwa katika mambo ya nchi za Afrika. Atakapokuwa nchini Kongo Brazaville, waziri mkuu Wen Jiabao atafanya mazungumzo na rais Sassuo na waziri mkuu Mwuba, na kutembelea hospitali wanakofanya kazi madaktari wa China na shule ya sekondari inayofundisha lugha ya Kichina. Pande hizo mbili pia zitasaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali za uchumi,elimu na kilimo.

Kuhusu ziara atakayofanya waziri mkuu Wen Jiabao nchini Angola, Bw. He Yafei alifahamisha kuwa, Angola ni moja ya nchi muhimu barani Afrika. Wakati watu wa Angola walipopigania uhuru, watu wa China waliwaunga mkono kihali na kimali, na wameanzisha urafiki mkubwa. Tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1983, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umepata maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali, ambapo maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili umeimarishwa mwaka hadi mwaka. Atakapokuwa nchini Angola, Bw. Wen Jiabao atabadilishana maoni na rais Dos Santos kuhusu kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali na masuala yanayozihusu pande zote mbili. Nchi hizo mbili pia zitasaini makubaliano ya ushirikaino katika sekta za uchumi, biashara, kilimo, afya na sheria.

Alipotaja ziara ya Bw. Wen Jiabao nchini Afrika ya kusini, Bw. He Yafei alisema, China na Afrika ya kusini zote ni nchi zinazoendelea. Serikali ya China na watu wake waliunga mkono kwa muda mrefu mapambano ya watu wa Afrika ya kusini dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, na kuunda urafiki mkubwa. Baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Afrika ya kusini mwaka 1998, uhusiano wa pande hizo mbili umeendelea kwa haraka, uaminifu wa kisiasa umeimarishwa, nchi hizo mbili zimethibitisha uhusiano wa kimkakati na kiwenzi wa kuwa na usawa na kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja. Atakapokuwa nchini Afrika ya kusini, waziri mkuu Wen Jiabao atabadilishana maoni na rais Thabo Mbeki kuhusu kuzidisha ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Afrika ya kusini, pia atakutana na makamu wa rais na spika wa bunge wa nchi hiyo pamoja na ofisa mkuu mtendaji wa sekretarieti ya mpango mpya wa kirafiki wa maendeleo ya Afrika. Pia atahudhuria mkutano wa baraza la ushirikiano wa biashara kati ya China na Afrika ya kusini, na kutoa hotuba muhimu kuhusu uhusiano kati ya China na Afrika ya kusini, uhusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika.

Alipozungumzia ziara ya Bwana Wen Jiabao atakayofanya nchini Tanzania, Bw. He yafei alisema, urafiki wa jadi kati ya China na Tanzania una msingi mzuri. Katika miaka 42 iliyopita tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, zinaungana mkono na kufanya ushirikiano kwa udhati. Viongozi wa ngazi ya juu wa nchi hizo mbili wanatembeleana mara kwa mara, na kupata maendeleo mazuri katika ushirikiano wa sekta za uchumi na biashara, elimu na utamaduni na afya. Atakapokuwa nchini Tanzania, Bw. Wen Jiabao na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania maendeleo yaliyopatikana katika uhusiano wa China na Tanzania watakumbusha katika miaka 42 iliyopita, na kubadilishana maoni kuhusu kuzidisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili. Bw. Wen Jiabao pia atakutana na waziri mkuu wa Tanzania Bwana Edward Lowassa. Aidha atakwenda kutoa heshima kwenye makaburi ya wataalamu na wafanyakazi wa China waliokufa katika ujenzi wa reli ya TAZARA, na kutembelea mahali pa ujenzi wa uwanja mpya wa taifa wa Tanzania unaojengwa kwa msaada wa serikali ya China. Pande hizo mbili pia zitasaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta za uchumi na biashara, kilimo, elimu na afya.

Alipotaja ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao atakayofanya nchini Uganda, Bw. He Yafei alisema, uhusiano kati ya China na Uganda unaendelea vizuri katika miaka 44 iliyopita, pande hizo mbili zilikuwa zimefanya ushirikiano mzuri katika sekta za siasa, uchumi, utamaduni, elimu na afya. Viongozi wa ngazi ya juu wa nchi hizo mbili wanawasiliana mara kwa mara. Atakapokuwa nchini Uganda, Bw. Wen Jiabao atafanya mazungumzo na rais Yoweri Museveni wa Uganda, kukutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Bwana Nsibambi, na kubadilishana maoni yao kuhusu kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Pia atashiriki kwenye shughuli za tamasha la watu wa China na Uganda, na kutembelea kituo cha kinga na tiba ya ugonjwa wa Ukimwi cha Uganda. Pande hizo mbili pia zitasaini nyaraka za ushirikiano kuhusu sekta za uchumi na biashara, kilimo, elimu na afya.

Bw. He Yafei alisema kutokana na juhudi za pamoja za pande mbalimbali husika, ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao kwenye nchi hizo saba za Afrika bila shaka itapata mafanikio mazuri, na kuchangia zaidi maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika.