Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-16 20:56:26    
Hamas yatoa ishara ya kusimamisha mapambano na Israel kwa masharti

cri

Tarehe 15 msemaji wa Hamas alisema kwamba Hamas inakubali kusimamisha mapambano na Israel kwa masharti. Wachambuzi wanaona kwamba hatua hiyo ya Hamas inasaidia kupunguza wasiwasi kati ya nchi hizo mbili, lakini pia ni vigumu kusema hali itakuwaje.

Tarehe 9 Aprili Israel ilirusha mabomu kwenye sehemu ya Gaza na kusababisha vifo vya raia kadhaa wa kawaida, kisha makundi yenye silaha ya Hamas yakatangaza kuwa hayataheshimu makubaliano ya kusimamisha mapigano na Israel na yakarusha makombora kwenye sehemu ya kusini ya Israel. Kadhalika, Israel pia ilitangaza "kumaliza uvumilivu" na kuitishia Palestina kufanya mashambulizi makali.

Tokea hapo, mapambano yaliyosimamishwa kwa miezi 17 yameingia hatarini. Tarehe 14 vyombo vya habari vya Israel vilisema kwamba kiongozi wa Hamas ambaye pia ni waziri mkuu wa serikali ya mpito Bw. Ismail Haniyeh siku hizi alifanya mazungumzo na viongozi wa makundi ya Hamas akijaribu kuwashawishi wasimamishe mapambano dhidi ya Israel. Ingawa Hamas ilikataa kwa mdomo lakini kwa vitendo imesimamisha mapambano yake. Msemaji wa Hamas Bw. Ghazi Hamad alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Israel alisema, Hamas inakubali kurudisha makubaliano ya kusimamisha mapambano na kuyashawishi makundi yake kuacha kurusha makombora nchini Israel, lakini Israel sharti isimamishe vitendo vyake vya kuivamia Palestina.

Vyombo vya habari vinaona kuwa, siku hizi Hamas kwa mara nyingi ilitoa ishara ya kutaka kupoza joto la mapambano kwa sababu mbili: Moja ni kukwepa hasara inayoweza kusababishwa na shinikizo kubwa ya Israel kwa serikali ya Hamas ambayo bado haijakuwa imara. Habari kutoka Palestina na Israel zinasema jeshi la Israel na idara ya usalama ya Israel imetoa onyo kuwa, ikiwa Hamas itaendelea kuishambulia Israel, viongozi wa Hamasi watakuwa shabaha ya kupigwa. Baada ya kupima faida na hasara, Hamas inaona ingawa hivi karibuni Israel mara kwa mara ilirusha makombora na kuwaua raia wa kawaida wa Palestina na kusabisha hasira kubwa dhidi ya Israel, hali ambayo inasaidia Hamasi kulipa kisasi na kuumba sura nzuri ya "kupinga wavamizi", lakini kwa upande mwingine, mashambulizi ya Israel yataleta hatari kubwa ambayo mapambano yataongezeka, na Palestina na Israel zitaingia katika mzunguko mbaya wa kulipizana kisasi, na kuhatarisha serikali mpya ya Hamas.

Sababu nyingine ni kuwa, hivi sasa mashindano ya kisiasa kati ya Hamas na Fatah yamekuwa katika kipindi muhimu. Ili kusuluhisha tofauti ya kisiasa kati ya pande mbili, jioni ya tarehe 14 wajumbe wa Hamas na Fatah walifanya mazungumzo huko Gaza na kujadili pendekezo la Misri la kuunda "serikali ya wataalamu" ambayo mtu mmoja huru awe waziri mkuu badala ya serikali ya sasa ya Hamas, lakini Hamas ina haki ya "kusimamia" serikali hiyo ya wataalamu", na kwa mujibu wa pendekezo hilo, Fatah itarudisha mazungumzo yake na Israel, lakini makubaliano yoyote yatakayopatikana katika mazungumzo lazima yaamuliwe kwa kura za maoni za wananchi. Habari kutoka kwa maofisa wa Palestina zinasema kwamba pendekezo hilo linawavutia viongozi wa Fatah na Hamas.

Wachambuzi wanafafanua kwamba ingawa Hamas kwa mara nyingi imetoa ishara ya kutaka kusimamisha mapambano, lakini "mara nyingi mambo hayaendi kama jumuyia au viongozi fulani wanavyotarajia".