Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-19 19:23:32    
Tutajenga nchi zetu kwa elimu tuliyopata nchini China

cri

Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao anafanya ziara rasmi ya kirafiki katika nchi za Afrika zikiwemo Misri, Tanzania, Uganda na Afrika ya Kusini tokea tarehe 17 hadi 24 mwezi Juni. Kabla ya ziara ya waziri mkuu Wen Jiabao, mwandishi wetu wa habari alitembelea vyuo vikuu kadhaa vya Beijing na kufanya mahojiano na baadhi ya wanafunzi wa nchi za Afrika, wanafunzi hao walisema, serikali ya China inazingatia sana uhusiano na Afrika na hilo ni jambo linalowahamasisha, wanatarajia kujenga nchi zao kwa kutumia elimu waliyopata nchini China.

Takwimu iliyotolewa na wizara ya elimu ya China mwishoni mwa mwaka 2005, inaonesha kuwa katika miaka 50 iliyopita, serikali ya China iliwagharimia masomo wanafunzi elfu 17 na 800 wa nchi za Afrika nchini China. Katika vyuo vikuu vingi vya China, ni rahisi sana kwa watu kukutana na wanafunzi wa nchi za Afrika. Katika chuo kikuu cha lugha cha Beijing, tulikuta kundi moja la wanafunzi waliotoka nchi za Afrika. Mmoja kati yao ni Bw. Kadila, ambaye alifika nchini China mwezi Septemba mwaka uliopita, hivi sasa anasoma lugha ya kichina, na anatarajia kuchukua shahada ya udaktari ya uhandisi . Alituambia kwa kichina kuwa;

"Hapo zamani, nchini Uganda walikuweko wachina wachache sana. Lakini hivi sasa wamekuwa wengi. Naona uhusiano kati ya China na Uganda umekuwa mkubwa mwaka hadi mwaka."

Hivi sasa China ina miradi mingi ya ujenzi ambayo ni ya misaada nchini Uganda. Miradi hiyo inaboresha maisha ya watu wa Uganda, mradi unaoukumbuka sana Bw. Kadila mradi wa ujenzi wa uwanja wa taifa wa Mandela. Huo ni mradi mkubwa kabisa kwa hivi sasa nchini Uganda, baada ya kukamilishwa ujenzi wake, uwanja huo utakuwa na zana za kisasa kabisa. Ingawa China siyo nchi inayoongoza duniani katika eneo la usimamizi wa uhandisi, lakini Bw. Kadila alichagua kusoma nchini China. Alisema,

"Kila nchi inaweza kuongoza katika upande fulani katika eneo la teknolojia ya uhandisi, ina umaalumu wake. Lakini ninavyoona mimi, China ni nchi yenye kasi kubwa kabisa ya maendeleo duniani, nchini China kuna miradi mingi, ambayo ujenzi wake unaendelea hivi sasa. Miradi mingi inayoendelea hivi sasa nchini China inalingana na ile ya Uganda, ninaweza kushuhudia ujenzi wa miradi hiyo, ambao utanisaidia sana baadaye. Hivyo nilichagua kusomea uhandisi nchini China."

Katika chuo kikuu cha Beijing, nilimwona mwanafunzi anayetoka nchini Tanzania Bw. Anthony Monge. Hivi sasa anachukua shahada ya pili katika kozi ya idadi ya watu katika chuo kikuu cha Beijing. Alisema, sababu ya kuchagua masomo hayo kwake ni kwamba uzoefu wa China katika upande huo utaweza kuisaidia Tanzania.

"Hivi sasa nchi za Afrika zinahitaji wataalamu wa sekta hiyo. Ingawa suala la idadi ya watu siyo lenye tatizo kubwa kama la China, lakini inekabiliwa na baadhi ya matatizo. Katika miaka 20 ijayo, idadi ya watu nchini Tanzania itaongezeka kwa haraka. Serikali inatakiwa kuchukua hatua tokea sasa hivi, hatua ambayo itanufaisha maendeleo ya nchi.

Ingawa elimu anayojifunza Bw. Antony hivi sasa ni kuhusu idadi ya watu, lakini moyoni mwake anataka sana kujifunza zaidi elimu ya habari. Alisema, watu wa bara la Afrika hawafahamu vizuri China, tena hawana njia nyingi za kuifahamu nchi hiyo. Mambo waliyoona na kusikia nyakati nyingi zaidi ni yale yaliyoelezwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi. Kusikia siyo kuona, hali halisi ya China siyo kama inavyoelezwa na vyombo vya habari vya nchi za magharibi. Kwa hiyo anataka sana kufanya kazi ya uandishi wa habari, na kuwaeleza watu wa Tanzania hali halisi ya China.

"Nilipoambiwa kuwa nitapata mafunzo nchini China, jamaa na marafiki zangu walisikitika sana. Kwani waliona kuwa hali ya China ni yenye vurugu na ghasia nyingi, tena hakuna haki za binadamu. Baada ya kufika China, naona hali ya China ni nzuri sana, na ni salama kabisa."

Aliongeza, "hivi sasa kampuni nyingi za China zimekwenda kuwekeza katika bara la Afrika, na kukaribishwa na watu wa huko. Shughuli za biashara kati ya wachina na waafrika zinafanyika kwa usawa na za kunufaishana. Sisi tunaihitaji China, na China pia inatuhitaji sisi. Tuwe na ushirikiano na kuwa ndugu wazuri na kuijenga dunia kuwa nzuri zaidi!"