Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-20 15:30:03    
China itajenga kituo cha umeme cha nyukilia sehemu ya kaskazini mashariki

cri

Ujenzi wa kipindi cha kwanza wa mradi wa uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia kwenye mto Hongyan, mkoani Liaoning, umeidhinishwa na kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa, hatua ambayo inaonesha kuwa China itajenga kituo cha uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia kwa mara ya kwanza sehemu ya kaskazini mashariki.

Naibu mkuu wa mkoa wa Liaoning Bw. Li Wancai alisema, mradi wa uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia ulioko mkoani Liaoning, ni hatua halisi inayochukuliwa na serikali ya kustawisha kituo cha viwanda cha zamani cha kaskazini mashariki.

Habari zinasema, ujenzi wa mradi huo wa uzalishaji umeme unagawanyika katika vipindi viwili, ambapo mitambo 2 yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kilowati milioni 1 kila mmoja itawekwa kwa uzalishaji umeme. Mpango wa ujenzi wa kipindi cha kwanza, ambao utagharimu Yuan bilioni 23, utakamilika mwaka 2011. Ofisa mmoja wa serikali ya mkoa wa Liaoning alisema, ni nadra kuona mitambo ya uzalishaji umeme yenye uwezo wa kuzalisha umeme kilowati milioni 1 iliwekwa katika vituo vya uzalishaji umeme vilivyoko nchini China hivi sasa.

Idara husika ilianza kufanya maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho cha uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia tokea mwaka 1978, mradi ambao umezinduliwa rasmi baada ya kupita miaka karibu 20. mradi huo umewekezwa na kampuni 4, ambazo kampuni ya uwekezaji wa umeme ya China na kampuni ya uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia ya Guangdong za China zinamiliki zaidi ya 50 ya hisa za mradi huo wa umeme, kampuni ya uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia ya Liaoning ilianzishwa mwanzoni mwa mwaka 2005, na inashughulikia ujenzi na uendeshaji wa mradi huo wa umeme.

Kituo cha uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia cha mto Hongyan, mkoani Liaoning, kiko katika mji wa Wafangdian, sehemu ya kusini mwa penisula ya Liaodong, kituo hicho chenye eneo la hekta 380, kiko karibu na bahari ya Bo. Hivi sasa maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho yanaendelea vizuri, na ujenzi wa mradi huo umewekwa katika mpango wa 11 wa maendeleo ya miaka 5.

Meneja mkuu wa kampuni ya uwekezaji wa umeme ya China, Bw. Wang Binghua alisema, kituo cha uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia cha Liaoning ni cha kwanza kwa ukubwa cha kampuni hiyo katika uwekezaji mkoani Liaoning, washirika wa kampuni hiyo wamesema, watajitahidi kadiri wawezavyo kukamilisha ujenzi wa mradi huo.

Mfanyakazi mmoja wa kampuni hiyo alisema, kituo cha uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia cha mto Hongyan, kitafuata kwa makini kanuni za usalama na hifadhi ya mazingira, licha ya kuhakikisha kwamba kituo hicho kinahakikisha usalama wa ujenzi na uendeshaji wa shughuli za uzalishaji umeme, kituo hicho kinawafahamisha wakazi walio karibu na kituo cha umeme kuhusu usalama wa uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia. Alisema, kituo cha uzalishaji umeme cha mto Hongyan kitatumia teknolojia ya kupata maji baridi kwa kutumia maji ya baharini ili kudhibiti matumizi ya maji baridi, licha ya maji baridi yaliyochujwa kutokana na maji ya baharini kutumika katika kituo cha uzalishaji umeme, ziada ya maji hayo itatolewa kwa wakazi walio karibu na kituo hicho cha umeme.

Tokea miaka ya 80 ya karne iliyopita, China imejenga vituo vinne vya uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia. Kanuni zinazofuatwa na China katika kuendeleza uzalishaji umeme kwa nguvu za nyukilia ni kujitegemea na kuwa na ushirikiano na nchi za nje. Habari zinasema, mitambo itakayotumika katika kituo cha umeme cha mto Hongyan, ilisanifiwa na kutengenezwa na China yenyewe.

Pamoja na kuimarika kwa haraka kwa nguvu za uchumi wa China, China inahitaji umeme kwa wingi. Uzalishaji wa umeme kwa nguvu za nyukilia utawekwa kipaumbele katika siku za baadaye katika ujenzi wa uzalishaji wa umeme nchini China.

Idhaa ya kiswahili 2006-06-20