Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-20 18:49:34    
Kundi la madakatari wa China wanatoa msaada barani Afrika

cri

Bibi Chen Shuming ni dakatari wa China, hivi sasa yeye ni mmoja wa madakatari wa China wanaotoa huduma katika nchi za nje, hivi sasa anafanya kazi katika hospitali moja nchini Zimbabwe, kusini mwa Afrika. Katika kipindi hiki cha leo, nitawaletea habari kuhus kazi na maisha ya madakatari wanaotoa msaada wa huduma nchini Zimbabwe.

Kikundi cha madakatari wa China nchini Zimbabwe kina madakatari 9, ambao 6 kati yao wanafanyakazi katika mji mkuu wa Harare, na wengine watatu wanafanya kazi mjini Bulawayo, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe. Kila mmoja wa madakatari hao anafanya kazi katika hospitali kadhaa kwa nyakati mbalimbali.

Bibi Chen Shuming alisema, nchini China madakatari wanaotaka kushiriki katika kundi la madakatari wanaotoa huduma katika nchi za nje, wanapaswa kufaulu mitihani mbalimbali kabla ya kupelekwa kutoa huduma ya tiba katika nchi za nje.

"Dakatari anayeshiriki utoaji huduma za tiba katika nchi za nje, kwanza anapaswa kupendekezwa na kiongozi wa hospitali, halafu anapaswa kufaulu katika mitihani mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya kuandika, kujibu maswali ana kwa ana na kutibu mgonjwa."

Madakatari wanaopelekwa katika nchi za nje, kwa kawaida wanafanya kazi kuishi katika mazingira mazuri nchini China, tena ni madakatari waliokwisha pata mafanikio fulani katika idara yao. Kwa mfano, bibi Chen Shuming alipofanya kazi nchini China, alikuwa mkurugenzi wa idara ya upusuaji(anaesthetic) ya hospitali ya wilaya Dongan, mji wa Yongzhou, kusini mwa mkoa wa Hunan. Bibi Chen anafanya kazi nyingi nchini Zimbabwe, lakini mazingira ya maisha na pato lake yanalingana na yale aliyokuwa nayo nchini China. Madakatari hao hawakulalamika. Alipozungumzia suala hilo, bibi Chen alieleza lengo la madakatari wanaofanya kazi katika nchi za nje.

"Sisi hatuna matatizo ya kimawazo, kwa kuwa tulifika hapa kwa lengo la namna moja la kutoa msaada katika nchi ya nje. Kwanza, ni kuimarisha urafiki kati ya nchi zetu mbili, pili ni kutoa mchango wetu kwa ajili ya afya ya watu wa nchi hiyo."

China ilianza kutoa misaada ya tiba katika nchi za Afrika mnamo mwaka 1963. katika miaka zaidi ya 40 iliyopita, China ilipaleka madakatari zaidi ya elfu 15 na 800 kwa nchi 47 za Afrika, na kuwatibu wagonjwa zaidi ya milioni 170. Madakatari wa China wakishirikiana na madakatari wa huko, waliokoa maisha ya wagonjwa wengi mahututi. Mbali na hayo, walipeleka madawa ya jadi ya kichina, akyupancha, massage na tiba ya uunganishaji wa tiba za kichina na za nchi za magharibi katika nchi za nje.

Aidha, madakatari wa China waliwafundisha madakatari wenzao wa nchi za nje uzoefu wao kwa njia za kufanya upasuaji kwa pamoja, kutoa mihadhara na semina. Hadi hivi leo, madakatari wa China wametoa mafunzo kwa madakatari na wauguzi wa ngazi za chini na kati wa nchi za nje wapatao 3,000 kwa jumla, na kuwafundisha madakatari na wauguzi elfu makumi kadhaa kwa njia ya kufanya kazi nao kwa pamoja.

Madakatari wa China wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa magonjwa kutokana na kwamba kila siku wako karibu sana na wagonjwa. Nchini Zimbabwe kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa ukimwi, lakini madakatari wanaweka mbele kazi za kuokoa maisha ya wagonjwa. Bibi Chen Shuming alisema, "siku moja nilifanya upasuaji na kutoa mtoto mchanga kutoka tumbani mwa mama yake, mtoto huyu alishindwa kupumua na moyo wake uliacha kudunda, ili kuokoa maisha ya mtoto mchanga, niliingiza hewa mdomoni mwake kwa kutumia kinywa changu, nilifanikiwa, mtoto alianza kupumua yeye mwenyewe na moyo wake ukaanza kudunda-dunda."

Serikali za nchi nyingi zilipongeza kazi za madakatari wa China walioko nchini mwao, na ziliwapa medali au hati za sifa. Watu wa nchi nyingi za Afrika wanapenda madakatari wa china na kuwaita "malaika wanaovalia mavazi meupe".