Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao ambaye yuko ziarani nchini Ghana pamoja na rais John Kufuor wa nchi hiyo tarehe 19 juni huko Accra walihudhuria kwa pamoja sherehe ya kuzinduliwa kwa mradi wa ukarabati wa barabara nchini humo unaofadhiliwa na serikali ya China.
Barabara hiyo ni moja ya barabara kuu nchini Ghana inayotoka kusini hadi kaskazini mwa nchi hiyo, ambayo inaunganisha mji mkuu Accra na mji mkubwa wa pili wa kaskazini Kumasi, na ina umuhimu mkubwa kiuchumi. Kwenye hafla ya uzinduzi wa barabara hiyo, waziri mkuu wa China alisema:
Barabara hiyo ni alama nyingine ya urafiki na ushirikiano kati ya China na Ghana, na vilevile ni barabara hiyo mpya inazidisha urafiki wa jadi kati ya China na Ghana.
Ujenzi wa Mradi wa ukarabati na upanuzi wa barabara toka Accra hadi Kumasi ulianzia mwezi Mei mwaka 2004, serikali ya China imetoa mikopo wa yuan milioni 180 bila riba ili kufanikisha mradi huo.. Kampuni kuu ya miradi ya reli ya China iliyobeba jukumu la ujenzi wa barabara hiyo ilituma mafundi na wasimamizi hodari, kununua zana na vifaa vyenye sifa bora na kuandaa mpango kabambe wa ujenzi. Katika ujenzi wa miaka miwili, mafundi wa China na Ghana walishinda taabu na kushirikiana barabara, wakajenga barabara hiyo pana kwa akili zao na kutokwa jasho jingi. Mkuu wa kundi la mafundi wa China Bwana He Chengmao alisema:
Barabara hiyo ina urefu wa kilomita 17.424, kwenye barabara kuna njia 4 za kupita kwa magari, kutokana na usanifu, muda wa matumizi yake ni miaka 15, na mwendo wa uendeshaji wa magari ni kilomita 100 kwa saa.
Ofisa wa serikali ya Jimbo la Accra Bibi Theresa Tagoe alisifu sana kazi nzuri iliyofanya kamapuni ya China, alisema:
Zamani kwenye barabara hilo kuna msongamano siku zote, hasa jumamosi na jumapili, waendeshaji magari walikuwa wakitaka kupita barabara hilo walipaswa kutumia saa 3 hadi 4. Ukarabati na upanuzi wa barabara hilo umetusaidia kutatua tatizo kubwa.
Barabara hiyo jipya iliyojengwa kwa msaada wa China si kama tu imepunguza muda wa kupita magari kati ya Accra na Kumasi na kuiwezesha safari iwe ya usalama na raha zaidi, bali pia itaboresha na kuhimiza ongezeko la biashara na uuzaji wa nyumba kwenye sehemu iliyoko karibu na barabara hio. Rais Kufuor wa Ghana alisema:
Kwa kupitia ujenzi wa mradi huo, tumeona ufanisi mkubwa wa kazi na sifa bora ya ujenzi wa miradi waliyoonesha mafunzi wa China, hivyo tuna matumaini kuwa wataendelea kubaki nchini mwetu kutusaidia kukamilisha miradi mingine ya ukarabati wa njia nyingine.
Mradi wa ukarabati na upanuzi wa barabara la kutoka Accra hadi Kumasi ni moja kati ya miradi inayojengwa kwa msaada wa China nchini Ghana. Waziri mkuu Wen Jiabao alisema, katika miaka mingi iliyopita, China na Ghana zimeanzisha ushirikaino mzuri wenye mafanikio katika sekta za siasa, uchumi na biashara, afya, utamaduni na elimu.
Serikali ya China imetoa msaada wa kidhati na kirafiki kwa Ghana kadiri kwa iwezekanavyo, miradi mbalimbali inayojengwa kwa msaada wa China nchini Ghana imezidisha maelewano na urafiki kati ya wananchi wa China na Ghana, pia imechangia maendeleo ya uchumi na jamii ya Ghana.
Katika miaka 50 iliyopita, miradi ya kiuchumi na kijamii iliyojengwa kwa msaada wa China barani Afrika ilifikia karibu 900. Serikali ya China ilipotoa mikopo bila riba au kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa nchi za Afrika, pia iliyahamasisha makampuni ya China yenye nguvu na sifa bora kwenda kuwekeza barani Afrika na kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia wa aina mbalimbali. Barabara la kutoka Accra hadi Kumasi nchini Ghana ni mfano mmojawapo.
|