Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-21 19:31:43    
Waziri mkuu wa China atembelea shule ya sekondari ya Congo Brazaville

cri

Waziri mkuu wa China Bwana Wen Jiabao alitembelea shule ya sekondari ya Brazaville tarehe 20 juni asubuhi kwa saa za huko. Shule hiyo inajulikana sana nchini Congo Brazavil kutokana na masomo yake ya lugha ya kichina. Ziara ya Waziri mkuu Wen Jiabao iliwafurahisha wanafunzi wa shule hiyo.

Asubuhi ya siku hiyo, vifijo na vigelele vilisikika katika sehemu iliko shule ya Sekondari ya Brazaville.

Walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Brazaville pamoja na wakazi wa sehemu iliyo karibu na shule hiyo waliimba nyimbo na kucheza ngoma kwa furaha kumkaribisha waziri mkuu Wen Jiabao na ujumbe wa serikali ya China. Shule ya sekondari ya Brazaville ni shule kubwa zaidi kuliko nyingine nchini Congo Brazaville, shule hiyo ya sekondari ina wanafunzi zaidi ya 4000. Kuanzia mwaka 1990, walimu wa shule hiyo walianzisha somo la lugha ya kichina kwenye madarasa ya sekondari ya juu, hivi sasa wanafunzi 158 wanajifunza lugha ya kichina. Waziri mkuu Wen Jiabao akiambatana na walimu wa shule hiyo alifika katika darasa kwanza la kidato cha tatu, ambapo katika ubao wa darasani aliona maneno yaliyoandikwa kwa lugha ya kichina: Sisi ni daraja la urafiki kati ya Jamhuri ya Congo na China. Wanafunzi wote wa darasa hilo waliongea kwa kichina kuwakaribisha wageni kutoka China.

Walisema, tunafurahia sana ziara ya waziri mkuu wa China, walimu wetu wametuambia kuwa, China ni nchi yenye historia ndefu na utamaduni unaong'ara. Leo umetutembelea na kutuletea urafiki wa wananchi wa China kwa wananchi wa Congo Brazaville.

Ingawa matamshi ya kichina ya wanafunzi hao bado siyo sanifu sana, lakini sura za watoto hao zimeonesha hisia za dhati. Waziri mkuu Wen Jiabao alitiwa moyo kweli alipokutana na wanafunzi hao wa barani Afrika wanaojifunza kichina na walimu wao ambao wameshughulikia mafunzo ya lugha ya kichina kwa miaka mingi, aliwaambia kwa dhati:

Ni matumaini yangu kuwa mtaweza kujifunza vizuri kichina na kutembelea nchini China.

Wanafunzi wa darasa la pili la kidato cha tatu cha sekondari ya juu walimwonyesha waziri mkuu madaftari yao ya masomo, waziri mkuu Wen Jiabao alimfuata mwanafunzi mmoja akachukua daftari lake na akasoma sentensi moja ya kichina aliyoandika mwanafunzi huyo:

"Alicheza vizuri mpira wa meza. Jana nilishiriki mashindano ya soka shuleni", kumbe wewe unaandika kichina vizuri, hakuna kosa hata kidogo.

Baadaye Bwana Wen Jiabao alichukua chaki akaandika maneno maarufu yaliyoandikwa na mshairi Wang Bo wa Enzi ya Tang ya kale ya China yasemayo: Marafiki wapo popote duniani, nchi zote zilizoko mbali ni kama majirani. Waziri mkuu Wen alisema:

Maneno hayo yameonesha kuwa ingawa China na Afrika ziko mbali sana, lakini bado kama ni majirani.

Waziri mkuu Wen Jiabao alipoondoka darasani, walimu na wanafunzi wa shule hiyo ya sekondari wapatao elfu kadhaa walipiga saluti kumsalimia wakisema kwa kichina: Ni Hao, Ni Hao. Hujambo, Hujambo.

Ingawa ziara yake hiyo katika shue hiyo ya sekondari ni ya muda mfupi, lakini waziri mkuu Wen Jiabao na ujumbe wa China walijionea uchangamfu na urafiki wa wananchi wa Congo Brazaville kwa wananchi wa China, kweli umbali wa kijioglafia hauwezekani kuzuia urafiki kati ya nchi hizo mbili.