Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-21 19:17:33    
Hospitali ya Talangai ni uthibitisho wa urafiki kati ya China na Jamhuri ya Congo Brazaville

cri

Waziri mkuu wa serikali ya China Bw. Wen Jiabao asubuhi ya tarehe 20 mwezi Juni alikwenda kuwaangalia madaktari wa kichina wanaofanya kazi katika Hospitali ya Talangai, iliyopo Brazaville ambao ni mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, ambapo alikuwa na mazungumzo na mkuu wa hospitali hiyo bibi Dimi Elisa. Walipozungumzia ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika eneo la utibabu na mambo ya afya, pande hizo mbili zote zilisema hospitali ya Talangai ni uthibitisho wa urafiki kati ya watu wa China na Jamhuri ya Congo Brazaville.

Hospitali ya Talangai ilikuwa hospitali moja kwa ajili ya akina mama katika miaka ya 60 ya karne iliyopita, ambayo ilifanyiwa ukarabati na kukuzwa kuwa hospitali yenye idara mbalimbali za tiba kutokana na msaada wa China, na sasa inachukua nafasi ya 3 kwa ukubwa mjini Blazaville. Hivi sasa hospitali hiyo ina idara 13, na ilihudumia wagonjwa karibu elfu 58 mwaka uliopita; hadi hivi sasa, watoto kiasi cha elfu 10 wameshazaliwa katika hospitali hiyo. Mkuu wa hospitali bibi Dimi Elisa alimweleza waziri mkuu Wen Jiabao akisema,

"Hivi sasa hospitali yetu ina vitanda 226 kwa wagonjwa, na madakatari 38, hospitali hiyo ni uthibitisho wa ushirikiano kati ya China na Jamhuri ya Congo Brazaville. Toka mwaka 1970, China inaleta madakatari katika hospitali hii, na wako madakatari wa China karibu katika kila idara ya hospitali."

China kupeleka vikundi vya madakatari kwa nchi za Afrika ni mradi unaotekelezwa kwa miaka mingi katika nchi nyingi za Afrika. Katika miaka 43 iliyopita, China imepeleka madaktari kiasi cha elfu 16 kwa nchi 47 za Afrika, ambao waliwatibu wagonjwa wa huko karibu milioni 240. Madakatari wa China wanafanya kazi bega kwa bega na madaktari wa Afrika, licha ya kuwatibu wa gonjwa wa huko, wanawafundisha madakatari wa huko madawa na tiba ya jadi ya kichina, na wameshatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa huduma ya tiba wa ngazi ya chini na kati wapatao zaidi ya elfu 10.

Bibi Elisa alisema, hakuna tofauti kati ya madaktari wa China na madaktari wa Congo katika hospitali ya Talangai, madakatari na wagonjwa wa Congo wanawachukulia madakatari wa China kama madaktari wa Congo."

Bibi Zhang Lijuan ni dakatari aliyetoka hospitali ya Nankai iliyopo katika mji wa Tianjin, kaskazini mwa China, alisema, wanaona wagonjwa wa Jamhuri ya Congo wanaheshimu sana madaktari wa China, wanashirikiana vizuri sana na madaktari wa Congo katika hospitali.

"Tunawaelekeza wauguzi wa hospitali hiyo ujuzi wa tiba, sasa wanafahamu mambo mengi. Wanatusaidia sana katika maisha yetu, kwa mfano wanatunza usafi wa vyumba vya hospitali, na kutusaidia wakati tunapopatwa na shida katika maisha yetu."

Ili kuonesha uungaji mkono kwa jitihada ya serikali ya Congo ya kudhibiti ugonjwa wa malaria, waziri mkuu Wen Jiabao aliikabidhi serikali ya Jamhuri ya Congo madawa ya malaria yenye thamani ya Yuan za Renminbi milioni 2 yaliyotolewa na serikali ya China kama msaada, na kuzipa hospitali 2 za Blazavia wanazofanya kazi madaktari wa China vifaa vya tiba. Waziri mkuu Wen Jiabao alisema,

"Hospitali ya Talangai ni thibitisho la urafiki wa watu wa China na Jamhuri ya Congo. Nina tumaini hospitali hiyo itakuwa hospitali ya ushirikiano wa nchi zetu mbili na kutoa huduma ya kiafya kwa watu wa Jamhuri ya Congo."

Waziri mkuu Wen Jiabao alisema, serikali ya China itaendelea kuzisadia nchi za Afrika kujenga na kuboresha hospitali, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa huduma ya utibabu kwa njia ya kupeleka madaktari na kutoa misaada ya kujenga hospitali na vifaa vya tiba, ili kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika udhibiti wa maradhi makubwa ya kuambukiza na mfumo wa kukabiliana na matukio ya dharura kuhusu mambo ya afya ya umma.