Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-21 20:21:29    
Magari yanayotumia nguvu ya betre yakuwa karibu nasi

cri

Endapo unatembelea miji ya China, pengine bas unayopanda, ambayo inaonekana ni ya kawaida, lakini bas hiyo huenda ni bas inayotumia nguvu ya betre, na magari ya aina hiyo yanayotumia nguvu ya betre yanachukuliwa kuwa ni magari ya siku za baadaye. Kutokana na sababu mbalimbali zinazohusika na nishati na hifadhi ya mazingira, hivi sasa magari ya aina mpya yanayotumia nguvu ya betre na kuchangia hifadhi ya mazingira, yanakaribia hatua kwa hatua maisha ya watu.

Hivi karibuni China ilipandisha tena bei ya petroli, hivyo matumizi ya kila mwezi ya watu wenye magari yameongezeka zaidi. Bw. Zhang Rui anayeishi katika mji wa Shenyang, kaskazini mashariki mwa China, ni mmoja kati ya watu wenye magari, alisema,

"Bei ya petroli ilipanda kwa mfululizo katika miezi michache iliyopita, watu wenye magari wanahisi kuwa gharama ya petroli ya kila mwezi imekuwa kubwa katika jumla ya matumizi ya kimaisha. Licha ya hayo, kimazingira, magari yanatumia mafuta mengi ya petroli, inaathiri vibaya mazingira ya asili. Na itakuwa vizuri, kama iko siku moja, magari hayatatumia tena mafuta ya petroli."

Wazo la bwana Zhang si ya ndoto, hali halisi ni kwamba magari yasiyotumia petroli, ambayo yanatumia nguvu za betre sasa yanajisogeza na maisha ya watu. Tangu kufanya utafiti wa magari yanayotumia nguvu za betre katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, hivi sasa aina kadhaa za magari yanayotumia nguvu za betre yaliyosanifiwa na kutengenezwa na China yenyewe yametoka katika maabara, na kutumika rasmi. Habari zinasema, magari yanayotumia nguvu za betre yanaweza kugawanyika katika katika aina tatu: Aina ya kwanza ni magari yanayotumia nguvu za betre yanazobeba; Aina ya pili ni kutumia nishati za aina mbili za petroli na nguvu za betre; na aina ya tatu ni kutumia umeme, ambao unazalishwa kwa hewa ya hydrogen.

Bibi Han Ke kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Beijing, ambaye anashiriki utafiti na utengenezaji wa magari yanayotumia nguvu za bere na umeme, alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa magari yanayotumia nguvu za betre ya chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Beijing, hivi sasa yametumika kwa majaribio kama mabas ya kawaida.

"Mabas hayo yanaonekana kama mabas yanayotumika hivi sasa, isipokuwa yanatumia nguvu ya betre. Btre ya magari ni sawa na betre za simu ya mkono, ambazo zinaweza kuongezwa nguvu moja kwa moja. Gari la aina hiyo linaweza kukimbia kilomita kati ya 150 na 300 hivi baada ya kuongezwa nguvu. Hivi sasa magari hayo yanatumika kama mabas ya kawaida kwenye njia ya mabas ya No 121."

Mwandishi wetu wa habari aliona, magari mapya zaidi ya 10 yamewekwa kwenye stesheni ya mabas ya No. 121. madereva wa magari hayo walisema, magari hayo hayana makelele, na yanakwenda kwa utulivu, abiria hawawezi kusikia harufu ya petroli. Abiria bibi Rong Xiumin alimwambia mwandishi wetu wa habari, kwa kulinganishwa na magari yanayotumia petroli, anapenda kupanda magari hayo yanayotumia nguvu za betre.

Hivi sasa, licha ya wakazi wa Beijing, wakazi wa miji mingine wakiwemo wa miji ya Wuhan, Tianjin na Weihai pia wanaweza kutumia magari hayo yanayotumia nguvu za betre. Magari hayo yanatumika mchana, na yanaongezwa nguvu za betre wakati wa usiku, hivyo yanaweza kutumia ziada ya umeme katika wakati wa usiku, ambapo umeme hautumiki kwa wingi kama mchama. Lakini magari hayo yana dosari moja, ambayo magari yanashindwa kukimbia kwa kasi.

Je, tunaweza kuwa na magari yanayoweza kwenda kwa kasi na kutotegemea kabisamafuta ya petroli? Jibu ni ndiyo. Magari hayo yanamifumo miwili ya nguvu za uendeshaji; mmoja ni injin ya jadi inayotumia mafuta ya petroli, na mwingine ni kutumia nguvu za betre. Wakati magari yanapokwenda kwa kasi, injin na electromotor zinafanya kazi kwa pamoja; wakati magari yanapoenda taratibu, magari yanaendeshwa kwa electromotor peke yake.

Hivi sasa watafiti wa China wanajaribu kutumia nishati ya hewa ya hydrogen, ambayo inatumika kurusha maroketi. kitu muhimu cha teknolojia hiyo ni nishati ya betre, ambayo inabadilisha hewa ya hydrogen kuwa nishati ya umeme, na kuendesha magari kwa nguvu za umeme.