Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-21 20:55:11    
bidhaa za teknolojia zaongoza maisha mapya

cri

Bila shaka mmewahi kufikiria kuwa wakati michezo ya Olimpiki ya Beijing itakapofanyika mwaka 2008, kabla ya kuondoka nyumbani mnaweza kupata taarifa za moja kwa moja kuhusu mawasiliano barabarani kwenye mtandao wa Internet, na kuchagua njia bora ya kwenda kwenye uwanja fulani wa michezo; katika mapumziko ya adhuhuri, utaweza kupata habari za michezo kwenye simu ya mkononi na kuhifadhi matangazo ya moja kwa moja ya michezo kwenye simu yako? Bidhaa hizo za teknolojia zimeoneshwa kwenye maonesho ya tisa ya kimataifa ya teknolojia ya Beijing yaliyofungwa hivi karibuni. Bado kuna bidhaa nyingi nyingine za teknolojia kama hizo zinazohusiana na maisha ya kisasa.

Maonesho hayo yakiwa ni yenye athari kubwa kabisa nchini China, yamevutia mashirika zaidi ya 2000 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 20 zikiwemo Marekani, Ujerumani, Austria, Uholanzi na Russia. Miongoni mwa mashirika hayo, bidhaa zenye uvumbuzi wa teknolojia zilizotolewa na mashirika ya China zimewavutia watazamaji na wawekezaji wengi, na mfumo wa kisasa wa usimamizi wa mawasiliano barabarani ni moja kati ya bidhaa hizo. Ikilinganishwa na mfumo wa usimamizi unaotumika hivi sasa, mfumo huo mpya unaweza kuonesha hali halisi ya barabarani kwa haraka zaidi, na ubora wa picha ni mkubwa, na picha hizo zinaweza kuhifadhiwa kwa mitindo mingi. Aidha mtu yeyote ataweza kuingia kwenye mfumo huo na kupata taarifa moja kwa moja. Maneja mauzo wa kampuni iliyosanifu mfumo huo Bw. Yang Di Geng alisema:

"michezo ya Olimpiki itakapofanyika mjini Beijing mwaka 2008, mfumo mpya wa usimamizi kwa mawimbi ya picha za video utawekwa kwenye njia panda kubwa au sehemu muhimu kama majumba ya michezo. watazamaji au wachezaji wote wataweza kupata taarifa za moja kwa moja ya barabarani na kurahisisha safari zao."

Mbali na mfumo huo, simu za mkononi zenye televisheni au muziki pia inavutia watazamaji wengi. Kampuni ya teknolojia bila waya ya Dacheng ya Beijing ilionesha simu moja ya mikononi inayoweza kuhifadhi matangazo ya televisheni. Meneja wa idara inayoshughulikia wateja Bi. Xing Yue alieleza:

"Nia ya kampuni yetu ni kusanifu simu za mkononi zenye bei nafuu. Huduma ya televisheni kwenye simu za mkononi haina malipo. Ifikapo mwaka 2008, utaweza kutazama vipindi vyovyote kama unavyotaka."

Kutokana na uwezo mpya na bei rahisi, simu za aina hiyo zimewavutia watazamaji wengi. Mfanyakazi wa kampuni moja ya utangazaji ya Beijing Bi. Jiang Ling pia anataka kununua simu ya aina hiyo. Alisema:

"naona simu ya aina hiyo ni nzuri, sijawahi kuona simu kama hiyo, tena ina bei nafuu. Kama ikiwepo sokoni nikiiona huenda nitainunua."

Huenda watu wengi wanakumbuka kuwa katika filamu za Hollywood mchezaji anaweza kuingia kwenye kompyuta bila kutumia password yoyote kwa kutegemea sura ya uso wake tu. Hivi sasa teknolojia hiyo haipo kwenye televisheni tu. Kompyuta aina ya laptop iliyotolewa na Kampuni maarufu ya kampyuta ya China Lenovo inaweza kumtambua mtu kwa sura yake. Fundi mmoja wa kampuni hiyo Bw. Wang Hu alisema:

"hii ni teknolojia yetu ya uvumbuzi, si kama tu inaweza kuinua kiwango cha usalama, bali pia inaweza kukumbuka password na kuchukua nafasi ya uwezo kadhaa wa password."

Hivi sasa bei ya mafuta imeendelea kuongezeka, ili punguza matumizi ya mafuta na uchafuzi wa mazingira, nchi nyingi zinajitahidi kutafiti magari yasiyotumia mafuta. Katika maonesho hayo ya teknolojia, kamapuni ya usanifu wa magari ya Lee ya China ilionesha gari moja dogo inayotumia umeme na kuwavutia watazamaji wengi. Gari la aina hiyo ikichajiwa umeme kwa saa 5 linaweza kusafiri kilomita 260, na kwa kila kilomita mia moja linatumia umeme nyuzi 5.5. magari ya aina hiyo yameanza kuzalishwa kwa wingi na tayari kuuzwa sokoni, pia litaoneshwa kwenye maonesho ya magari ya kimataifa yatakayofanyika mwezi Oktaba huko Paris.

Miongoni mwa watazamaji, Bi. Xu Jiang alionesha kupenda sana gari la aina hiyo. Alisema:

"naona gari aina hii ni zuri, kwa kuwa matumizi yake ya pesa ni madogo, tena halina klachi, ni rahisi kuiendesha."

Ili kutimiza ahadi ya Olimpiki ya kijani, bidhaa nyingi za teknolojia zenye uwezo wa kusafisha hewa, kupunguza uchafuzi wa mazingira na kusaidia kuhifadhi mazingira ya viumbe zimeoneshwa kwenye maonesho hayo. Katika jumba la maonesho la Zhouguancun, kioo kinachoweza kujisafisha kilichosanifiwa na kampuni ya taasisi ya miradi ya teknolojia ya nano ya Zhongke kinafuatiliwa sana. Manejia mauzo wa kampuni hiyo Bw. Gai Wanguo alisema, kikilinganishwa na kioo cha kawaida, kioo cha aina hiyo kina uwezo maalum wa kujisafisha. Uwezo huo si kama tu umepunguza matumizi ya dawa za kusafisha kioo ambazo zinaharibu mazingira, bali pia umerahisisha kazi ya kusafisha kioo.

Bidhaa hizo zote za teknolojia zilizooneshwa kwenye maonesho ya tisa ya teknolojia ya kimataifa yatarahisisha maisha na kuinua kiwango cha maisha yetu.