Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-21 21:07:56    
Mapishi ya kupika nyama ya ng'ombe pamoja na vitunguu saumu

cri

Mahitaji:

Nyama ya paja la ng'ombe, kiasi kidogo cha vitunguu maji na tangawizi, vitunguu saumu, sukari kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, mchuzi wa soya kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, supu ya nyama mabakuli matano.

Njia:

1. tia nyama ya paja la ng'ombe kwenye maji moto, ichemshwe kwa ajili ya kuondoa damu ya nyama ya ng'ombe, ipakue halafu uiweke kwenye maji safi, tia vitunguu maji na tangawizi vichemshwe kwa dakika 40 mpaka ilainiki tia supu ya nyama, iendelee kuchemsha kwa dakika 20, ipakue na uikate iwe vipande.

2. kata vitunguu saumu iwe vipande, na uiweke kwenye maji kwa dakika 10 uvipakue na kukausha, halafu viweke kwenye vipande vya nyama ya ng'ombe.

3. koroga mvinyo wa kupikia, mchuzi wa soya na vipande vya vitunguu saumu, mimina kwenye nyama ya ng'ombe, korogakoroga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.