Reli ya TAZARA iliyojengwa kwa msaada wa serikali ya China ilianza kazi rasmi miaka 30 iliyopita. Hivi sasa reli hiyo inayoonesha urafiki mkubwa kati ya wananchi wa China na Afrika ina hali gani? Waandishi wetu wa habari wametuletea maelezo kutoka Tanzania wakisema, Reli ya TAZARA imejaa matumaini makubwa.
Katika kituo cha magari moshi cha Dar es Salaamu ambacho ni mwanzo wa Reli ya TAZARA, waandishi wetu wa habari wameona kuwa, kituo hicho kilichojengwa miaka 30 iliyopita kimekarabatiwa upya. Reli ya TAZARA inayoanzia Dar es Salaamu, mji ulio mashariki mwa Tanzania hadi Kapiri Mposhi, nchini Zambia ina urefu wa kilomita 1860.5. Mwezi Oktoba mwaka 1970, ujenzi wa reli ya TAZARA ulianza rasmi, ambapo sehemu zilizo pembeni mwa reli ni zenye utafauti wa kijioglafia. Serikali ya China ilitoa mikopo bila riba ya fedha za renminbi yuan milioni 988, na kuwatuma mafundi na wahandisi karibu elfu 50. Reli ya TAZARA ilizinduliwa na kuanza majaribio ya kazi mwezi Juni mwaka 1975.
Bwana Robert Mona ni mhandisi mkuu wa Tanzania katika reli ya TAZARA, akisifu reli hiyo alisema:
Reli hiyo imesaidia sana kutatua suala la uchukuzi katika mgodi wa shaba wa Zambia. Katika miaka hiyo iliyopita, kwenye sehemu zilizo karibu na reli hiyo, vimejengwa viwanda vingi vikiwemo viwanda vya kutengeneza karatasi na saruji, ambapo pia vimekuwa na vijiji vingi vidogo vidogo, wakazi wa huko wanategemea reli ya TAZARA kusafirisha mazao yao ya kilimo hadi Dar es Salaam na miji mingine. Ndiyo maana, Reli ya TAZARA imesukuma mbele maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Zambia, na kuinua kiwango cha maisha ya wakazi wanaoishi katika sehemu zilizo karibu na reli hiyo.
Mpaka sasa Reli ya TAZARA imesafirisha tani milioni 23 za bidhaa kwa jumla, na kuwasafirisha abiria milioni 37, ambayo imeonesha umuhimu wake mkubwa kwa maendeleo ya uchumi na ukombozi wa taifa wa Tanzania na Zambia hata kwa sehemu ya kusini mwa Afrika. Miaka 30 imepita tangu reli hiyo ianze kufanya kazi, hivi sasa reli hiyo iliyong'ara pia inakabiliwa na matatizo mbalimbali. Mkuu wa kikundi cha wataalamu cha reli cha China Bwana Du Jian alisema:
Hivi sasa hakuna fedha za kutosha kufanya ujenzi wa miundo mbinu ya reli hiyo, na kufanya utengenezaji wa kila siku wa zana na vifaa kwenye reli, ndiyo maana, nguvu ya uendeshaji wa reli hiyo bado haitoshi, na uwezo wake wa uchukuzi bado si wa kutosha, kwani vichwa vya magari moshi vingi si vya kutosha , na vinavyoweza kufanya kazi vipo 11 tu kwa hivi sasa.
Bwana Du aliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa, ili kutatua tatizo hilo, upande wa China umechukua hatua mbalimbali, kufanya ushirikiano wa kiteknolojia ni moja kati ya hatua hizo. Kuanzia mwaka 1976, kila baada ya miaka miwili, China,Tanzania na Zambia husaini mkataba wa ushirikiano wa kiteknolojia. Tokea mwaka 2002 mkataba huo wa awamu ya 11 uanze kutekelezwa, China imetoa msaada wa vifaa na zana za aina mbalimbali ambazo zimechangia sana uendeshaji wa reli ya TAZARA, hasa China imetoa msaada wa dola za kimarekani milioni 6 kuzisaidia kununua nishati ya mafuta na vipuri, na kutengeneza vichwa 6 vya magari moshi, hayo yote yametatua tatizo la dharura la idara ya Reli ya TAZARA?
Meneja wa ofisi ya mawasiliano na uchukuzi katika Idara ya Reli ya TAZARA Bwana Abdurahmani Saidi alisema:
Marafiki zetu wa China wameshiriki ujenzi na utengezaji wa reli hiyo, katika miaka mingi iliyopita wanaelewa sana matatizo yetu, na msaada wao wa kila mara umetusaidia sana.
Bwana Du Jian alisema, kama Reli ya RAZARA itapata fedha za kutosha, kuinua kiwango cha usimamizi na kupata zana na vifaa vipya, mustakbali wa reli hiyo utakuwa na matumaini makubwa.
|