Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-28 16:55:31    
Mapishi ya Doufu kwa sosi ya nyanya

cri

Mahitaji:

Tambi zilizotengenezwa kwa wanga, doufu gramu 200, sosi ya nyanya gramu 50, nyanya moja, nyama ya kuku gramu 100, njegere gramu 20, sukari kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, na maji ya wanga gramu 15

Njia:

1. osha nyama ya kuku, uikate iwe vipande, kata doufu na nyanya ziwe vipande.

2. tia maji kwenye sufuria yachemke, baada ya kuchemka tia vipande vya doufu kwenye sufuria na vichemke kwa dakika 1 vipakue.

3. tia mafuta kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 80, tia tambi zilizotengenezwa kwa wanga kwenye sufuria mpaka zichemke, kisha zipakue na uziweke kwenye sahani.

4. pasha moto tena, tia vipande vya nyama ya kuku, korogakoroga, halafu tia vipande vya nyanya na sosi ya nyanya, mimina maji kidogo, baada ya kuchemka, tia vipande vya doufu, njegere, chumvi na sukari, korogakoroga polepole, baada ya dakika 5, mimina maji ya wanga, korogakoroga uipakue na kuweka kwenye tambi. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.