Mkutano wa kwanza wa nchi zilizosaini "Mkataba wa kuhifadhi urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi" ulifanyika huko Paris, tarehe 27 Juni, ambapo nchi 45 zilituma wajumbe kuhudhuria mkutano huo. Huu ni mkutano wa kwanza wa nchi zilizosaini mkataba huo tangu mkataba huo uanze kazi.
Urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi unahusu aina mbalimbali za utamaduni wa jadi na nafasi za utamaduni zinazorithiwa na wananchi wa makabila mbalimbali vizazi kwa vizazi, ambazo zinahusiana karibu na maisha ya wananchi. Katika miaka ya hivi karibuni, jumuiya ya kimataifa inatilia maanani siku hadi siku uhifadhi wa urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi. Tarehe 17 Oktoba mwaka 2003, Mkutano wa 32 wa Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa ulipitisha "Mkataba wa kuhifadhi urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi". Mkataba huo unaona kuwa "kuna uhusiano wa kutegemeana kwa kuwepo pamoja kati ya urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi, urithi wa utamaduni ulio wa vitu halisi na urithi wa mali za kimaumbile", ingawa mchakato wa utandawazi wa uchumi duniani na mageuzi ya jamii umeanzisha mazingira mapya kwa makundi mbalimbali ya watu, lakini wakati huo huo umeufanya urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi ukabiliwe na tishio kubwa la kuharibiwa na kutoweka. Kuhifadhi urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi wa binadamu kumekuwa somo kuu linalopaswa kufuatiliwa kwa pamoja na binadamu wote.
Serikali ya China inatilia maanani sana uhifadhi wa urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi kama inavyofanya jumuiya ya kimataifa. Tokea mwaka 2000 Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa lianzishe kazi ya kuorodhesha "urithi wa utamaduni wa mdomoni na usio wa vitu halisi", China imefanya juhudi kutoa maombi, na tokea mwaka 2001 sanaa ya opera ya Kungqu, sanaa ya kinanda cha kale, sanaa ya Mukamu ya Xinjiang Uyghur na nyimbo za kienyeji za Changdiao za kabila la wamongolia nchini China zilifanikiwa kuorodheshwa na Shirika la UNESCO. Mwezi Agosti mwaka 2004, China iliidhinisha "Mkataba wa kuhifadhi urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi", na kuwa nchi ya 6 ya kusaini na mkataba huo. Baadaye wizara ya utamaduni ya China ilianzisha mradi wa kuokoa urithi wa utamaduni wa makabila madogomadogo na wa sehemu mbalimbali nchini, ambapo idara zinazohusika zilifanya mahesabu, uhifadhi na kutunga sheria na kanuni zinazohusika, kwani China ni mojawapo kati ya nchi zenye mali nyingi za urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi duniani, lakini hali ilivyo ya uhifadhi wa mali hizo haifurahishi. Wakati huo huo, zimeanzishwa kazi za kuokoa urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi wa aina mbalimbali uliopo sehemu mbalimbali nchini China, hivyo urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi umehifadhiwa vizuri nchini China.
Aidha, China inatilia maanani sana kufanya ushirikiano na jumuiya ya kimataifa katika uhifadhi wa urithi wa mali usio wa vitu halisi. Kwenye mkutano huo wa kwanza wa nchi zilizosaini "Mkataba wa kuhifadhi urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi" wa Shirika la UNESCO, China imeshiriki katika ugombeaji wa nchi wajumbe wa Kamati ya kiserikali ya uhifadhi wa urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi. Naibu katibu mkuu wa Baraza la serikali la China Bwana Chen Jinyu anayeongoza ujumbe wa China kuhudhuria mkutano huo alipotoa hotuba alisema, tokea China ijiunge na "Mkataba wa kuhifadhi urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi" mwezi Agosti mwaka 2004, China imepata manufaa katika kuongeza nguvu ya kuhifadhi urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi. Tarehe 10 Juni mwaka huu China kwa mara ya kwanza iliadhimisha "siku ya uhifadhi wa urithi wa utamaduni usio wa vitu halisi", ambapo wachina wameshiriki kwenye shughuli mbalimbali za maadhimisho hayo. Ukweli wa mambo umeonesha kuwa, serikali ikitetea kuenzi aina mbalimbali za utamaduni, kazi hiyo inasaidia kuongeza maisha ya utamaduni ya wananchi, kuvuta watalii, kuongeza nafasi za ajira, na muhimu zaidi kusaidia kuwahamasisha wananchi washiriki kwenye shughuli za kuhifadhi utamaduni wao wenyewe, ili kuongeza maelewano, uaminifu na heshima kati ya watu wenye desturi na mila tofauti, na kuhimiza ujenzi wa jamii yenye masikilizano.
Idhaa ya Kiswahili 2006-06-28
|