Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-06-30 16:27:33    
Israel imeahirisha mashambulizi dhidi ya ukanda wa Gaza

cri

    

Tarehe 29 serikali ya Israel iliamua kuahirisha mpango wake wa kuishambulia sehemu ya kaskazini ya Gaza jioni ya siku hiyo, uamuzi huo umeleta tumaini dogo la kutatua mgogoro kati ya Palestina na Israel kwa njia ya mazungumzo.

Jioni ya siku hiyo, waandisi wa habari walifika kwenye sehemu ya Nahal Oz kwenye mpaka kati ya Israel na ukanda wa Gaza. Ingawa waandishi hao walizuiliwa na askari wa Israel kwa kuambiwa kitu fulani kwa lugha ambayo hawakuielewa, lakini miungurumo ya mizinga iliwafanya watambue kuwa wapo kwenye kituo cha mizinga cha kushambulia Gaza. Katika siku hiyo ya tarehe 29 askari wa Israel walipiga mizinga zaidi ya 400, umeme kwenye sehemu ya kaskazini ya Gaza ulikatika na kuifanya sehemu hiyo iwe giza kabisa.

Kutokana na mpango, jioni ya tarehe 29 Israel ingeshambulia sehemu ya kaskazini ya Gaza. Vifaru karibu mia moja viliwekwa tayari kando ya msitu karibu na Gaza kwa kilomita kadhaa, na askari walikuwa tayari kufanya shambulizi wakati wote. Lakini jioni hiyo waandishi wa habari waliona kwamba hali ilikuwa tulivu kinyume na walivyofikiri, askari wawili wawili au watatu watatu walipumzika msituni, na vifaru vilivyopangwa kwa safu kadhaa vilikuwa vimewekwa kwenye mashamba ya ngano yaliyovunwa. Ingawa miungurumo ya mizinga ilikuwa ikisikika mara moja moja lakini waandishi wa habari kutoka nchi za ng'ambo walikuwa tayari kurudi nyumbani. Kwa sababu muda wa kufanya mashambulizi ulipokaribia, waziri mkuu Ehud Olmert na waziri wa ulinzi Amir Peretz walifanya uamuzi wa kusimamisha mashambulizi hayo.

Habari kutoka kwa mmoja wa wasuluhishi wa mgogoro kati ya Israel na Palestina alidokeza kwamba katika siku hiyo baada ya askari mmoja wa Israel kutekwa nyara, serikali ya Misri iliyofanya mazungumzo na viongozi wa Hamas iliiambia serikali ya Israel kuwa bado kuna uwezekano wa kutatua mgogoro kati ya Palestina na Israel kwa njia ya kidiplomasia, ikitumai Israel itatoa nafasi nyingine ya mazungumzo ya kumwokoa askari aliyetekwa nyara kwa amani. Serikali ya Israel ilikubali pendekezo hilo la Misri na kufanya uamuzi wa kuahirisha mashambulizi yake.

Wachambuzi wanaona kwamba tukio la kutekwa nyara kwa askari wa Israel ni mtihani mkubwa wa kisasa kwa serikali ya Ehud Olmert aliyeshika wadhifa kwa miezi miwili tu. Wapinzani wake wanaona kwamba kuondoka kutoka Gaza hakukuiletea Israel usalama wowote, hata rais wa Israel ambaye hakuwahi kutia mkono kwenye mambo ya serikali alikosoa kitendo cha upande mmoja cha Israel kwamba "hakina maana yoyote kidiplomasia".

Kuweza au kutoweza kutatua vizuri tatizo la kutekwa nyara kwa askari wa Israel ni pia mtihani kwa uwezo wa Ehud Olmert na hata kunahusisha maisha yake ya kisiasa. Kwa Ehud Olmert, kwanza lazima ahakikishe askari huyo "arudi nyumbani salama", la sivyo, juhudi zote zitakuwa bure. Lakini kumwokoa askari huyo kwa kufanya mashambulizi makubwa pengine licha ya kuleta hatari ya kuuawa kwa askari huyo, tena itasababisha "vita vya msituni" dhidi ya Israel na vifo vya raia wengi wasio na hatia, Israel pia itapata shinikizo kubwa kutoka kwa jumuyia ya kimataifa. Kutokana na hali hiyo serikali ya Ehud Olmert imeamua kuahirisha mashambulizi.