Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-03 18:50:51    
Nchi zilizoendelea zinatakiwa kuonesha nia ya kisiasa ili kuyawezesha Mazungumzo ya Doha yapate mafanikio

cri

Baada ya kufanyika pilikapilika kwenye majadiliano ya siku 3, wawakilishi wa nchi wanachama wa Shirika la biashara duniani wakiwemo mawaziri 60 wa biashara na kilimo, bado hawajaweza kufikia maoni ya pamoja kuhusu masuala muhimu ya mazungumzo hayo yaani masuala ya kilimo na kuruhusu bidhaa zisizo za kilimo kuingia kwenye soko, hivyo mazungumzo hayo ya ngazi ya juu ya shirika la WTO yalimalizika tarehe 1 Julai kwa siku moja kabla ya wakati uliowekwa. Mazungumzo ya Doha yameshindwa kwa mara nyingine tena.

Kabla ya hapo katibu mkuu wa Shirika la WTO Bwana Pascal Lamy alionya mara kwa mara kuwa, nchi wanachama wa shirika hilo zinapaswa kufikia maoni ya pamoja kabla ya mwishoni mwa mwezi Juni kuhusu masuala ya kilimo na kuziruhusu bidhaa zisizo za kilimo ziingie kwenye soko, ili kupata muda wa kutosha wa kushughulikia masuala mengine, ama sivyo lengo la kutimiza makubaliano ya biashara ya pande zote kabla ya mwishoni mwa mwaka huu litakabiliwa na hatari. Hivi sasa kikomo cha muda kimepita, lakini hali ya mvutano bado ipo, Bwana Lamy hana la kufanya, ila kukiri kuwa mazungumzo yameingia katika hali ya msukosuko.

Wachambuzi wanaona kuwa sababu kuu ya kuleta hali hiyo ni kuwa nchi zilizoendelea zilizo za wanachama wa Shirika la WTO hazina nia ya kisiasa katika kupunguza kwa kiasi kikubwa ruzuku za kilimo na kupunguza ushuru wa forodha wa mazao ya kilimo.

Kama inavyojulikana kwa wengi, lengo kuu la Mazungumzo ya Doha ni kupunguza vizuizi vya kibiashara, na kujenga mazingira ya kibiashara yaliyo ya haki zaidi ili kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa dunia nzima hasa nchi zinazoendelea. Kwa kuwa suala la maendeleo limesisitizwa zaidi, hivyo Mazungumzo ya Doha pia yameitwa kuwa ni "Mazungumzo ya maendeleo". Lakini tokea mazungumzo hayo yaanze mwaka 2001, watu wanaona kuwa wawakilishi wa nchi zilizoendelea kama vile Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya zimekwenda mrama juu ya ahadi zao za mwanzoni kwa "Mazungumzo ya maendeleo".

Katika muda mrefu uliopita nchi zilizoendelea zimetekeleza sera ya kutoa ruzuku kubwa na uungaji mkono mkubwa kwa kilimo, na kutoza ushuru mkubwa wa forodha kwa mazao ya kilimo; lakini nchi zinazoendelea zenye tija ya chini kwenye uzalishaji, kidhahiri, mazao yao ya kilimo hayana uwezo mkubwa wa ushindani kwenye soko la kimataifa. Nchi zinazoendelea zinadai vikali kubadilisha hali hiyo isiyo ya halali, ili kuyawezesha mazao yao ya kilimo yaingie kwa wingi kwenye soko la nchi zilizoendelea, na kujipatia nafasi nyingi za maendeleo. Lakini kutokana na sababu mbalimbali nchini na ulimwenguni, hasa Marekani kukaribia kwenye uchaguzi wa mwaka 2007, hata hivi sasa haijapania kufanya mageuzi kikamilifu juu ya kazi ya kilimo, hivyo si rahisi kwa mazungumzo ya Doha kuepukana na hali ya mvutano.

Tarehe 1 Julai nchi wanachama zaidi ya 100 wa Shirika la WTO zilitoa taarifa ya pamoja ikisema, Mazungumzo ya Doha yanapaswa kufuata jukumu lake la maendeleo, na kuweka mkazo katika kuzingatia mahitaji na maslahi ya nchi zinazoendelea. Mazungumzo hayo yakitaka kupata maendeleo, kazi ya dharura ni kuondoa ruzuku za kilimo ambazo zimepotosha vibaya shughuli za biashara, ambapo mazao ya kilimo ya nchi zinazoendelea yamezuiliwa vibaya, hali hii inatishia maisha ya wakulima maskini wapatao milioni mia kadhaa. Taarifa hiyo inasisitiza kuwa kufanikiwa kwa Mazungumzo ya Doha ni lazima kutegemea mchango mkubwa wa nchi zilizoendelea, nchi zilizoendelea zinapaswa kubeba wajibu, wakati nchi zinazoendelea zinapenda kuchangia mazungumzo hayo kwa kadiri iwezekanavyo.

Katibu mkuu wa Shirika la WTO Bwana Lamy alisema, ingawa mazungumzo hayo ya ngazi ya juu hayajaweza kupata maendeleo, lakini nchi wanachama wa shirika hilo wanaunga mkono kithabiti kukamilisha mazungumzo hayo kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, ili kutimiza lengo la kufikia makubaliano ya biashara kwa pande zote.