Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-03 19:15:50    
Vivutio maarufu vya utalii kwenye sehemu zilizoko kando za Reli ya Qinghai-Tibet

cri

Reli ya kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet, China imezinduliwa kuanzia tarehe 1 Julai mwaka huu, reli hiyo imejengwa kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet wenye mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari. Watalii wanaopanda garimoshi kwenye reli hiyo, wanaweza kuvutiwa na vivutio vya mazingira ya kimaumbile ya Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet, pia wanaweza kuhisi utamaduni wa kabila la watibet wenye harufu nzito ya kidini.

Katika sehemu zilizoko kwenye kando mbili za Reli ya Qinghai-Tibet kuna vivutio vingi. Katika sehemu ya mwanzo ya Reli ya Qinghai-Tibet, kuna mji wa kale wa uwanda wa juu Xining, ambapo Msikiti wa Tar ulioko kwenye bonde la Mlima Lianhua katika wilaya ya Huangzhong unajulikana zaidi. Msikiti wa Tar ni sehemu alikozaliwa Lama mkuu Zongkeba ambaye ni mwanzilishi wa madhehebu ya Geru ya dini ya kibudhaa ya kitibet, pia ni kituo cha shughuli za dini ya kilama cha sehemu ya kaskazini magharibi ya China. Jengo kuu la msikiti huo ni Jengo la Dajinwa ambalo kuta zake ni za rangi ya kijani na paa la jengo ni la rangi ya dhahabu, jengo hilo linalong'ara zaidi katikati ya majengo mengine yaliyojengwa zamani ambayo yameonesha sanaa za makabila ya wahan na watibet yenye mtindo wa kipekee.

Watalii wakifunga safari kutoka Xining kuelekea Ziwa Qinghai lililoko kaskazini mashariki mwa Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, wataona kwa furaha mandhari nzuri ya ziwa hilo ambalo ni kubwa zaidi lenye maji chumvi nchini China. Ziwa la Qinghai lina mwinuko wa mita 3260 kutoka usawa wa bahari, ambalo maji yake yanayoonekana ya rangi ya kijani ni safi sana. Toka mwezi wa Aprili hadi Julai kila mwaka, ndege wanaohamahama wapatao laki kadhaa hukusanyika kwenye kisiwa kilichoko kwenye ziwa hilo, ambapo ndege hao wanaorukaruka angani au wanaochezacheza ziwani, ama kupumzika kwenye ufukwe?milio yao husikika mbali sana, hali ya huko kweli inawavutia sana watalii.

Watalii wakifunga safari kutoka Ziwa Qinghai kwa kilomita 800 watafika Germu, mji uliojitokeza kwenye jangwa. Kwenye sehemu hiyo kuna Ziwa Chalhan ambalo ni ziwa kubwa zaidi la maji chumvi nchini China, maji ya ziwa hiyo yanang'ara kwa rangi nzuri ajabu kutokana na chembechembe za chumvi. Katika siku yenye hali ya hewa nzuri, usawa mkubwa wa ziwa huonekana kama kioo kikubwa chenye miujiza ambacho kinaweza kutoa mionzi ya rangi ya dhahabu au rangi buluu kabisa, hata wakati fulani inaibuka hali ajabu ya mazigazi yanayobadilikabadilika. Na kuna sehemu yenye hali ya kijiografia ya Yadan yaani vilima virefu vya udongo, sehemu hiyo ina urefu wa kilomita karibu mia moja na upana wa kilomita 10 kadhaa, hali ya kijiografia ya sehemu hiyo ina sura ya aina mbalimbali, ambayo ni kivutio cha ajabu katika sehemu ya magharibi ya China.

Maana ya neno Kokoxili la kimongolia ni "msichana mrembo", sehemu ya Kokoxili iko kaskazini magharibi ya Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, katikati ya Milima Kunlun na Milima Tanggula, eneo la sehemu hiyo ni kilomita elfu 83 za mraba, na mwinuko wake kutoka kwenye usawa wa bahari ni zaidi ya mita 4600, sehemu hiyo ni moja ya hifadhi kubwa za maumbile ya ngazi ya juu, ambapo kuna wanyama pori wengi zaidi, watalii wakipita kwenye sehemu ya Kokoxili isiyo na wakazi, wataweza kuona paa wengi wa kitibe wanarukaruka kwa furaha kwenye sehemu hiyo, pia wanaweza kuona msururu mkubwa wa magari yanayosafirisha vifaa kwenda Lhasa, mji mkuu wa mkoa wa Tibet.

Mto Tuotuo ni chanzo kikuu cha Mto Changjiang, chanzo hicho kilitoka Mlima Gladandong kwenye Milima Tangula wenye mwinuko wa mita 6621 kutoka kwenye usawa wa bahari. Upande wa kusini magharibi ya Mlima barafu wa Gladandong ni Mlima wa barafu Jianggendiru, na sehemu ya mkia wa mto huo barafu ni "Msitu wa minara ya barafu" wenye kilomita 2. "Msitu wa minara ya barafu" unaonekana kuwa na sura ya nchi ya aina mbalimbali, jinsi ulivyo ni kama ulichongwa kwa dhahabu na jade. Zaidi ya hayo, hali ya nchi ya aina mbalimbali za daraja barafu, ziwa barafu na ulimi barafu pia inaonekana hapa na pale katika sehemu hiyo, na mlima wa barafu una mvuto mkubwa kwa watalii.

Wakipita kwenye mlango wa Mlima Tanggula, watalii wanaweza kuona mbuga kubwa sana ya Qiangtang iliyoko kaskazini ya Tibet. Kwenye mbuga huo sehemu Shenzha ambayo ni sehemu wanakokusanyika ndege wengi, na Ziwa Shuanghu ambapo kuna wanyama pori wengi. Na siku ya mashindano ya mbio za farasi huko Naqu pia inawavutia sana watalii.

Na Ziwa Namucuo ni ziwa lenye maji chumvi ambalo liko kwenye mwinuko mkubwa zaidi kutoka usawa wa bahari kuliko mengine duniani, mwinuko huo ni mita 4,718, ziwa hizo ni ziwa kubwa zaidi miongoni mwa maziwa matatu makubwa ya yenye hali ajabu mkoani Tibet. Waumini wa dini ya kibudha ya kitibet wanaopiga magoti kwa mwili nzima na kusonga mbele kuabudu Buddha wanaonekana hapa na pale kwenye sehemu hiyo.

Na Mji wa Lhasa ni kituo cha mwisho cha Reli ya Qinghai-Tibet, Kasri la Budara mjini Lhasa ni kasri lililojengwa kwenye sehemu yenye mwinuko wa juu zaidi duniani, ambalo inajulikana duniani kwa thamani yake kubwa ya kihistoria na kisanii. Ndani ya kasri hilo vimehifadhiwa vitu vingi vya kale na michoro kwenye kuta vyenye thamani kubwa.

Na reli yenyewe kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet ni reli inayowavutia watu. Watalii wakipanda garimoshi kwenye njia hiyo ya reli wataona Daraja la Mto Sancha ambalo ni daraja kubwa la juu zaidi lenye urefu wa mita zaidi ya 50 na Daraja kubwa la Mto Qingsui ambalo umbo lake linafanana na upinde wa mvua, linasimama kwenye sehemu isiyo na wakazi kwenye sehemu ya Kokoxili. Aidha, watalii pia wanaweza kuona Handaki la Mlima Kunlun ambalo ni refu zaidi kuliko mengine duniani, na udongo wa handaki hilo ni udongo ulioganda kuwa barafu kwa miaka mingi, aidha wanaweza kuona mahandaki mengine ya udongo ulioganda kwenye sehemu hiyo ya uwanda wa juu.