Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-04 15:59:43    
Sekta mbalimbali nchini China zahimiza udhibiti wa matumizi ya nishati

cri

Udhibiti wa matumizi ya nishati nchini China umekuwa moja ya sera za kimsingi za taifa, siyo tu kwamba udhibiti wa matumizi ya nishati umekuwa wazo la umma, bali pia maeneo yale yanayotumia nishati kwa wingi yakiwemo majengo na viwanda, yanafuatilia udhibiti wa matumizi ya nishati, hivi sasa sekta mbalimbali nchini China zinajitahidi kuvumbua teknolojia ya udhibiti wa matumizi ya nishati, na zimepata ufanisi katika harakati hizo.

Tokea miaka mingi iliyopita, majengo yanatumia nishati kwa wingi. Pamoja na kupanuka kwa soko la nyumba, ujenzi wa majengo unapamba moto hivi sasa nchini China, majengo ambayo ujenzi wake unakamilika yanakaribia mita za mraba bilioni 2 kwa mwaka, ambayo 97% ya majengo hayo yanatumia nishati kwa wingi. Katika miaka ya karibuni serikali ya China inajitahidi kudhibiti matumizi ya nishati ya majengo, kuhimiza uvumbuzi na uenezaji wa teknolojia inayodhibiti matumizi ya nishati, hivi sasa aina mpya ya majengo yenye uwezo wa kudhibiti matumizi ya nishati yanajengwa kwa wingi. Mengi ya majengo ya aina hiyo yanatumia teknolojia ya kutunza joto ndani kwa kuta za majengo, kutumia teknolojia ya kupunguza joto za ndani kwa mitambo inayopooza hewa badala ya viyoyozi vinavyotumia nishati kwa wingi, na baadhi ya majengo mapya yamekuwa na mfumo wa kutoa mwangaza wakati wa usiku kwa kutumia nishati ya mwangaza wa jua na zana za kutumia maji yaliyotumika baada ya kusafishwa. Majengo mapya kwenye makazi yanayojulikana kwa "Zhongqiao", mkoani Hubei sehemu ya kati ya China, yanatumia teknolojia mbalimbali za kisasa za kudhibiti matumizi ya nishati, majengo hayo yanapendwa sana na wateja. Kiongozi anayeshughulikia majengo ya makazi hayo wa kampuni ya ujenzi wa majengo, Bw. Ding Kongshi alisema, wazo la kujenga majengo yanayodhibiti matumizi ya nishati lilitokana na agizo la serikali, alisema,

"Tulipojenga majengo ya makazi ya 'Zhongqiao', tulitekeleza sera na maagizo ya kudhibiti matumizi ya nishati yaliyotolewa na wizara ya ujenzi na serikali katika ngazi mbalimbali, na kukuza uwezo wa majengo wa kuhifadhi mazingira na kudhibiti matumizi ya nishati. Kwa mfano, katika kutoa mwangaza usiku kwenye sehemu za umma na kuhifadhi bustani ndogo kwenye makazi, tulitumia vifaa vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa. Tulijitahidi kadiri tulivyoweza."

Kitu muhimu zaidi katika kukuza uchumi kwa kudhibiti matumizi ya nishati ni kudhibiti matumizi ya nishati ya viwanda. Hivi sasa viwanda vya aina mbalimbali vya China vinarekebishwa kuwa vya kudhibiti matumizi ya nishati, licha ya kuzingatia kusafisha na kutumia maji yaliyotumika na takataka za viwanda, viwanda hivyo pia vinatekeleza wazo la kudhibiti matumizi ya nishati katika mchakato wa uzalishaji bidhaa, hata kutoka mwanzo kabisa wa kuchagua aina za mali-ghafi na vifaa vinavyotumika viwandani. Kampuni ya Yihua ya Hubei ni mashuhuri sana miongoni mwa kampuni za kazi za kemikali nchini China, ambayo inajulikana zaidi baada ya kutumia teknolojia ya kubadilisha unga wa makaa ya mawe kuwa mabonge, ambao ni vigumu kuunganishwa pamoja. Mhandisi mkuu wa kampuni hiyo Bw. Yang Xiaoqin alimweleza mwandishi wetu wa habari teknolojia hiyo huku akichukua unga wa makaa ya mawe na kumwonesha.

"Unga wa makaa ya mawe baada ya kuchanganywa kwa aina ya makaa ya mawe ya lignite, na kukutengenezwa kuwa mabonge ya makaa ya mawe, ambayo yanaweza kuwaka ndani ya tanuri la kiwandani, njia hii inapunguza matumizi ya fedha kwa kiasi kikubwa, vile vile yanapunguza gharama za uzalishaji mali na kuokoa makaa ya mawe bora."

Hivi sasa viwanda mbalimbali nchini China vinafanya utafiti kuhusu teknolojia hiyo inayoendana na hali zao halisi. Katika mji wa Nanyang, mkoani Henan ulioko sehemu ya kati ya China, kuna kampuni moja ya spiriti inayojulikana kwa jina la "Tianguan", ambayo katika miaka ya karibuni inazalisha gesi ya asili kwa kutumia maji taka yanayotolewa katika uzalishaji wa spiriti, hivi sasa familia laki 2 zilizo karibu na kiwanda hicho zinatumia nishati ya gesi ya asili, ambayo haina uchafuzi kwa mazingira.

Ili kudumisha maendeleo endelevu ya uchumi na jamii, China imeweka lengo la kupunguza 20% ya matumizi ya nishati katika uzalishaji mali kuliko zamani katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano ijayo.

Idhaa ya kiswahili 07-04