Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-04 16:39:44    
Msomi wa India asema kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet kutaleta fursa za kibiashara kati ya China na India

cri

Reli ya Qinghai-Tibet yenye urefu wa kilomita 2,000 inayopita kwenye uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet ambao ni uwanda wa juu wenye mwinuko mkubwa zaidi duniani imezinduliwa rasmi tarehe 1 Julai mwaka huu. Mtaalamu maarufu wa elimu ya kimkakati wa India, ambaye pia ni mhariri mkuu wa gazeti la The Indian Express Bw. Raja Mohan hivi karibuni alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, utekelezaji wa sera ya kimkakati ya kuendeleza sehemu ya magharibi ya China hasa kujenga na kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet utahimiza maendeleo ya uhusiano wa kibiashara wa sehemu ya mpakani kati ya China na India, wala siyo kuleta tishio kwa India.

Bw. Raja Mohan aliyewahi kuitembelea Tibet kwa mara mbili alisema:

"Maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya China na India yamehimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye sehemu ya magharibi ya China na India. Mpango wa China kuendeleza sehemu ya magharibi umeleta fursa nyingi za ushirikiano kati ya sehemu hiyo ya China na sehemu ya kaskazini mashariki ya India."

Bw. Raja Mohan pia alipendekeza kuwa, China na India zinapaswa kuunganisha mifumo ya barabara kati ya sehemu ya magharibi ya China na sehemu ya kaskazini mashariki ya India. Alisema:

"China na India zinapaswa kuunganisha mifumo ya barabara kwenye sehemu za mpakani. Kama tutaichukua Tibet, China kuwa kituo kimoja kwenye mfumo wa mawasiliano wa reli barani Asia, basi tutaweza kuunganisha mifumo ya mawasiliano ya nchi mbalimbali za Asia. Mifumo hiyo itarahisisha mawasiliano ya biashara kati ya sehemu ya magharibi, China na sehemu ya Asia kusini, hasa India. Maendeleo ya ushirikiano kati ya China na India yataleta mustakabali mzuri kwa maendeleo ya sehemu ya magharibi ya China na sehemu ya kaskazini mashariki ya India."

Bw. Raja alisisitiza kuwa, India haichukulii uzinduzi wa reli ya Qinghai-Tibet kama tishio kwake, maendeleo ya uchumi wa China na India yameleta fursa mpya kwa maendeleo ya uchumi duniani. Alisema:

"India haichukulii uzinduzi wa reli ya Qinghai-Tibet kuwa ni tishio kwake, kituo cha mwisho cha reli hiyo ni mji wa Lhasa, reli hiyo itarahisisha mawasiliano ya biashara kati ya sehemu ya magharibi ya China, na sehemu ya kaskazini na Calcutta ya India. Naamini kuwa, China na India hazipaswi kuwa na uadui kwa sababu kuna nafasi kubwa kwa maendeleo ya nchi hizo mbili barani Asia. Japokuwa nchi hizo mbili zina ushindani katika sekta kadhaa, lakini kama ushindani huo unaweza kuendelea vizuri hautaleta wasiwasi. Nchi hizo mbili zinaweza kutatua masuala yatakayotokea katika ushindani kati yao kwa kufanya mazungumzo ya kisiasa.

Kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet kutaleta fursa nyingi za uwekezaji

Reli ya Qinghai-Tibet itaunganisha pamoja soko la mkoa wa Tibet, mkoa wa Qinghai na sehemu nyingine nchini China, ambapo shughuli zenye umaalum wa uwanda wa juu ambazo ni pamoja na utalii, dawa, uchimbaji madini, utengenezaji wa mazao ya kilimo na mifugo, sanaa za mikono na viumbe vya uwanda wa juu zitaingia katika mzunguko mzuri wa maendeleo endelevu, na kuleta ongezeko jipya la uchumi kwenye sehemu ya uwanda wa juu wa huko.

Wakati mikoa ya Tibet na Qinghai inapojitahidi kuboresha mazingira ya uwekezaji, baadhi ya wawekezaji wanaojua namna ya kutumia fursa za uwekezaji wameanza kufanya ukaguzi na kutafuta fursa za biashara kwenye sehemu zilizo kando za reli ya Qinghai-Tibet.

Kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet pia kutaunganisha sehemu za vivutio vya utalii vilivyoko kando za reli hiyo. Na shughuli za mikahawa na utalii za huko pia zitaingia katika kipindi cha usitawishaji. Miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba ya kila mwaka ni majira mazuri kwa utalii mkoani Tibet, wakati huo hoteli zote za mjini Lhasa hujaa na watalii. Kutokana na takwimu zisizokamilika, baada ya kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet, kwa wastani idadi ya watalii 4000 watakaotembelea Lhasa itaongezeka kwa siku, hivyo mji huo unapaswa kujenga hoteli nyingine zaidi ya 13 ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la watalii.

Kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet pia kutahimiza maendeleo ya shughuli nyingine za huko, ambazo ni pamoja na tiba na dawa za kitibet, uchimbaji madini, usindikaji mazao ya mifugo na kilimo, sanaa za mikono za kikabila na viumbe vya uwanda wa juu, wataalamu wamekadiria kuwa shughuli hizo zitaleta ongezeko kubwa kwa uchumi wa huko.

Aidha kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet pia kutarahisisha uchukuzi wa mboga. Kwa sababu Tibet inategemea sana kuagiza mboga kutoka sehemu nyingine, hivyo bei yake ya mboga huwa ni kubwa sana. Kwa upande mwingine, mkoa wa Tibet una mwangaza mwingi wa jua, hivyo kuwekeza mkoani humo kujenga mabanda ya plastiki na nyumba za vioo za kupanda mboga kutaleta ufanisi mzuri.

Kuzinduliwa kwa reli ya Qinghai-Tibet pia kutahimiza ujenzi wa miji wa sehemu ya Qinghai- Tibet. Kutakuwa na nafasi nyingi za uwekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo ujenzi wa miundo mbinu kama vile mawasiliano ya barabara, nishati, mawasiliano ya simu, utoaji wa maji, utoaji wa gesi asilia utoaji wa joto na miundo mbinu ya majengo ya umma kama vile hospitali, shule, maduka na benki.

Idhaa ya kiswahili 07-04