Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-05 19:01:20    
Jamii inapaswa kufanya juhudi kuwaepusha watoto wasiathiriwe na dawa za kulevya

cri
Tarehe 26, Juni ni Siku ya 19 ya kupambana na dawa za kulevya duniani, na kauli mbiu ya mwaka huu ni "dawa za kulevya si mchezo wa kujiburudisha kwa watoto". Je, ni kwa nini kauli mwaka huu inafuatilia matumizi ya dawa za kulevya kwa watoto? Je hali ya hivi sasa ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwenye sehemu ya Asia na Pasifiki ikoje? Mwandishi wetu wa habari alimhoji Bw. Akira Fujino ambaye ni mkuu wa Kituo cha Asia Mashariki na sehemu ya Pasifiki kwenye Ofisi ya udhibiti wa dawa za kulevya na kudhibiti uhalifu ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia kauli mbiu siku ya kimataifa ya dawa za kulevya ya mwaka huu Bw. Akira Fujino anasema:

"Watoto hudadisi vitu vipya, na tunapaswa kutoa onyo kwao kabla hawajapata fursa ya kutumia dawa za kulevya. Hivi sasa mtandao wa Internet ni njia rahisi kuwapatia watoto ujuzi usio sahihi, hivyo kuna haja ya kutoa mafunzo na onyo kwao kwa wakati. Kutokana na hali hiyo, kauli mbiu ya siku ya kimataifa ya kupiga marufuku dawa za kulevya ya mwaka huu inafuatilia sana athari inayoletwa na dawa za kulevya kwa watoto."

Bw. Fujino akizungumzia sababu ya watoto ya kutumia dawa za kulevya anasema:

"Naona familia na jamii ni sababu mbili muhimu. Kutalikiana kwa wazazi na hali ngumu ya kiuchumi ya familia zinawafanya watoto watumie dawa za kulevya, na watoto hao husema kuwa walikuwa pamoja na marafiki zao walipotumia dawa za kulevya kwa mara ya kwanza. Hivyo wazazi, walimu na jamii zinapaswa kuwajibika na kuathiriwa na dawa za kulevya kwa watoto."

Lakini Bw Fujino pia alisisitiza kuwa, jambo muhimu zaidi kwa jamii ni kufanya juhudi za kuwalinda watoto, ili kuwaepusha wasiathiriwe na dawa za kulevya, na Ofisi ya udhibiti wa dawa za kulevya na kinga ya uhalifu ya Umoja wa Mataifa imechukua hatua kadhaa?

"Tumefanya majaribio katika nchi kadhaa, ili kuwasaidia watoto walioathiriwa vibaya na dawa za kulevya. Maofisa wetu walioko nchini Philippines na Thailand waliwatafuta watoto wanaotumia dawa za kulevya, na kushirikiana na serikali za huko kuwapatia misaada. Kazi yetu imepata uungaji mkono wa mashirika yasiyo ya kiserikali, na tulianzisha shughuli mbalimbali za matangazo yanayohusu kupinga matumizi ya dawa hizo."

Bw. Fujino alisema, Umoja wa Mataifa utaweka mkazo kutoa mafunzo kwa watoto kuhusu hatari ya dawa za kulevya huku ukiweka mkazo katika kutoa mafunzo kwa wazazi wa watoto hao. Aidha, Umoja wa Mataifa na idara zinazohusika za nchi mbalimbali zitaanzisha ushirikiano kupambana na vyanzo vya dawa za kulevya, ili kuzuia watoto wasitumie dawa za kulevya.

Kazi muhimu ya Kituo cha Asia Mashariki na sehemu ya Pasifiki kwenye Ofisi ya udhibiti wa dawa za kulevya na kinga ya uhalifu ya Umoja wa Mataifa ni kutoa misaada ya fedha na teknolojia kwa kinga na udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya kwenye sehemu ya Asia Mashariki na sehemu ya Pasifiki. Akizungumzia hali ya suala la dawa za kulevya katika sehemu ya Asia na Pasifiki, Bw. Fujino anasema:

"Nchi nyingi zilizoko kwenye sehemu ya Asia na Pasifiki zinakabiliwa na hali mpya ya matumizi na magendo ya dawa za kulevya yanayotengenezwa kwa njia ya kikemikali. Uzalishaji wa mipopi kwenye sehemu ya "pembetatu ya dhahabu"unapungua, wakati dawa za kulevya zinazotengenezwa kwa njia ya kikemikali zinafuatiliwa na watu siku hadi siku. Kutokana na hali hiyo, kazi yetu muhimu ni kufuatilia matumizi, uzalishaji na magendo ya dawa ya Heroin, wakati huo huo tunapaswa kufuatilia aina mpya ya dawa za kulevya zinazotengenezwa kwa njia ya kikemikali."

Kwenye mahojiano hayo, Bw. Fujino alisifu mafanikio ya China katika kupiga marufuku dawa za kulevya?akisema, serikali ya China si kama tu inakatisha vyanzo vya utoaji wa dawa za kulevya, pia inachukua hatua zenye mafanikio kukabiliana na maambukizi ya Ukimwi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Akizungumzia kazi ya kupambana na dawa za kulevya ya China, Bw. Fujino anasema:

"Serikali ya China imekuwa ikijifunza uzoefu wa nchi nyingine katika kupambana na dawa za kulevya, na China inapaswa kuendelea na kazi hiyo?kutekeleza mpango wa kupunguza mahitaji ya dawa za kulevya, kutilia mkazo matibabu, kuwaponesha watu wanaotumia dawa za kulevya?na kuwasaidia wajiunge tena na jamii. Idara za utekelezaji wa sheria na idara zinazohusika zinapaswa kushirikiana na idara za afya kuanzisha kwa pamoja shughuli za kupambana na dawa za kulevya?na mashirika yasiyo ya kiserikali na ya kiraia pia yanaweza kushiriki kwenye shughuli hiyo."

Idhaa ya Kiswahili 2006-07-05