Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-05 19:18:12    
Mapishi ya vipande vya samaki

cri

Mahitaji

Samaki aina ya tuna, yai moja, kiasi kidogo cha sukari, chumvi, M.S.G, wanga, mvinyo wa kupikia na uyoga wa mweusi

Njia

1. ondoa vitu vyote vyilivyo ndani ya tumbo la samaki, katakata nyama ya samaki iwe vipande vipande, koroga pamoja na chumvi, ute wa yai na wanga, kasha uweke kwenye jokofu. Weke uyoga wa mweusi ndani ya maji ya moto, halafu pakua na aweke kwenye sahani.

2. tia mafuta kwenye sufuria yachemke mpaka yawe na joto la nyuzi 30, tia vipande vya samaki, korogakoroga kasha vipakue.

3. tia maji kidogo na chumvi kwenye sufuria halafu tia vipande vya samaki, korogakoroga baada ya kuchemka, tia mvinyo wa kupikia, sukari, M.S.G, korogakoroga polepole tia maji ya wanga, mimina mafuta ya moto, vipakue na uviweke kwenye sahani. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.