Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-06 18:51:25    
Wageni waeleza picha waliyoipata kuhusu wanachama wa Chama cha kikomunisti cha China

cri

Chama cha kikomunisti cha China ni chama tawala nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni, wageni wengi wamekuwa wanakuja China kufanya kazi, kusoma au kutembelea, ambapo wamewasiliana moja kwa moja na Wachina wa kawaida wakiwemo wanachama wa chama cha kikomunisti cha China. Katika makala hii, wageni kadhaa walieleza maoni yao kuhusu chama hicho tawala cha China na wanachama wake.

Katika miaka ya 30 ya karne iliyopita, mwandishi wa habari wa Marekani Bw. Edgar Snow alipokutana kwa mara ya kwanza na wanachama wa Chama cha kikomunisti cha China huko Yanan, kaskazini magharibi mwa China aliona kuwa, watu hao ni miongoni mwa Wachina hodari kabisa. Katika kitabu chake maarufu kiitwacho "nyota nyekundu wanaoimurika China" (Red Star over China), alitoa maoni yake kuhusu wanachama wa chama hicho kama akisema: "vijana hao wana uchangamfu mkubwa usiodidimia, wanashikilia matumaini mpaka siku ya mwisho, wana imani kubwa kwa mapinduzi inayowashangaza watu, na imani waliyo nayo ni kama moto mkali. Vijana hao kamwe hawakubali kushindwa ama mbele ya nguvu ya watu, ama mbele ya dunia ya maumbile, walipokabiliana na changamoto ya kujitolea muhanga."

Sasa ni miaka zaidi ya 70 imeshapita, Mmarekani mwingine Bw. Bill Milewski ambaye anafanya kazi katika kampuni moja ya mtandao wa Internet hapa mjini Beijing, alielezea maoni yake juu ya wanachama wa chama cha kikomunisti cha China. Alimwambia mwandishi wa habari wa Radio China Kimataifa kuwa kwa ujumla wana ushujaa wa kukabiliana na shida. Wanachapa kazi kwa makini na kwa kila wawezalo, wakikabiliwa na shida hawarudi nyuma hata kidogo. Mmarekani huyo alifurahi kushirikiana na wanachama hao wa chama cha kikomunisti cha China katika kazi. Alisema (sauti 1) "Katika kampuni yetu ya mtandao wa Internet, wanachama wa chama cha kikomunisti cha China ni vijana, ambao wengi walikuwa wamehitimu masomo muda si mrefu uliopita. Wana sifa nzuri ya kitaaluma, pia wana busara. Mimi nafurahi sana kushirikiana nao kuendeleza kampuni yetu, pia nafurahi kufanya kazi na wanachama wa namna hii wa chama cha kikomunisti cha China."

Bw. Bill mwenye umri wa miaka 43 ameishi hapa nchini China kwa miaka kumi. Alisema yeye alizaliwa katika familia ya wafanyakazi yenye watu zaidi ya 10, ambao wana maoni tofauti ya kisiasa yenye mgongano mara kwa mara. Alisema nchini Marekani, hakuna chama hata kimoja kama chama cha kikomunisti cha China, ambacho kimefanikiwa kuondoa tatizo la chakula kwa idadi kubwa ya wananchi, kuwapa makazi na kuwahakikishia maisha. Hayo ni mafanikio ya kujivunia. Bw. Bill aliongeza kuwa awali Bw. Snow alipotembelea Yanan, kiongozi wa chama cha kikomunisti cha China Bw. Mao Zedong alikuwa na umri wa miaka 43, huku kiongozi mwingine Bw. Zhou Enlai alikuwa na umri wa miaka 37 tu. Lakini wao walikuwa viongozi awamu ya kwanza wa chama hicho, na moyo wao wa mshikamano na kutokubali kushindwa uliwavutia vijana kutoka sehemu mbalimbali za China wajiunge na chama hicho. Na miaka zaidi ya 10 baadaye, chama hicho kilifanya mwujiza wa kuanzisha China mpya. Alisema mpaka sasa wanachama wa chama cha kikomunisti cha China bado wanashikilia moyo wa namna hii.

Bibi Helena Darcq aliyetoka Ufaransa anafanya kazi katika chombo cha habari mjini Beijing. Kijana huyo alieleza picha aliyoipata kuhusu wanachama wa chama cha kikomunisti cha China akisema, "Msiniambie nani anatoka chama cha kikomunisti, naweza kuwatambulisha, kwamba bila shaka ni wale wapole, wakarimu na wanaochapa kazi kwa makini." Alisema (sauti 2) "Nashika zamu ya usiku mara kwa mara. Mwenzangu mmoja wa kike ambaye ni mkubwa kuliko mimi ananisaidia sana, pia anafanya kazi kwa makini bila uzembe. Anaongea nami mara kwa mara, akiniuliza vipi maisha na kazi yangu huko Beijing. Naona yeye pia anawasaidia wengine. Baadaye nikaambiwa kuwa yeye ni mwanachama wa chama cha kikomunisti cha China. Awali sikutambua nani ni mwanachama wa chama hicho, nikagundua baadaye kuwa kumbe wenzangu wengi ni wanachama wa chama hicho."

Subo ni mwanafunzi kutoka Jamhuri ya Mongolia, ni mwanafunzi wa shahada la pili ya taaluma ya diplomasia kwenye Chuo kikuu cha umma cha China. Ameishi nchini China kwa miaka mitano. Katika kipindi hicho, alikuwa anawasiliana na wanachama wengi wa chama cha kikomunisti cha China, wakiwemo wanafunzi wenzake, walimu na marafiki zake. Bw. Subo alisema, mwanzoni alidhani wanachama wa chama tawala cha nchi kubwa wangeonesha majivuno makubwa zaidi kuliko wengine, lakini hali halisi si ya namna hii. Aliona kuwa, wanachama hao si kama tu ni wapole, bali pia wanapenda kuwasaidia wengine wenye shida.

Kijana huyo alikumbusha siku za mwanzo alipokuja China, alisema kuwa alikuwa hajui vizuri lugha ya Kichina, ilikuwa vigumu kwake kufuata masomo darasani. Wakati huo wanafunzi wenzake na walimu ambao ni wanachama wa chama cha kikomunisti cha China walimpa uungaji mkono na msaada.

Alisema (sauti 3) "Kwa mfano nilipotunga insha kwa Kichina nilikumbwa na matatizo ya lugha, ambapo walinisaidia sana. Kutokana na misaada yao, kila mara niliweza kukamlisha vizuri insha."

Katika miaka ya hivi karibuni, wageni wengi wamekuja China kufanya kazi, kusoma au kuishi, ambapo walipata ufahamu mwingi kuhusu wanachama wa chama cha kikomunisti cha China. Katika mahojiano na wageni hao, mwandishi wetu wa habari aliona kuwa, walieleza picha inayofanana kuhusu wanachama hao, kwamba wao ni wenye matumaini, wanaofanya juhudi na kujitahidi kutimiza matumaini yao. Walisema ni kutokana na wanachama hao, chama cha kikomunisti cha China kimepata nguvu kubwa na uhai mkubwa.