Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-10 15:40:35    
Reli ya kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet, China

cri

Reli ya kutoka mkoa wa Qinghai hadi mkoa wa Tibet, China imezinduliwa kuanzia tarehe 1 Julai mwaka huu. Reli hiyo imejengwa kwenye Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet wenye mwinuko mkubwa kutoka usawa wa bahari. Ili kuwawezesha watalii wanaopanda garimoshi wapate raha na usalama kwenye safari yao, idara husika zilifanya usanifu maalum wa garimoshi linalopita kwenye reli hiyo.
Ili kutatua tatizo la upungufu wa oksijeni ndani ya garimoshi kwenye reli hiyo iliyojengwa kwenye uwanda wa juu, ndani ya garimoshi kuna mifumo miwili ya kutoa oksijeni, mfumo mmoja unatoa oksijeni kwenye behewa, yaani kupitia hewa ndani ya mfumo wa mseto wa viyoyozi kudumisha kiwango kati ya asilimia 23.5 na asilimia 25 ya oksijeni katika kila behewa, ili kukidhi mahitaji ya oksijeni ya watalii wengi kwenye behewa; na mfumo mwingine ni mirija miwili inayoweza kufungwa kwenye viti vya watalii, kama watalii wanahitaji kupata oksijeni nyingi, wanaweza kuvuta oksijeni kupitia mirija hiyo, ili kukwepa athari mbaya ya upungufu wa oksijeni kwenye uwanda wa juu.
Kwenye sehemu iliyo karibu na mlango wa Mlima Tangula wenye mwinuko wa zaidi ya mita 5000 kutoka usawa wa bahari, matabaka ya mawingu yako chini sana, hivyo radi inapita mara kwa mara kwenye mawingu hayo, ambayo yanaweza kuteketeza majani na miti kwenye ardhi, na kutishia vibaya usalama wa majengo yaliyoko kwenye ardhi. Ili kukinga radi hiyo inayoviringika kwenye ardhi", ndani ya magarimoshi ya abiria kwenye Reli ya Qinghai-Tibet, vimefungwa vyombo vya umeme vyenye uwezo wa kuvumilia shinikizo na kukinga umeme, ili kulinda usalama wa kutegemeka wa magarimoshi wakati yanapopita kwenye sehemu ya Uwanda wa Juu.
Mazingira ya viumbe kwenye Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet ni rahisi sana kuharibiwa, hivyo kazi ya uhifadhi wa mazingira inatakiwa kufanyika kwa makini kwenye kiwango cha juu. Ili kuyawezesha magarimoshi yasitoe majitaka au takataka kwenye Reli ya Qinghai-Tibet, vyoo kwenye magarimoshi hayo vyote ni vifaa visivyo na hewa ambavyo vinakusanya takataka zote ndani, wakati garimoshi likifika kituo cha mwisho, takataka hizo zinachukuliwa na gari maalum ili kuzipeleka mahali pa kuzishughulikia. Na kwenye magarimoshi pia kuna mashine zinazoshughulikia takataka nyingine ili kuhakikisha mazingira ya njia ya reli yasichafuliwe na takataka.
Na kwenye Uwanda wa juu, mionzi ya jua ni mikali sana pamoja na upepo wa mchanga huvuma mara kwa mara, hayo yote yanaweza kuathiri vibaya matumizi ya magarimoshi kwa miaka mingi na uwezo wa kuyaendesha kwenye reli ya uwanda wa juu. Ndiyo maana rangi iliyopakwa nje ya garimoshi inapaswa kulingana na mahitaji maalum ya uendeshaji wake kwenye Reli ya Qinghai-Tibet. Baada ya kufanyiwa majaribio kwa mwaka mmoja, rangi iliyopakwa nje ya garimoshi haikuharibika, ambayo uwezo wake wa kukinga mionzi ya jua, upepo wa mchanga na joto kali unalingana kabisa na matakwa.
Na ili kupunguza madhara ya mionzi mikali ya jua dhidi ya abiria, kwenye vioo vyenye matabaka mawili vya madirisha ndani ya magarimoshi ya abiria yanayoingia mkoani Tibet pia kumebandikwa plastiki ya kuzuia mionzi kali ya jua, madirisha yote yanafungwa kabisa, baada ya kuchujwa, mionzi ya jua ndani ya garimoshi inalingana kimsingi na mionzi ya jua katika mazingira ya tambarare.
Ndani ya garimoshi linaloendeshwa kwenye Reli ya Qinghai-Tibet, kila behewa limewekwa dirisha moja la kutoka nje kwa dharura, ili abiria waweze kukimbia nje wakati wa kutokea hali ya dharura. Hata ndani ya vyoo, kuna kitufe chekundu cha kuonesha hali ya hatari, wakati abiria akikumbwa na hali ya dharura ya taabu au hatari, anaweza kubonyeza kitufe hicho, basi mhudumu ndani ya garimoshi atakuja mara moja kumsaidia kuondoa taabu.
Ndani ya garimoshi linaloendeshwa kwenye Reli ya Qinghai-Tibet, viti wanavyokaa abiria vinawawezesha abiria waone raha, na hali kadhalika kwa vitanda vilivyoongezwa upana kuliko vingine vya magarimoshi yanayoendeshwa kwenye reli nyingine nchini China. Kwenye garimoshi pia kuna vyoo vinavyotumiwa na walemavu. Na kutokana hali ya kutikisa vikali kwa garimoshi linaloendeshwa kwenye Uwanda wa juu, kila behewa limefungwa mfumo kamili wa kupunguza mtikisiko, tena kutumia teknolojia mpya ya kuzuia makelele. Ndani ya behewa la kulia chakula, pia kuna televisheni za aina mpya, sehemu ya baa, ambapo abiria wanaweza kujiburudisha kwa raha starehe katika safari yao ya kuelekea Lhasa.
Zaidi ya hayo watalii wakipanda garimoshi linaloendeshwa kwenye Reli ya Qinghai-Tibet, watapita kwenye vituo mbalimbali vya garimoshi vyenye majina mbalimbali tofauti. Majina hayo yalitokana na lugha ya kitibet, kimongolia, kihan, na kila jina lina maana yake halisi, na umaalum wa lugha za makabila madogo umewawezesha watu waone hali ya ajabu iliyo ya kuwavutia. Kwa mfano, Kituo cha "Couna", maana yake ya kitibet ni "Ziwa jeusi", Kituo cha Toutouhe, maana yake ya kimongolia ni "Mto mtulivu".

Idhaa ya kiswahili 2006-07-10