Tarehe 13 Shirika la Chakula Duniani lilitoa ripoti ya "hali ya njaa duniani mwaka 2006" ikisema njaa na utapiamlo sio tu vinaathiri akili za watu, bali pia vitaathiri maendeleo ya uchumi wa nchi mbalimbali.
Ripoti inasema, katika kipindi cha miongo kadhaa, ingawa hali ya njaa imepungua kidogo lakini bado iko mbali na malengo ya maendeleo ya milenia, kama tukiondoa maendeleo yaliyopatikana nchini China, idadi ya watu wenye utapiamlo imeongezeka kwa milioni 18 duniani kuanzia mwaka 1900.
Imefahamika kwamba hivi sasa kila mwaka watoto milioni sita wanakufa kutokana na njaa au magonjwa yanayohusiana na utapiamlo, na kiasi cha watoto milioni 100 wanashindwa kwenda shule kutokana na umaskini, na watoto wanaoweza kuendelea na masomo pia wanashindwa kusoma kwa makini kutokana na ukosefu wa lishe bora. Kwa hiyo njaa inaathiri watoto kusoma na kushindwa kwenda shule.
Ripoti inasema katika kipindi ambapo wanawake wanapokuwa wajawazito na watoto wanaponyonyeshwa ni kipindi muhimu kwa ukuaji wa akili wa binadamu, ukosefu wa lishe katika kipindi cha watoto unachelewesha ukuaji wa akili na athari hiyo haiwezi kufidiwa baadaye, kisha watoto hao watakuwa uwezo duni wa kusoma au kuwa taahira. Ripoti imetoa taarifa ya uchunguzi uliofanyika katika nchi zaidi ya 60, ikisema kwamba watu wa nchi hizo kutokana na kukosa madini ya joto tu kiwango cha akili kinakuwa cha chini ikilinganishwa na watu wa nchi nyingine. Kadhalika, ripoti pia inasema kwamba kutokana na njaa watu wazima wanashindwa kufanya kazi kama kawaida na wanawatumbukiza watoto wao kwenye janga la njaa. Mzunguko mbaya kama huo maendeleo ya taifa hakika yataathirika. Kwa hiyo kila nchi ni lazima ijitahidi kukwepa hali hiyo.
Ripoti hiyo imefafanua uhusiano kati ya hali ya lishe na uwezo wa kusoma na maendeleo ya nchi husika, ikisema kwamba kuboresha lishe na kuinua uwezo wa kusoma hakika kutainua afya na elimu ya wananchi na kuwafahamisha namna ya kupata mazoea bora ya kimaisha na chakula, namna ya kujikinga na maradhi na kuhakikisha afya bora ili kufanya kazi kwa uvumbuzi kwa elimu waliyopata. Na yote hayo yataweza kuleta ufanisi mkubwa kwa taifa. Kutumia nyenzo za watu hodari na kumwezesha kila mtu atumie akili vya kutosha ni msingi wa ustawi wa taifa. kwa msingi wa ufahamu huo ndipo nchi mbalimbali zitaweza kujenga utaratibu wa kuhimiza mzunguko bora kati ya lishe na masomo bora na kurithisha kizazi hadi kizazi.
Aidha, ripoti inasema, hali ya mtu fulani ya lishe na masomo kwa kawaida huamua hali ya familia yake katika uchumi na maisha, na wastani wa hali ya lishe na masomo ya kitaifa huamua mustakbali wa taifa hilo. Lakini jambo linalosikitisha ni kwamba hivi sasa hapa duniani hali ya njaa inayoathiri afya na masomo na maendeleo ya taifa inaonekana kila mahali.
Katibu mkuu wa Shirika la Chakula Duniani Bw. Sheila Sisulu kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, masomo ni njia ya uhakika ya kutatua tatizo la njaa. Elimu sio tu inamaanisha kusoma na kufanya hesabu, bali pia licha ya kuwapatia uwezo wa kimsingi nje ya masomo wanapata afya, elimu ya lishe na kuwawezesha kuzikimu familia zao. Serikali za kila nchi ni lazima zizingatie athari ya njaa kwa uwezo wa kusoma na kuchukua hatua za haraka kuwasaidia watoto wenye njaa na kuanzisha mzunguko bora kati ya lishe na masomo na kuweka mpango husika wa kipindi kirefu
Idhaa ya kiswahili 2006-07-14
|