Mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 8 uliingia siku ya pili tarehe 16. Nyaraka zilizopitishwa kwenye mkutano katika siku hiyo kwa uchache zilikuwa 11, ambazo zinahusu masuala ya kimataifa ya kupambana na ugaidi, kupinga ufisadi, biashara ya kimataifa, hifadhi ya haki-miliki ya kielimu na maendeleo ya uchumi ya barani Afrika, licha ya mada tatu zilizothibitishwa kabla ya kufanyika mkutano huo, ambazo ni kuhusu usalama wa nishati, udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na elimu. Hata masuala kuhusu majaribio ya makombora ya Korea ya kaskazini, suala la nyukilia la Iran na migogoro kati ya Lebanon na Israel pia yamekuwa mambo yanayojadiliwa kwenye mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 8 wa siku hiyo. Wachambuzi wanasema, ni nadra kuona hali ya namna hiyo, ambayo mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 8 kujadili mambo mengi kama safari hiyo. Hivi sasa kundi la nchi 8 linafuatilia mambo mengi ya kimataifa.
Siku hiyo asubuhi viongozi wa nchi 8 walikuwa na majadiliano kuhusu mada zilizowekwa za usalama wa nishati, udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na maendeleo ya elimu, na kupitisha nyaraka 3 za pamoja. Katika nyaraka kuhusu usalama wa nishati, viongozi wa kundi la nchi 8 walitoa wito wa kutaka nchi zenye rasilimali nyingi za nishati duniani, nchi zilizo kama vituo vya kati kwenye njia ya usafirishaji nishati pamoja na nchi zinazoagiza nishati zianzishe uhusiano wa kiwenzi, kuboresha mazingira ya uwekezaji wa eneo la nishati, kuinua ufanisi wa matumizi ya nishati, kuhimiza matumizi ya aina nyingi za nishati, kuhifadhi usalama wa miundo-mbinu muhimu ya nishati na kuzisaidia nchi zinazoendelea kuimarisha utoshelezaji wa nishati wa nchi zinazoendelea.
Taarifa ya pamoja kuhusu maendeleo ya elimu, inatoa mapendekezo kwa nchi mbalimbali kuanzisha ushirikiano katika kuinua ubora wa elimu ya msingi, kujenga mfumo wa elimu ya kisasa wenye ufanisi wa kazi ili kutoa misaada kwa maendeleo ya elimu ya nchi zinazoendelea hususan kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo. Taarifa ya pamoja kuhusu udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza inataka nchi mbalimbali kuboresha mfumo wa udhibiti wa magonjwa wa kuambukiza duniani, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na kubuni mpango mwafaka wa kudhibiti maambukizi ya maradhi baada ya kutokea kwa maafa ya kimaumbile.
Kutokana na athari za kupamba moto hivi karibuni kwa migogoro ya kisilaha kwenye eneo la mashariki ya kati na tukio la Korea ya kaskazini kufanya majaribio ya makombora, viongozi wa kundi la nchi 8 kwa nyakati tofauti walipitisha taarifa mbili za pamoja kuhusu hali ya mashariki ya kati na suala la kuenea kwa silaha za nyukilia.
Katika taarifa kuhusu hali ya mashariki ya kati, viongozi wa nchi 8 wamesema mgogoro wa unaoikabili sehemu ya mashariki ya kati kwa hivi sasa umesababishwa na watu wenye msimamo mkali wanaojaribu kuharibu utulivu wa sehemu hiyo, taarifa inataka watu hao waache mara moja vitendo vyao vya mashambulizi vinavyoharibu utulivu wa sehemu hiyo. Taarifa hiyo pia inataka Israel ijizuie kadiri iwezavyo, na isitende kitendo chochote kinachoweza kuharibu utulivu wa sehemu hiyo, wala isisababishe vifo vingi zaidi vya wakazi wa huko. Taarifa inatarajia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litahakikisha kuwa maazimio ya No. 1559 na No. 1680 kuhusu suala la Lebanon yanatekelezwa kwa pande zote.
Taarifa ya pamoja kuhusu usambazaji wa silaha za nyukilia, viongozi wa nchi 8 wanaunga mkono azimio la No. 1695 lililopitishwa hivi karibuni na baraza la usalama kuhusu majaribio ya makombora ya Korea ya Kaskazini, taarifa hiyo inafuatilia sana tukio hilo na kulilaani vikali ikiona kuwa vitendo hivyo vya Korea ya Kaskazini vinatishia utulivu na usalama wa sehemu hiyo.
Wachambuzi wanaona kuwa kushughulikia mambo mengi zaidi kwa mkutano wa wakuu wa kundi la nchi 8, kunaonesha uwezo na madhumuni ya mkutano wa kundi la nchi 8 kwa sasa yanabadilika polepole. Kadiri hali ya dunia inavyobadilika, mkutano wa nchi 8 unaanza kushughulikia mambo mengi zaidi ya maeneo mengi yakiwemo ya siasa, mkakati wa kivita na usalama, hususan kwenye mkutano wa mwaka huu.
|