Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-18 18:44:06    
Vivutio vya reli ya Qinghai-Tibet

cri
1) Reli iliyojengwa kwenye uwanda wa juu kwenye mwinuko mkubwa zaidi kutoka usawa wa bahari duniani

Reli ya Qinghai-Tibet inatoka mji wa Xi Ning mkoani Qinghai, na kuishia mji wa Lhasa, mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Tibet, ina urefu wa kilomita 1956, reli hiyo ilijengwa kwenye uwanda wa juu wenye mwinuko wa wastani wa zaidi ya mita elfu 4 kutoka usawa wa bahari, na bonde la mlima wa Tanggula ambalo ni sehemu yake ya juu ina mwinuko wa mita 5072, reli hiyo inasifiwa kuwa "reli iliyo karibu zaidi na anga".

2) Reli iliyojengwa kwenye uwanda wa juu na kwa umbali mkubwa kabisa kupita kwenye sehemu yenye udongo ulioganda

Reli ya Qinghai-Tibet inapita sehemu ya kilomita 550 yenye udongo ulioganda ardhi inayoganda kwa miaka mingi duniani. Reli hiyo ni mfano wa kuigwa wa kutatua tatizo la udongo ulioganda kwa kutumia kwa pande zote hatua mbalimbali katika sekta ya ujenzi wa mradi mbalimbali kwenye sehemu yenye udongo ulioganda.

3) Handaki refu zaidi duniani kujengwa kwenye uwanda wa juu wenye udongo ulioganda, yaani Handaki la Fenghuo

Handaki la Fenghuo liko kwenye reli ya mkoani Qinghai, sehemu yenye mwinuko wa mita 4905 kutoka usawa wa bahari na lina urefu wa mita 1338, handaki hilo nzima liko sehemu yenye udongo ulioganda kwa miaka mingi. Handaki hilo lililojengwa kwenye uwanda wa juu wenye mwinuko mkubwa zaidi wa kutoka usawa wa bahari na kwenye udongo ulioganda daima, limesifiwa kuwa "handaki refu la kwanza duniani".

4) Handaki refu zaidi duniani lililojengwa kwenye uwanda wa juu wenye udongo ulioganda, yaani handaki la Mlima wa Kunlun

Handaki la mlima wa Kunlun liko mkoani Qinghai katika Reli ya Qinghai-Tibet, kwenye mwinuko wa zaidi ya mita 4600 kutoka usawa wa bahari na lina urefu wa mita 1686. Handaki hilo liko kwenye sehemu yenye udongo ulioganda kwa miaka mingi, hali yake ya kijiografia ni ya utatanishi, na hali yake ya mazingira ya kimaumbile ya sehemu hiyo ni mbaya. Handaki hilo linapita kwenye sehemu yenye mipasuko mingi, sehemu ya mlango wa kuingia handaki hilo ina barafu nene chini ya ardhi, na sehemu yake ya kutoka nje ina mawe mengi, kwa hiyo handaki hilo limejengwa kwenye sehemu ya uwanda wa juu yenye utatanishi wa kijiolojia.

5) Kituo cha garimoshi cha Tanggula kilichoko kwenye mwinuko wa juu kabisa kutoka usawa w bahari duniani

Kituo cha garimoshi cha Tanggula kimejengwa katika sehemu yenye udongo unaoganda kwa miaka mingi kwenye mwinuko wa mita 5068 kutoka usawa wa bahari. Eneo la kituo hicho ni mita za mraba elfu 77. Kituo hicho kina njia tatu za reli, ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya abiria na mizigo. Kituo cha Tanggula ni jengo lenye mtindo wa kabila la watibet, kwenye kituo hicho kuna uwanja wa kuangalia mandhari na paa la kuzuia mvua, ambapo watalii wanaweza pia kujiburudisha kwa mandhari ya sehemu hiyo, na kupiga picha au video mandhari ya "paa hilo la dunia".

6) Tuta la kutandika reli lililo kwenye uwanda wa juu wenye mwinuko wa juu kutoka usawa wa bahari duniani

Huko kaskazini ya wilaya ya Anduo, sehemu ya Naqu, Tibet kuna tuta la reli ya Qinghai-Tibet lililo kwenye mwinuko wa mita 4704 kutoka usawa wa bahari. Sehemu ya Anduo ni sehemu iliyotandikwa reli ambayo iko kwenye mwinuko mkubwa kabisa kutoka usawa wa bahari duniani.

7) Daraja la Qingshuihete, daraja refu kabisa lililojengwa kwenye uwanda wa juu wenye udongo ulioganda

Daraja la Qingshuihete liko katika sehemu ya Kekexili isiyo na wakazi lenye mwinuko wa mita 4500 kutoka usawa wa bahari duniani, urefu wa daraja hilo ni kilomita 11.7. Hiyo ni sehemu ambayo paa wa Kitibet na punda-pori wa Kitibet wanyama wengine pori wenye thamani wa uwanja wa juu huhamahama, hivyo upinde wa daraja hilo umekuwa njia ya kupita kwa wanyama pori wanaohamahama kwa uhuru.

8) Garimoshi lenye mwendo kasi zaidi duniani kwenye reli iliyojengwa kwenye uwanda wa juu wenye udongo ulioganda

Baada ya ujenzi wa Reli ya Qinghai-Tibet kukamilika na kuanza kutumika, mwendo wa garimoshi linaloendeshwa kwenye sehemu yenye udongo ulioganda unaweza kufika kilomita 100, na kwenye sehemu isiyo ardhi inayoganda utafikia kilomita 120, huu ni mwendo wa kasi kabisa duniani kwa garimoshi linalopita kwenye reli iliyojengwa kwenye uwanda wa juu wenye udongo ulioganda.