Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2006-07-19 19:38:39    
Idadi ya watu wanaojifunza kichina katika nchi za nje yaongezeka siku hadi siku

cri
Confucius alikuwa mwanafalsafa, mwanasiasa na mwelimishaji maarufu wa China. Hadi sasa vyuo vilivyopewa jina la Confucius vimeanzishwa katika nchi na sehemu 36 duniani, na idadi yake imefikia 80. Kwenye Mkutano wa kwanza vya vyuo vya Confucius, wajumbe 400 kutoka nchi na sehemu 38 duniani walijadili kwa pamoja ufundishaji wa lugha ya kichina duniani. Mjumbe wa taifa wa China Bibi Chen Zhili alisema, kadiri China na nchi mbalimbali duniani zinavyozidi kuwasiliana, ndivyo lugha ya kichina inavyozidi kutumiwa na kufuatiliwa zaidi.

Takwimu kutoka serikali ya China zinaonesha kuwa, hadi sasa watu zaidi ya milioni 30 wanajifunza lugha ya kichina katika nchi za nje, na masomo ya lugha ya kichina yameanzishwa kwenye vyuo vikuu 2,500 katika nchi 100. Uingereza, Thailand na Indonesia zimeweka lugha ya kichina kwenye utaratibu wa elimu, na idadi ya wanafunzi wanaojifunza kichina nchini Korea ya Kusini na Japan imezidi milioni 1. Aidha, katika sehemu za Latin Amerika, Mashariki ya Kati na Afrika idadi hiyo pia inazidi kuongezeka kwa haraka.

Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya masomo ya kichina katika nchi za nje, China ilianzisha mashirika ya kueneza lugha ya kichina katika nchi za nje kuanzia mwaka 2002, na kuyataja rasmi mashirika hayo kuwa ni "vyuo vya Confucius" kuanzia mwaka 2004. Hadi sasa vyuo 86 vya Confucius vimeanzishwa katika nchi na sehemu 36, na mashirika 99 kutoka nchi 38 yametoa maombi ya kuanzisha vyuo vya Confucius.

Tangu Shirika la ushirikiano wa maendeleo la China na Marekani lililoko huko New York, Marekani lianzishwe mwaka 1926 lilianza kufanya juhudi za kueneza lugha ya kichina. Naibu mkuu wa shirika hilo Bi. Jia Nan alipozuru China mwaka 1972, ambapo hakuweza kutarajia kuwa hivi sasa vyuo 2,400 vya Marekani vinaweza kuanzisha masomo ya kichina.

Bi Jia Nan alisema, "Ni shughuli yenye maana kujifunza lugha ya nchi yenye ongezeko la kasi la uchumi na idadi kubwa ya watu. Naona fahari kubwa kuwa chuo cha kwanza cha Confucius kitakachoanzishwa nchini Marekani kitawekwa kwenye Shirika la ushirikiano wa maendeleo la China na Marekani."

Chuo cha Poitiers cha Ufaransa kimeshirikiana na Chuo cha Nan Chang kuanzisha Chuo cha Confucius. Mkuu wa chuo hicho Bw. Alain Mignot alidokeza kuwa "Chuo cha Confucius kimekuwa sehemu ya kufanya maingiliano na ushirikiano kuhusu elimu, utamaduni, uchumi na biashara. "

Bw. Antonio Guiraraes Rodrigues ambaye ni mkuu wa chuo cha Miniho cha Ureno alisema, mawasiliano kati ya Ureno na China yana historia ndefu. Bw. Rodrigues alisema, "Watu wa Ureno hawapendi kukosa fursa ya kufanya biashara na wachina, na wanapaswa kufahamu mawazo ya wachina, na kuondoa vikwazo vya mawasiliano kati yao."

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi cha Kenya Bw. Jorge Margo alisema "kuanzishwa kwa chuo cha Confucius si kama tu ni mnara wa historia katika mawasiliano ya utamaduni na maendeleo kati ya China na Afrika, pia imetoa fursa nyingi zaidi kwa vijana kutokana na hali ya utandawazi wa uchumi duniani."

Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2005, nchi na sehemu zaidi ya 190 zimewekeza vitega uchumi nchini China, na China imeidhinisha kuanzishwa kwa mashirika zaidi ya laki 5 yanayowekezwa na nchi za nje, na mashirika zaidi ya elfu 30 ya China yameanzisha shughuli zake nchi za nje.

Mwezi Machi mwaka huu, Gazeti moja la Marekani lilieleza kuwa, China itaanzisha vyuo 100 vya Confucius duniani kabla ya mwaka 2010, na kusema kuwa vyuo hivyo vitaisaidia China kupata marafiki wengi na kuwa na athari kubwa zaidi duniani.

Inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2010, idadi ya watu wanaojifunza lugha ya kichina duniani itafikia milioni 100, na walimu milioni 4 wa lugha ya kichina watahitajika. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Fu Dan cha China Bw. Wang Shenghong alisema, "Hivi sasa China imekuwa ikipata maendeleo makubwa, ufundishaji wa lugha ya kichina unaonesha kuwa China inafuatiliwa sana na dunia."

Idhaa ya Kiswahili 2006-07-19